Fahamu kuhusu matumizi ya OverDrive (OD) kwenye gari automatic

Kwa ufahamu wangu OD ikiwa off yaani taa kwenye dashboard inawaka fuel consumption inakuwa low na speed inafika hadi 130 km/h na fuel rotation haipandi kuzidi 3 lakini OD ikiwa ON yaani taa imezima fuel consumption lazima itakuwa kubwa sbb umeweka extra power na hapo speed ni hadi unamaliza dashboard na rotation inafika 5.
USHAURI: usiendeshe gari OD ikiwa ON kwa maeneo ya mjini sbb ni wastage of fuel na kama upo long safar weka OD ON kama una overtake tu na si vinginevyo.

MKUU upo kinyume kisheria ya gari wakati inatumika dashboard inatakiwa isiwe na taa hata moja sasa kaangalie vizuri wakati unaendesha ukiona taa ya O/D inawaka angalia Gari itakuwa haimalizi gear lakini ikizima utaona gari ni nyepesi sana chunguza upya mkuu
 
Magari mengi taa ya OD inapaswa kuwaka Kama Ikimaanisha Over drive iko Off, Na iwe Imezima ikamaanisha OverDrive iko On.

Sasa nimegundua wengi wakiona taa inawaka huminya Button ili izime Kumbe ndio wameweka kwnye OD.
MKUU haupo sawa hata kidogo Kwa faida nitakueleza ukipenda ila Kwa hasara endelea kudanganya wana JF ila mi nimeshuka Kwenye gari yako safiri salama
 
Ngoja niwachambulie kuhusu taa kuwaka na overdrive yenyewe:
Kuhusu taa:
Taaa yoyote inapowaka wakati engine iko on, humaanisha kuwa kuna hitilafu inabidi irekebishwe. Unapoweka switch on kwenye dashboard, taa mbali mbali huwaka na unapowasha gari, taa zote huzima. Mathalani taa ya airbag ikiwaka au ya betri ikiwaka au ya oili ikiwaka, au ya over drive ikiwaka, inaonesha kuwa eneo hilo linashida na inabidi ufanye kitu ili taa hiyo ijizime.

Kuhusu over drive:
Tuchukue mfumo wa gari ya manual ili kuelezea maana ya over drive. Gari za zamani za manual zilikuaw na gear mwisho nne, lakini kutokana na kukua kwa teknolojia, wakagundua mtoto wa gearbox ambaye uki mu engage, gari inahama kutoka kutumia gearbox ya kawaida kwenye gear namba nne, na kuanza kutumia mtoto wa gear box ambaye kwenye gari ya manula itakuwa gear namba tano hadi sita kwa baadhi ya magari lakini kwenye gari ya automatic unapotumia mtoto wa gearbox ina maana unatumia gear ya over drive!
Kwa hiyo ili engine izunguke kidogo kwenye speed kubwa na ili uweze kuokoa mafuta, kwa gari ya manual utatumia gear namba tano, na kwe gari ya auto utatumia over drive. Kwa hiyo unapozima gear ya over drive, inamaana unaacha kutumia mtoto wa gearbox na hivyo gari itatumia gear kubwa kubwa, na hilo husababisha engine kuzunguka sana na mafuta kwenda kwa wingi. Kwa kifupi unapoendesha gari, taa ya over drive inabidi iwe imezimika wakati wote isipokuwa kwa vipindi maalum ambapo gari itahitaji nguvu ya ziada kama vile kuovertake au kupandisha milima.

Umeeleza vizuri kama unajua lakini umehitimisha Kwa kuonyesha hujui sawali la kujiuliza ni kwamba Gari ya manual ikiwa Kwenye namba tano wakati una overtaking halafu ukaona nguvu za ile gari unalo ovatek zimelingana na ya Gari yako ili uweze kuipita ni lazima utoe 5 uingize gia mamba 4 na hapo utasikia Gari inavuta na kuvuma ila mwendo utaizidi ile unayoiovatek sasa swali kama Gari ni automatic utaifanyaje? Na ikiwa rotation haipandi tena na gari ipo gear namba 5? Ukipata jibu na kuelewa nini nimeuliza utakuwa umekuwa dereva mzuri wa gari zote
 
Over Drive OD if you turn it on the light will go off.... Kama upo katika mazingira ya kawaida sio highway, hakuna milima, you don't overtake, unaendesha kawaida inatakiwa kuwa taa inawaka ikiwa ina masha kuwa OD off

Taa kuwaka mara nyingi uhashiria kuna taadhari lakini kwa OD ni tofauti. Opposite

th

Rudi kidogo shule MKUU
 
Ukiendesha hakikisha kwenye dashboard hakuna taa yoyote inawaka zaidi ya zile za gearliver tu.

Safi MKUU ww ni Dereva mzuri nashangaa watu wanavyodanganyana hapo inaonekana kabisa wamejifunzia magari ya mjomba
 
Lesseni za vichochoroni hizi kazi kweli kweli

Taa yoyote Ile inayowaka kwenye dashboard maanake ni "alert" au sijui niseme alarm kuwa either kuna kitu hakipo Sawa na unapaswa uchunguze au Kama umechunguza na ukaamua kuendesha hivyo hivyo manaake ni kuwa umekielewa hicho kisicho Sawa na umekusudia kutembea hivyo hivyo. Kuanzia indicator, hazard lights, Taa za kawaida, full lights, kufunga mkanda, betrii, oil check, Taa iliyoungua pamoja na hiyo OD. Dashboard inatakiwa iwe clear.

BTW Pale kwenye alert ya OD kuna hadi Taa za kucheki Kama airbags ziko zinafanya kazi au hazifanyi na sensor yake isipoziditect itawaka pia.

MKUU umesema kweli kabisa sasa najiuliza hivi hawa wapouoshaji wamesomea wapi na leseni walipataje kweli kama ndiyo hivi naona ndiyo maana kila siku serikali inabaki kusema madereva wote ni wazembe
 
mm kwa hili nakussuport saana . na ndio watu wanabisha .
huwezi zima taa /OD ON ,while gari iko kwnye speed ndogo . .. utawaiweka ON pale tu ambapo Uko kwenye speed saana na ushamaliza Gear Zote kubwa .

Udereva wako na mtoa Uzi pamoja na unaemsuport ni chini ya wastani saana natamani ungekuwa karibu nikupe maelezo ya vitendo ila basi itabidi mwisho kila mtuu atoe namba zake ili mpigiwe kuelimishwa juu ya O/D maana mnatutia madereva aibu sana
 
Ukiendesha hakikisha kwenye dashboard hakuna taa yoyote inawaka zaidi ya zile za gearliver tu.

Sasa mnatuchanganya, huyu anasema off taa nyekundu ikiwaka na mwingine off taa nyekundu ikizima. Sijui yupi sahihi
 
Nilichohundua hapa wote mko sahihi ila ni jinsi ya kueleza tu. Ni kweli kwa kawaida unatakiwa kuendesha gari OD ikiwa ON ina maanisha kwenye dashboard haitaonekana ila ukiweka off ndiyo itaonekana kwa mandishi mekundu. Cha kuzingatia unapoendesha gari hakikisha taa zinazowaka ni za gear tu ukuona nyingine imewaka ujue hauko sahihi.
 
Kawaida taa ya Over Drive ikiwa on gari huwa nyepesi sana na inatafuna sana mafuta...taa ikizima means Over Drive iko off na ndio normality yake....make sure km upo mjini au sehemu ambayo huhitaji kuendesha speed kali taa ya OD iko off ili ku-serve mafuta???

Wewe uko sawa. Wengine wanapotosha au hawajui
 
Back
Top Bottom