Fahamu kuhusu kusikilizwa kesi upande mmoja (exparte hearing), hukumu ya upande mmoja (exparte judgement), kesi za madai na kesi za jinai

Nyagawakelvin

Member
Apr 8, 2021
7
30
FAHAMU KUHUSU KUSIKILIZWA KESI UPANDE MMOJA (EXPARTE HEARING), HUKUMU YA UPANDE MMOJA (EXPARTE JUDGEMENT), KESI ZA MADAI NA KESI ZA JINAI.

INALETWA KWENU NAMI KELVIN EXZAUDI NYAGAWA, MWANASHERIA KUTOKA CHUO KIKUU MZUMBE MOROGORO

Kisheria,Nini maana ya "EX- PARTE" HEARING?
Nini maana ya "EX PARTE JUDGEMENT"?
Je, mshitakiwa anaweza akahukumiwa kifungo Gerezani na hukumu ikatolewa Mahakamani bila yeye kuwepo katika eneo hilo?

Order IX of Civil Procedure Code Cap. 33 R.E 2019 has it all together with Order VIII
 
FAHAMU KUHUSU KUSIKILIZWA KESI UPANDE MMOJA (EXPARTE HEARING), HUKUMU YA UPANDE MMOJA (EXPARTE JUDGEMENT), KESI ZA MADAI NA KESI ZA JINAI.

INALETWA KWENU NAMI KELVIN EXZAUDI NYAGAWA, MWANASHERIA KUTOKA CHUO KIKUU MZUMBE MOROGORO

Kisheria,Nini maana ya "EX- PARTE" HEARING?
Nini maana ya "EX PARTE JUDGEMENT"?
Je, mshitakiwa anaweza akahukumiwa kifungo Gerezani na hukumu ikatolewa Mahakamani bila yeye kuwepo katika eneo hilo?
Ni Lini Au Ni Katika Mazingira yapi Mahakama italazimika kusikiliza upande mmoja tu wa kesi na kutoa Hukumu ya upande mmoja (Exparte Judgement)?
Zipo aina Kuu mbili za kesi.Aina ya kwanza ya kesi hujulikana kama KESI ZA JINAI(CRIMINAL CASE) na Aina ya Pili ya kesi huitwa KESI AU MASHAURI YA MADAI(CIVIL SUITS/CASE).

Mfano mzuri wa Makosa yanayopelekea uwepo wa kesi za jinai Ni pamoja na wizi,utekaji nyara,kumpa ujauzito mwanafunzi,kutoa lugha ya matusi hadharani, kuharibu mali,kuchoma nyumba moto,kuua,uhaini,shambulio,unyang'anyi wa kutumia silaha,kukamatwa na nyara za Serikali,ubakaji,kutishia kuua kwa maneno,kukutwa na mali ya wizi, kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu; na kadhalika.
Wahusika au watu wanaoshitakiana katika kesi za jinai huitwa MLALAMIKAJI (MTENDEWA) pamoja na MSHITAKIWA (MTUHUMIWA) Complainant and Accused);
Mfano wa Makosa yanayoweza kupelekea kuwepo na Kesi ya Madai ni pamoja na Kuvunja mkataba(makubaliano) kinyume cha maafikiano yenu; kuvamia eneo la mtu; kumkashifu mtu; mirathi; migogoro ya ndoa(talaka na mgawanyo wa mali); kumgonga mtu na kumsababishia majeraha au ulemavu;kukopa pesa na kushindwa kulipa deni na kadhalika.
Katika mashauri ya madai watu wanaoshitakiana huitwa MDAI na MDAIWA;(Plaintiff and Defendant; Applicant and Respondent; Appellant and Respondent).
Adhabu zinazoweza kutolewa na Mahakama katika kesi za jinai ni pamoja na adhabu ya faini,adhabu ya viboko,adhabu ya kunyongwa Hadi kufa; adhabu ya kifungo cha maisha Gerezani; adhabu ya kifungo cha miaka 30 Gerezani; kutaifishwa mali; kifungo cha nje nakadhalika.
Adhabu anazoweza kupewa mtu aliyeshindwa kesi ya madai Ni pamoja na kulipa deni analodaiwa,kulipa fidia ya hasara aliyosababisha,kulipa gharama za kuendeshea kesi,mali zako kupigwa mnada,kumsafisha mtu uliyemchafua kupitia kumuomba radhi kwa maandishi katika magazeti,redio au tv/runinga; kwenda Jela Kama mfungwa wa madai(civil prisoner) n.k
Kesi ikishafunguliwa Mahakamani, Mahakama hutoa wito(Summons) ya kumtaka mtu anayeshitakiwa afike Mahakamani tarehe fulani ili kutoa Utetezi wake.
Mshitakiwa au Mdaiwa anaweza akafika Mahakamani kujitetea akiwa yeye mwenyewe au akiwakilishwa na Wakili wake(His/her Advocate) ama akiwakilishwa na mtu yeyote aliyemruhusu kuzungumza kwa niaba yake(to be represented by a person holding POWER OF ATTORNEY).

Endapo Mshitakiwa au Mdaiwa asipofika Mahakamani kwa muda na tarehe aliyopangiwa na pasipo taarifa yoyote, Mahakama itataka kujiridhisha Kama kweli mtu huyo alipewa wito(summons) inayomtaka afike Mahakamani kwa siku husika.Endapo Mahakama ikajiridhisha kwamba ni kweli mtu huyo alipewa wito wa kuja Mahakamani lakini akaamua kupuuzia wito huo, Mahakama itamruhusu Mlalamikaji (Mdai) kuiomba Mahakama itoe kibali cha kesi hiyo kusikilizwa upande mmoja.

Kitendo cha kesi kusikilizwa upande mmoja kisheria huitwa "EX PARTE HEARING".
Hapa Mlalamikaji peke yake ataruhusiwa kuleta mashahidi wake pamoja na vielelezo vyake vinavyothibitisha malalamiko yake dhidi ya Mshitakiwa.Kwakuwa mshitakiwa atakuwa hayupo Mahakamani,atakuwa amejikosesha haki yake ya kumhoji Mlalamikaji maswali pamoja na kuwasilisha Utetezi wake.
Mlalamikaji akimaliza kutoa Ushahidi wake Mahakama itatoa HUKUMU YA UPANDE mmoja(EX PARTE JUDGEMENT).
Mshitakiwa atatafutwa na kusomewa HUKUMU YA UPANDE MMOJA(EX PARTE JUDGEMENT) lakini pia anaweza akafunguliwa shitaka jingine la kudharau amri halali aliyopewa ya wito wa kuja Mahakamani wakati wa usikilizaji wa kesi yake(kosa hili huitwa DISOBEDIENCE OF LAWFUL ORDER).
Kwakuwa mdaiwa hakushiriki wakati wa usikilizaji wa kesi yake hadi Mahakama kutoa Hukumu ya upande mmoja (Exparte Judgement),mdaiwa atapoteza haki ya kukata rufaa (right to appeal) au haki ya kuomba marejeo ya hukumu(revision/review).(Exparte Judgement is neither appealable nor taken subject to revision/review).
Haki (remedy) pekee ambayo mdaiwa atakuwa nayo ni kuiomba Mahakama itupilie mbali hukumu ya upande mmoja na ianze upya kusikiliza kesi hiyo(application to set aside Exparte Judgement).
Mdaiwa atatakiwa atoe sababu zilizomfanya ashindwe kufika Mahakamani kwa siku ambayo kesi yake ilipangwa kusikilizwa,sababu hizo ziorodheshwe katika kiapo(affidavit).
Mahakama ikishawishiwa na sababu alizozitoa mdaiwa itafuta hukumu ya upande mmoja (Exparte Judgement) na kesi itaanza kusikilizwa upya.!
Mahakama ikigoma kuitupilia mbali hukumu ya upande mmoja (Exparte Judgement) mdaiwa anaruhusiwa kukata rufaa kukosoa uamzi wa Mahakama wa kusita kuifuta hukumu ya upande mmoja.
Hivyo basi ieleweke kuwa Mshitakiwa au Mdaiwa akigoma kufika Mahakamani wakati wa uendeshaji au usikilizaji wa kesi yake; Mahakama itasikiliza upande mmoja na kutoa Hukumu ya upande mmoja; Mshitakiwa anaweza kuhukumiwa kifungo Gerezani hata bila ya yeye kuwepo Mahakamani.

Kelvin Nyagawa (Mwanasheria)
0629700431
Asante mkuu kwa maarifa
 
Kesi nyingi za uhalifu wa kivita kama zile za Rwanda, Liberia, Ivory Coast, n.k. huendeshwa kwa utaratibu huu kwa sababu sometimes ni vigumu kuwapata watuhumiwa. Wengine hujibadili hadi jinsia wasikamatwe.
 
FAHAMU KUHUSU KUSIKILIZWA KESI UPANDE MMOJA (EXPARTE HEARING), HUKUMU YA UPANDE MMOJA (EXPARTE JUDGEMENT), KESI ZA MADAI NA KESI ZA JINAI.

INALETWA KWENU NAMI KELVIN EXZAUDI NYAGAWA, MWANASHERIA KUTOKA CHUO KIKUU MZUMBE MOROGORO

Kisheria,Nini maana ya "EX- PARTE" HEARING?
Nini maana ya "EX PARTE JUDGEMENT"?
Je, mshitakiwa anaweza akahukumiwa kifungo Gerezani na hukumu ikatolewa Mahakamani bila yeye kuwepo katika eneo hilo?

Ni Lini Au Ni Katika Mazingira yapi Mahakama italazimika kusikiliza upande mmoja tu wa kesi na kutoa Hukumu ya upande mmoja (Exparte Judgement)?

Zipo aina Kuu mbili za kesi.Aina ya kwanza ya kesi hujulikana kama KESI ZA JINAI(CRIMINAL CASE) na Aina ya Pili ya kesi huitwa KESI AU MASHAURI YA MADAI(CIVIL SUITS/CASE).

Mfano mzuri wa Makosa yanayopelekea uwepo wa kesi za jinai Ni pamoja na wizi,utekaji nyara,kumpa ujauzito mwanafunzi,kutoa lugha ya matusi hadharani, kuharibu mali,kuchoma nyumba moto, kuua, uhaini, shambulio, unyang'anyi wa kutumia silaha,kukamatwa na nyara za Serikali, ubakaji, kutishia kuua kwa maneno, kukutwa na mali ya wizi, kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu; na kadhalika.

Wahusika au watu wanaoshitakiana katika kesi za jinai huitwa MLALAMIKAJI (MTENDEWA) pamoja na MSHITAKIWA (MTUHUMIWA) Complainant and Accused); Mfano wa Makosa yanayoweza kupelekea kuwepo na Kesi ya Madai ni pamoja na Kuvunja mkataba(makubaliano) kinyume cha maafikiano yenu; kuvamia eneo la mtu; kumkashifu mtu; mirathi; migogoro ya ndoa(talaka na mgawanyo wa mali); kumgonga mtu na kumsababishia majeraha au ulemavu;kukopa pesa na kushindwa kulipa deni na kadhalika.
Katika mashauri ya madai watu wanaoshitakiana huitwa MDAI na MDAIWA;(Plaintiff and Defendant; Applicant and Respondent; Appellant and Respondent).

Adhabu zinazoweza kutolewa na Mahakama katika kesi za jinai ni pamoja na adhabu ya faini,adhabu ya viboko,adhabu ya kunyongwa Hadi kufa; adhabu ya kifungo cha maisha Gerezani; adhabu ya kifungo cha miaka 30 Gerezani; kutaifishwa mali; kifungo cha nje nakadhalika.

Adhabu anazoweza kupewa mtu aliyeshindwa kesi ya madai Ni pamoja na kulipa deni analodaiwa, kulipa fidia ya hasara aliyosababisha, kulipa gharama za kuendeshea kesi, mali zako kupigwa mnada, kumsafisha mtu uliyemchafua kupitia kumuomba radhi kwa maandishi katika magazeti, redio au tv/runinga; kwenda Jela Kama mfungwa wa madai (civil prisoner) n.k
Kesi ikishafunguliwa Mahakamani, Mahakama hutoa wito (Summons) ya kumtaka mtu anayeshitakiwa afike Mahakamani tarehe fulani ili kutoa Utetezi wake.

Mshitakiwa au Mdaiwa anaweza akafika Mahakamani kujitetea akiwa yeye mwenyewe au akiwakilishwa na Wakili wake(His/her Advocate) ama akiwakilishwa na mtu yeyote aliyemruhusu kuzungumza kwa niaba yake(to be represented by a person holding POWER OF ATTORNEY).

Endapo Mshitakiwa au Mdaiwa asipofika Mahakamani kwa muda na tarehe aliyopangiwa na pasipo taarifa yoyote, Mahakama itataka kujiridhisha Kama kweli mtu huyo alipewa wito(summons) inayomtaka afike Mahakamani kwa siku husika.

Endapo Mahakama ikajiridhisha kwamba ni kweli mtu huyo alipewa wito wa kuja Mahakamani lakini akaamua kupuuzia wito huo, Mahakama itamruhusu Mlalamikaji (Mdai) kuiomba Mahakama itoe kibali cha kesi hiyo kusikilizwa upande mmoja.

Kitendo cha kesi kusikilizwa upande mmoja kisheria huitwa "EX PARTE HEARING".
Hapa Mlalamikaji peke yake ataruhusiwa kuleta mashahidi wake pamoja na vielelezo vyake vinavyothibitisha malalamiko yake dhidi ya Mshitakiwa. Kwakuwa mshitakiwa atakuwa hayupo Mahakamani, atakuwa amejikosesha haki yake ya kumhoji Mlalamikaji maswali pamoja na kuwasilisha Utetezi wake.

Mlalamikaji akimaliza kutoa Ushahidi wake Mahakama itatoa HUKUMU YA UPANDE mmoja(EX PARTE JUDGEMENT).
Mshitakiwa atatafutwa na kusomewa HUKUMU YA UPANDE MMOJA(EX PARTE JUDGEMENT) lakini pia anaweza akafunguliwa shitaka jingine la kudharau amri halali aliyopewa ya wito wa kuja Mahakamani wakati wa usikilizaji wa kesi yake (kosa hili huitwa DISOBEDIENCE OF LAWFUL ORDER).

Kwakuwa mdaiwa hakushiriki wakati wa usikilizaji wa kesi yake hadi Mahakama kutoa Hukumu ya upande mmoja (Exparte Judgement),mdaiwa atapoteza haki ya kukata rufaa (right to appeal) au haki ya kuomba marejeo ya hukumu(revision/review).(Exparte Judgement is neither appealable nor taken subject to revision/review).
Haki (remedy) pekee ambayo mdaiwa atakuwa nayo ni kuiomba Mahakama itupilie mbali hukumu ya upande mmoja na ianze upya kusikiliza kesi hiyo(application to set aside Exparte Judgement).

Mdaiwa atatakiwa atoe sababu zilizomfanya ashindwe kufika Mahakamani kwa siku ambayo kesi yake ilipangwa kusikilizwa, sababu hizo ziorodheshwe katika kiapo(affidavit).
Mahakama ikishawishiwa na sababu alizozitoa mdaiwa itafuta hukumu ya upande mmoja (Exparte Judgement) na kesi itaanza kusikilizwa upya.
Mahakama ikigoma kuitupilia mbali hukumu ya upande mmoja (Exparte Judgement) mdaiwa anaruhusiwa kukata rufaa kukosoa uamzi wa Mahakama wa kusita kuifuta hukumu ya upande mmoja.

Hivyo basi ieleweke kuwa Mshitakiwa au Mdaiwa akigoma kufika Mahakamani wakati wa uendeshaji au usikilizaji wa kesi yake; Mahakama itasikiliza upande mmoja na kutoa Hukumu ya upande mmoja; Mshitakiwa anaweza kuhukumiwa kifungo Gerezani hata bila ya yeye kuwepo Mahakamani.

Kelvin Nyagawa (Mwanasheria)
0629700431
Mkuu hongera sana kwa uzi mzuri pls endelea kutoa nyuzi/ threads kwa upande wa cross, recross, jinsi ya ku tender docs Mahakamani, referal procedures etc
 
Hongera kwa Uzi mzuri ila Kwenye practice unaweza ukaappeal hata kama ni exparte judgement
 
Attachments

  • LJ- The right to appeal against exparte judgment is automatic.pdf
    283.9 KB · Views: 29
Back
Top Bottom