Fahamu kuhusu muigizaji N!xau maarufu kama Bushman

esc343

JF-Expert Member
Apr 17, 2014
354
580
IMG_7232.jpg


N!xau [HASHTAG]#Toma[/HASHTAG] ni mzaliwa wa Namibia katika kabila la San ambao wengi ni Bushman. Alikuwa hajui miaka yake. Kabla ya kuanza kuigiza, alikuwa hajui chochote kuhusu maisha ya kisasa “ Modern Civilization “. Alikuwa ashawahi kuona wazungu wa tatu tu kabla ya kuigiza na alikuwa hajui thamani ya fedha. Mshahara wake wa kwanza kupitia filamu ya “ The Gods Must Be Crazy” 300$ ulipeperushwa na upepo.

Alikuwa ametoka kwenye utamaduni ambao haukujua thamani ya fedha wala kuelewa matumizi yake. Ila baadae aliweza kutumia hela yake kujenga nyumba ya matofali yenye maji na umeme.

Filamu zake ziliingiza mapato mengi sana kwenye box office. Baada ya kustaafu uigizaji, alirudi Namibia na akawa mkulima wa Mahindi na maharage, alikuwa mfugaji wa ng’ombe ila hawakuzidi 20. Gazeti la “ the independent “ linaeleza kuwa alifanya hivyo kwa sababu alikuwa hajui kuhesabu zaidi ya 20.

Alifariki Julai 5 mwaka 2003. Julai mosi alienda kuwinda na hakurudi, familia yake iliupata mwili wake siku nne baadae. Ameacha mke mmoja na watoto 6.

John snow ️.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom