JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 624
- 934
Kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi kifungu cha 58 kifungu kidogo cha 1, sanduku la kura linatakiwa kutengenezwa kwa namna ambayo inamruhusu mpiga kura kuweza kuweka karatasi ya kura bila kuweza kuitoa
Kifungu kidogo cha pili kinasema kuwa kabla mchakato wa kupiga kura haujaanza, msimamizi kwenye kila kituo anatakiwa kuonesha sanduku la kura lililo tupu kwa watu waliopo katika eneo hilo kihalali ili waweze kuthibitisha kuwa halina kitu chochote
Baada ya hapo anatakiwa kulifunga sanduku hilo na kuliwekea utepe au muhuri ambao utalizuia kufunguka bila kukata utepe huo na kuliweka tayari kwa ajili ya kupokea karatasi za kura huku likiwa limefungwa
Karatasi ya Kupigia Kura
Kifungu cha 59 kinazungumza kuhusu namna karatasi ya kura inavyotakiwa kuwa
a) Inatakiwa kujumuisha yafuatayo;
- Jina kamili la mgombea
- Picha ya mgombea ya hivi karibuni, iliyopigwa ndani ya kipindi cha miezi mitatu
- Kifupisho au logo ya chama cha siasa kinachomfadhili mgombea husika
b) Inatakiwa kuwa na uwezo wa kukunjika
c) Inatakiwa kuambatana na nakala yenye namba ya mfululizo(serial number)