Fahamu kuhusu hali ya Usalama, Polisi na Haki ilivyo nchini

Sauti za Wananchi

Senior Member
Sep 2, 2014
113
138
Leo Taasisi ya TWAWEZA kupitia Sauti za Wananchi inatoa ripoti ya maoni ya Wananchi kuhusu Usalama, Polisi na Haki nchini.

Kumekuwepo na mfululizo wa matukio ya mauaji yanayotishia hali ya Usalama nchini hususani yake yanayotokea Kibiti, Mkoani Pwani.

Ripoti hii itatoa mtazamo wa Wananchi kuhusu hali ya usalama. Baadhi ya maswali yatakayojibiwa ni:- .

Ni kwa kiasi gani wananchi wanajisikia wapo salama kwenye nyumba zao na katika maeneo wanayoishi?

Wananchi wana uzoefu gani kuhusu uhalifu?

Jeshi la polisi lina jukumu gani katika kuhakikisha ulinzi na usalama?

Viongozi wa serikali za mitaa na sungusungu wana jukumu gani?

Ni kwa kiwango gani wananchi wana imani na uwezo wa mifumo ya utoaji haki katika kuwaadhibu wananchi na watu maarufu wanaofanya uhalifu?

Kwa uchache, tulipata matokeo haya;
  • Raia 6 kati ya 10 wanaona kwamba Wizi/Ujambazi ndio tishio kubwa la usalama katika maeneo yao.
  • Nusu ya raia pia wamesema hali ya usalama katika maeneo jirani nao imeimarika kuanzia mwaka jana.
  • Linapotokea tukio la Uhalifu, Raia 2 kati ya 3 hutafuta msaada kutoka kwa serikali ya kijiji/mtaa.
  • Nusu ya raia wanaridhishwa na utendaji kazi wa polisi na nusu iliyobaki hawaridhishwi na utendaji kazi wa Jeshi la Polisi.
Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi hapa hapa kwenye uzi huu.

Kwa muda huu, unaweza kuungana nasi moja kwa moja (Mubashara) kufuatilia kinachoendelea kwenye mjadala wa ripoti hii kupitia kurasa za mtandao wa JamiiForums huko Twitter, Facebook na Instagram.

Ripoti Kamili imeambatanishwa hapa chini:-

Attachments

  • SzW-Security2017-KIS-FINAL-web.pdf
    1.2 MB · Views: 14
Sample ilifanywa wapi mikoa ipi ilihusishwa watu wangapi walihojiwa wa umri gani jinsi kazi.
 
Utafiti wa JF naukubali sana maana wapo makini sana, ngoja niusome kwa umakini, ingekuwa twaweza ningepita tu kimyakimya
 
Leo tunazindua ripoti ya utafiti tulioufanya kuhusu hali ya Usalama, Polisi na Haki ilivyo hapa nchini.

Kwa uchache, tulipata matokeo haya;

  • Raia 6 kati ya 10 wanaona kwamba Wizi/Ujambazi ndio tishio kubwa la usalama katika maeneo yao.
  • Nusu ya raia pia wamesema hali ya usalama katika maeneo jirani nao imeimarika kuanzia mwaka jana.
  • Linapotokea tukio la Uhalifu, Raia 2 kati ya 3 hutafuta msaada kutoka kwa serikali ya kijiji/mtaa.
  • Nusu ya raia wanaridhishwa na utendaji kazi wa polisi na nusu iliyobaki hawaridhishwi na utendaji kazi wa Jeshi la Polisi.
Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi hapa hapa kwenye uzi huu.

Kwa muda huu, unaweza kuungana nasi moja kwa moja (Mubashara) kufuatilia kinachoendelea kwenye mjadala wa ripoti hii kupitia kurasa za mtandao wa JamiiForums huko Twitter, Facebook na Instagram.

View attachment 551695
Kwa nchi yetu tulipofikia, report kama hizi ni rubbish maana hakuna aliye tayari kutoa ripoti ya kupingana na wishes za serikali kuhatarisha maisha yake/kazi yake/uwepo wa taasisi yake etc.! Any sensible man can not bank on these rubbish report. No one is courageous enough to withstand government intimidation with true report!
 
DONDOO;

- Asilimia 53 ya wananchi wamesema kuwa hali ya usalama imeimarika katika maeno yao ndani ya mwaka 1 uliopita

twawz.jpg

- 55% ya wananchi wa mjini wana vituo vya polisi ndani ya mwendo wa dakika 30 kutoka wanapoishi, ukilinganisha na 23% vijijini

twawezaaa.jpg
 
Pindi wanapokumbwa na tukio la uhalifu, 66% hutafuta msaada kwa Mwenyekiti wa kijiji/mtaa

Ni 26% tu ndio huenda kwanza polisi

twa4.jpg
 
Asilimia 61 ya wananchi Tanzania wanaona kuwa wezi ndilo tatizo kuwa la usalama katika maeneo wanayoishi

twaweza wezi.jpg
 
Hii twaweza think tanks wao si Prof. mkumbo na Prof. bana?
Sidhani Kama haya matokeo ni ya kuaminiwa kwa kiasi hicho!!
 
Back
Top Bottom