Fahamu kuhusu HISA

youngin

Member
Jan 31, 2020
17
15
Hisa ni nini?
Hisa ni sehemu ya umiliki wa kampuni. Hivyo hisa inawakilisha asilimia fulani ya umiliki katika kampuni. Kama kampuni ina hisa milioni moja na mwekezaji (mwanahisa) anamiliki hisa 100,000 mwekezaji huyu anamiliki 10% ya kampuni. Mwekezaji anayenunua hisa basi ananunua haki ya kumiliki kampuni.
 
@ Soko la hisa, UTT AMIS

Hisa ni nini?

Hisa ni sehemu ya umiliki wa kampuni. Hivyo hisa
inawakilisha asilimia fulani ya umiliki katika kampuni. Kama
kampuni ina hisa milioni moja na mwekezaji (mwanahisa)
anamiliki hisa 100,000 mwekezaji huyu anamiliki 10% ya
kampuni.Mwekezaji anayenunua hisa basi ananunua haki ya
kumiliki kampuni.
Stahili za mwanahisa kisheria ni pamoja na kushiriki katika
kutoa maamuzi ya kampuni katika mkutano mkuu wa
wanahisa na kupata gawio litokanalo na faida iliyozalishwa
na kampuni. Mwanahisa ana haki pia ya kuuza hisa zake
wakati wowote ule.

Gawio ni nini?

Gawio ni malipo kwa wanahisa yanayotokana na sehemu ya
faida inayozalishwa na kampuni. Kwa utaratibu, malipo haya
huwa yanapendekezwa na wakurugenzi na kuidhinishwa
na mkutano mkuu wa wanahisa. Gawio linaweza kulipwa
kutokana na faida ya mwaka husika au malimbikizo ya faida
za nyuma. Gawio linaweza kulipwa kwa fedha taslim au kwa
kuwaongezea hisa wanahisa.

Hatifungani ni nini?

Hatifungani ni hati ya deni ambalo kampuni au serikali
hukopa toka kwa wawekezaji kwa makubaliano maalumu na
kuwalipa riba na marejesho baada ya kuiva kwa hatifungani
hiyo.
Mwenye hatifungani anastahili kulipwa riba (kufika tarehe
ya kurejesha mkopo) na kurudishiwa mtaji wake pale
hatifungani ikishaiva. Pale ambapo kampuni inafilisika,
wanaomiliki hatifungani wana haki ya kulipwa pesa zao
kabla ya wale wanaomiliki hisa. Hii ni moja kati ya tofauti
kubwa uwekezaji katika hisa na hatifungani.
Shukraan..endelea kutupa elimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mbona haya maswala ya hisa Kuna Uzi mods wameupin kabisa katika jukwaa hili la biashara ukiscroll juu kabisa kule
 
Watanzania sasa hivi ukiwaambia habari ya hisa hawataelewa maana VIKOBA vilishawapa elimu tofauti hivyo akiba wataita hisa, Amana wataita hisa, gawio wataita hisa, interest on saving wataita hisa....ni mchanganjo usioeleweka
 
Back
Top Bottom