Sauti za Wananchi
Senior Member
- Sep 2, 2014
- 113
- 138
Leo Taasisi ya TWAWEZA kupitia Sauti za Wananchi inatoa ripoti ya maoni ya Wananchi kuhusu Usalama, Polisi na Haki nchini.
Kumekuwepo na mfululizo wa matukio ya mauaji yanayotishia hali ya Usalama nchini hususani yake yanayotokea Kibiti, Mkoani Pwani.
Ripoti hii itatoa mtazamo wa Wananchi kuhusu hali ya usalama. Baadhi ya maswali yatakayojibiwa ni:- .
Ni kwa kiasi gani wananchi wanajisikia wapo salama kwenye nyumba zao na katika maeneo wanayoishi?
Wananchi wana uzoefu gani kuhusu uhalifu?
Jeshi la polisi lina jukumu gani katika kuhakikisha ulinzi na usalama?
Viongozi wa serikali za mitaa na sungusungu wana jukumu gani?
Ni kwa kiwango gani wananchi wana imani na uwezo wa mifumo ya utoaji haki katika kuwaadhibu wananchi na watu maarufu wanaofanya uhalifu?
Kwa uchache, tulipata matokeo haya;
Kwa muda huu, unaweza kuungana nasi moja kwa moja (Mubashara) kufuatilia kinachoendelea kwenye mjadala wa ripoti hii kupitia kurasa za mtandao wa JamiiForums huko Twitter, Facebook na Instagram.
Ripoti Kamili imeambatanishwa hapa chini:-

- Raia 6 kati ya 10 wanaona kwamba Wizi/Ujambazi ndio tishio kubwa la usalama katika maeneo yao.
- Nusu ya raia pia wamesema hali ya usalama katika maeneo jirani nao imeimarika kuanzia mwaka jana.
- Linapotokea tukio la Uhalifu, Raia 2 kati ya 3 hutafuta msaada kutoka kwa serikali ya kijiji/mtaa.
- Nusu ya raia wanaridhishwa na utendaji kazi wa polisi na nusu iliyobaki hawaridhishwi na utendaji kazi wa Jeshi la Polisi.