Fahamu kuhusu Human Papilloma Virus ambayo husababisha Saratani ya Shingo ya Kizazi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Human papilloma virus au kwa kifupi HPV ni kirusi ambacho husambaa kwa asilimia kubwa kwa Njia ya kufanya tendo la ndoa au kujamiiana. Hivyo watu ambao wanafanya mapenzi bila kinga, Wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile, au aina yoyote ya sex( Vaginal sex,anal sex,oral sex) wote wapo kwenye hatari ya kupata kirusi hiki.

MAGONJWA AMBAYO HUSABABISHWA NA KIRUSI HIKI CHA HPV

– HPV au Human papilloma virus huweza kusababisha aina mbali mbali za kansa kwenye mwili wa binadamu kama vile;

1. Kansa ya shingo ya kizazi au kwa kitaalam hujulikana kama Cervical cancer

2. Kansa ya njia ya haja kubwa

3. Kansa ya uume kwa wanaume

4. Kansa ya ukeni kwa wanawake

5. Kansa ya kooni (throat cancer)

N.K

– Asilimia kubwa ya watu wenye maambukizi ya HPV hupata vipele au genital warts kwa wanawake, maumivu wakati wa mapenzi, kuwashwa, kutoa damu wakati wa mapenzi n.k

WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA HPV

– Watu ambao wanafanya mapenzi bila kinga

– Watu wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile

– Watu wenye shida ya kinga ndogo ya mwili mfano wale wenye magonjwa kama vile; UKIMWI

– Watu wenye umri mkubwa zaidi

N.k

MATIBABU YA MAAMBUKIZI YA HPV
– Maambukizi ya human papilloma virus(HPV) hupona yenyewe hasa kwa watoto wadogo, lakini kwa watu wazima ni ngumu kidogo, na kwa bahati mbaya hakuna dawa ya moja kwa moja ya kudhibiti kirusi hiki, bali matibabu yapo kwa ajili ya kudhibiti dalili zinazoletwa na kirusi hiki kama ilivyo matibabu ya magonjwa mengi ambayo huletwa na Virusi mbali mbali.

=====================================

Mnamo mwaka wa 2020, inakadiriwa wanawake 604,000 waligunduliwa na saratani ya shingo ya kizazi ulimwenguni kote na takriban wanawake 342,000 walikufa kutokana na ugonjwa huo.

Sababu kuu ya saratani ya shingo ya kizazi ni maambukizi ya mara kwa mara ya aina hatarishi za virusi ya papilloma ya binadamu (HPV), ambavyo huambukizwa kwa njia ya ngono. Maambukizi ya HPV hayasababishi dalili zozote na kinga ya mwili huweza pambana na kirusi hiki.

Endapo kinga ya mwili ikipungua, uwezekano wa maambukizi kusababisha saratani huongezeka. Takriban saratani zote za shingo ya kizazi inatokana na HPV za aina mbili, HPV16 na HPV18

Chanjo dhidi ya HPV hulinda dhidi ya aina hatarishi za HPV, na programu za uchunguzi zinaweza kutambua dalili za ugonjwa unaoweza sababisha saratani ya shingo ya kizazi katika hatua ya awali kuruhusu matibabu madhubuti na udhibiti wa saratani isitokee.

Chanjo dhidi ya HPV hupewa kwa mtu kabla ya kupata maambukizi kwa hivyo inapendekezwa wasichana walio kati ya umri wa miaka 9 na 13 kupewa. Hii ina maana kwamba saratani ya shingo ya kizazi inapaswa kuwa mojawapo ya aina za saratani zinazoweza kuzuilika na zinazoweza kutibika.

Inashauriwa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi kwa kipimo cha HPV pekee kila baada ya miaka 5 kwa kila mwanamke kuanzia umri wa miaka 30 hadi 65. Ikiwa upimaji wa HPV pekee haupatikani, watu wanaweza kuchunguzwa kwa uchunguzi kipimo cha Papanicolaou kila baada ya miaka 3.
 
Faida ya kunyonya K! Lianaume lizima zinanyonya uchafu
 
Kazi ipo, tujitahidi kula chakula bora ili tuimalishe kinga ya mwili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom