Fahamu kuhusu ishara ya kupiga goti moja chini inayofanywa katika maandamano ya George Floyd nchini Marekani

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
4,350
2,000
Habari!

Ikiwa ni takribani wiki mbili zimepita baada ya tukio la kuuawa kwa Mmarekani mweusi George Perry Floyd Jr. ama George Floyd jijini Minneapolis, Minnesota nchini Marekani yakifuatiwa na maandamano makubwa ya kupinga kitendo hicho sambamba na udhalilishwaji wa watu weusi kwa ujumla unaofanywa na polisi, moja ya matukio ambayo yamewaacha baadhi ya watu wakipigwa na butwaa ama bumbuwazi au niseme yameacha mshangao mkubwa kwa watu ni kuhusu kitendo hiki ama ishara hii ya kupiga goti moja chini ama kwa lugha nyingine 'taking a knee' ama 'going down on one knee'.

Makundi ya waandamanaji katika mitaa na miji mbalimbali wamekuwa wakionekana kufanya ishara hii na zaidi ni pale ambapo ishara hii imekuwa ikionekana pia kufanywa na polisi, jambo ambalo pengine ndilo limeonekana kuwashangaza watu wengi zaidi duniani. Wapo watu walio hoji kuwa, kwanini lipigwe goti moja na si yote mawili? Huku wengine wakidai kwamba polisi wanaoonesha ishara hiyo ni wanafiki kwa sababu hata askari aliyemuua Floyd naye alipiga goti.

Kwa wale wasiofahamu, ishara hii imekuwepo kabla hata ya tukio hili la hivi karibuni la kuuawa kwa Floyd. Vilevile, ishara hii haikuasisiwa na yule polisi Derek Chauvin aliyefanya kitendo kile cha kumkandamiza kwa goti George Floyd kama baadhi ya watu wanavyodhani na wala haikuanzia kwa hawa polisi pamoja na waandamanaji wengine wanaoonekana kuifanya ishara hiyo hivi sasa.

Ishara hii imekuwa ikitumika hapo kabla na imepata umaarufu sana katika miaka ya hivi karibuni kupitia kwa mtu mmoja aitwaye Colin Kaepernick ambaye anatajwa kama ndie muasisi wa ishara hii mnamo mwaka 2016 kama ishara ya kupinga unyanyasaji wa polisi na ubaguzi dhidi ya watu weusi.

Colin Kaepernick ama kwa majina yake kamili Colin Rand Kaepernick ni mwanaharakati wa haki za kiraia nchini Marekani ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupinga unyanyasaji na mauaji ya Wamarekani weusi yanayofanya na vyombo vya kusimamia utekelezaji wa sheria. Mbali na hilo, Kaepernick pia ni mchezaji wa mpira wa miguu.

Kwa wale wanaofahamu mpira wa miguu unaojulikana kama 'American Football' ama kwa jina jingine 'Gridiron' basi pengine watakuwa wamepata kumfahamu mtu huyu ambaye amewahi kuitumikia timu inayofahamika kama San Francisco 49ers kuanzia mwaka 2011 hadi mwaka 2016 inayoshiriki ligi la NFL (National Football League) nchini Marekani.

Wakati akiitumikia San Francisco 49ers katika mchezo wa tatu kabla ya msimu wa mwaka 2016 kuanza, Kaepernick alionekana kukaa chini wakati ambapo wimbo wa taifa ulipokuwa ukiimbwa kinyume na utamaduni uliozoeleka wa kusimama.

Wakati wa mahojiano na waandishi wa habari baada ya mchezo, alielezea msimamo wake akisema, "Sitasimama kuonesha kujivunia bendera ya nchi inayowakandamiza watu weusi. Kwangu mimi, jambo hili ni kubwa kuliko mpira wa miguu. Kuna miili ya watu waliouawa barabarani huku wauaji wakiachwa", akimaanisha matukio kadhaa ya mauaji ya Wamarekani weusi yaliyosababishwa na vyombo vya usalama ambayo yalipelekea kuanzishwa kwa harakati za kimataifa za 'Black Lives Matter' za kupinga unyanyasaji na ubaguzi dhidi ya watu weusi.

Colin Kaepernick aliendeleza msimamo wake kwa kusema kuwa ataendelea na mgomo huo mpaka pale ambapo mauaji na vitendo vya kibaguzi dhidi ya Wamarekani weusi vitakapo komeshwa. Katika mchezo wa nne wa timu yake ya San Francisco 49ers kabla ya msimu wa mwaka 2016 kuanza, Kaepernick alipiga goti moja chini wakati wimbo wa taifa wa Marekani ulipokuwa ukiimbwa kama ishara ya kuendeleza mgomo wake.

Tokea hapo, Kaepernick aliendelea kupiga goti moja wakati wimbo wa taifa ulipokuwa ukiimbwa katika kila mchezo wa timu yake msimu mzima wa 2016. Tukio hilo la Colin Kaepernick la kupiga goti moja katika kila mechi ama mchezo liliwavutia wachezaji wengine wa NFL ambapo nao walikuwa wakifanya migomo ya namna hiyo kila wakati wa wimbo wa taifa.

Mtindo huo wa Kaepernick umepokelewa upya mwaka huu wa 2020 wakati wa maandamano ya George Floyd dhidi ya ukatili wa polisi na ubaguzi wa rangi. Makundi mbalimbali ya waandamanaji si nchini Marekani tu bali hata mataifa mengine duniani wamekuwa yakiutumia mtindo huo ama ishara hiyo kama ishara ya kupinga vitendo vya ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi dhidi ya watu weusi.

Natumai mpaka hapa ndugu msomaji utakuwa umepata kufahamu walau machache kuhusiana na ishara hii ama mtindo huu wa kupiga goti moja chini ambao umekuwa ukishamiri katika maandamano ya hivi karibuni nchini Marekani. Nashukuru sana kwa kunifuatilia na karibu kwa maoni. Asante!

Imeandaliwa nami FRANC THE GREAT kutoka vyanzo mbalimbali.

PICHA:
11.jpg

10.jpg

21.jpg

3.jpg

8.jpg

q.jpg

6.jpg
 

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
4,350
2,000
Dortmund and Hertha Berlin players take a knee in powerful show of support for the Black Lives Matter movement on Saturday

adad.jpg

borussia-dortmund-and-hertha-berlin-take-a-knee-protests-continue n.jpg
 

kwakina itafakari

JF-Expert Member
Sep 12, 2018
306
500
Nafikiri jamaa atakuwa anafarijika sana kuona watu wanamuelewa sasa hivi,na style yake inatumika dunia nzima.

Unajua jamaa msimamo wake huo wa kupiga goti moja kipindi wimbo wa Taifa unaimbwa ulimgharimu sana,ilisababisha mtafaruku miongoni mwa wadau wa mchezo huo Marekani, na Donald Trump alikuwa anamind sana kiasi alisema kama wachezaji wakiendelea kufanya hivyo basi watimuliwe tu kwenye team zao,jamaa alijikuta anakosa team ya kumsajili tena msimu uliofuata nafikiri!!!
 

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
42,209
2,000
Imem cost kucheza tena mpira
Timu za wazungu zimegoma kumsajili.
Wazungu wanafiki wanajifanya wanaunga mkono now wakati timu na uongozi wa NFL
Umemtosa Colin wao wakakaa kiimya
 

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
4,350
2,000
Nafikiri jamaa atakuwa anafarijika sana kuona watu wanamuelewa sasa hivi,na style yake inatumika dunia nzima.

Unajua jamaa msimamo wake huo wa kupiga goti moja kipindi wimbo wa Taifa unaimbwa ulimgharimu sana,ilisababisha mtafaruku miongoni mwa wadau wa mchezo huo Marekani, na Donald Trump alikuwa anamind sana kiasi alisema kama wachezaji wakiendelea kufanya hivyo basi watimuliwe tu kwenye team zao,jamaa alijikuta anakosa team ya kumsajili tena msimu uliofuata nafikiri!!!
Hakika.
 

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
4,350
2,000
Dr. Martin Luther King Jr. took a knee as well!

mlk-jr-kneel-lede.jpg

mlk-taking-a-knee (1).jpg


====

PHOTO: Dr. Martin Luther King Jr., center, leads a group of civil rights workers and Selma black people in prayer on Feb. 1, 1965 in Selma, Alabama after they were arrested on charges of parading without a permit. More than 250 persons were arrested as they marched to the Dallas County courthouse as part of a voter registration drive. [TIME]
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom