Fahamu kuhusu betri zinazowekwa kwenye moyo ili kuwasaidia wenye matatizo ya moyo kusukuma damu mwilini

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,685
2,000
Betri ya moyo ambayo kitabibu huitwa ‘pacemaker’ ni miongoni mwa vifaa ambavyo vimebuniwa ili kumsaidia mtu ambaye moyo wake unashindwa kuzalisha umeme wa kusukuma damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili.

Taarifa zilizopo zinabainisha kuwa, binadamu wa kwanza kunufaika na tiba hiyo, aliwekewa kifaa hicho mwaka 1960 ilikimsaidie kusukuma damu katika moyo ulioshindwa kusukuma damu kwa kutumia umeme wa asili.

Tangu kuanzishwa kwa huduma za upandikizaji wa betri ya moyo kwenye mwili wa binadamu, watu zaidi ya milioni tatu dunianihuwekewa kifaa hicho kila mwaka. Miongoni mwa watu maarufu waliopandikizwa mashine hiyo ya moyo kifua ni kocha aliyewahi kuifundisha klabu ya soka ya Manchester United ya Uingereza, Sir Alex Ferguson aliyewekewa kifaa hicho mwaka 2003.

Huu ni mwaka wa 17 Ferguson akiishi na kifaa hicho mwilini. Mwingine ni wanamuziki maarufu, Sir Elton John aliyewekewa kifaa hicho mwaka 1999. Huyu alikuwa kwenye safari ya kwenda kwenye sherehe ya David Beckam.

Alipofika uwanja wa ndege, alijisikia vibaya na baada ya kufanyiwa vipimo, iligundulika kuwa mapigo yake ya moyo hayafanyi kazi vizuri hivyo, alifanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa hicho.

Aidha, yupo Dick Chen, aliyekuwa Naibu Rais wa Marekani, katika uongozi wa Rais George Bush. Hata hivyo, licha ya kifaa hicho kuwa mkombozi kwa watu wenye matatizo ya umeme wa moyo, inaelezwa kuwa, baadhi ya wagonjwa wanaowekewa kifaa hicho hupata sonona na baadhi yao huishia kujiua.

Hayo yalibainika katika utafiti uliofanywa na jopo la madaktari wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikina na Kitengo cha Magonjwa ya Akili katika Hosptiali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na kupitishwa rasmi Novemba 29 mwaka jana.

Akizungumzia utafiti huo, Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, Dk Pedro Pallangyo anasema wagonjwa wenye shida ya moyo wanawekewa kifaa hicho maalum (pacemaker) ili kuwasaidia moyo kupiga mapigo yanayokidhi mahitaji yao.

“Hata hivyo, siyo wagonjwa wote ambao wakiwekewa wanapokea vifaa hivi kama ipasavyo kiakili; tafiti zimeonesha baadhi ya wagonjwa hupata hofu, sonona na wengine hata kujiua baada ya kuwekewa vifaa hicho,” anasema Dk Pallangyo.

Anasema kwa wengi walioripotiwa kupata changamoto hiyo, imetokana na kujawa na hofu kubwa akimtolea mfano mzee wa miaka 83 aliyefikishwa hospitali hapo na kutibiwa kwa kuwekewa kifaa hicho, lakini baadae alikutwa amefariki kifo ambacho hakikueleweka.

“Katika utafiti wetu, ‘case study’ yetu ilikuwa ni mzee wa miaka 83 ambaye alitokea Nyanda za Juu Kusini na kuletwa JKCI kwa uchunguzi zaidi,” anasema Pallagyo Anasema mzee huyo alifikishwa katika taasisi hiyo akiwa na maumivu kifuani na mwilini na pia alikuwa amepoteza fahamu kwa takribani miezi sita.

Kwa mujibu wa Dk Pallangyo, historia yam zee huyo ilionesha alikuwa na matatizo hayo ya moyo kwa miaka tisa. Hata hivyo, walifanikiwa kumtibu na matarajio ya kumrudishia uhai yalikuwa makubwa, lakini mgonjwa alifariki baadaye kwa sababu ambazo hazikujulikana. Kutokana na hali hiyo Pallagyo anasema wagonjwa wanaowekewa betri ya moyo wanahitaji pia uchunguzi zaidi wa kisaikolojia ili kugundua matatizo ambayo hayajabainika.

“Ni muhimu kufanya uchunguzi wa aina hii mapema na kuchukua hatua kwa wakati ili kuleta matokeo chanya katika matibabu,” anasema Anaongeza: “Mpaka sasa duniani kote watu watatu wameripotiwa kujiua baada ya kuwekewa betri na wawili kabla ya huyu wetu mzee wa Nyanda za Juu Kusini waliripotiwa kuwa na matatizo ya akili,” alisisitiza.

Dk Pallagyo anasema chapisho hilo la JKCI kuhusu utafitiu ni la kwanza duniani kuhusisha mtu ambae hana historia ya magonjwa ya akili kujiua baada ya kuwekewa betri.

“Kilichomuua mgonjwa siyo kifaa alichowekewa, bali ni mabadiliko ya kisaikolojia aliyopata mgonjwa baada ya kuwekewa kifaa,” anasisitiza na kuongeza “Fundisho hapa ni kwa watoa huduma na ndugu wa mgonjwa kuwa makini kugundua na kutoa msaada wa haraka kabla hayajatokea kama haya tuliyochapisha.”

IMG_20200118_171636_401.jpg
 

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
8,596
2,000
Niliangalia series ya Homeland kuna episode gaidi akafanya mpango apate serial number ya box lilobeba Pace maker aliyokuwa amewekewa makamu wa Rais Marekani. Kwamba zinatumika serial number kuziharibu kwa kutumia kompyuta!! Sijajua kiuhalisia hili lina ukweli kiasi gani
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
22,760
2,000
Come on! Hivi unajua unasema nini au unabwabwaja! Au wewe bado kinda hukumjua amini wakati anaitawala Uganda ! Huwezi kulinganisha JPM na Amini ni ukosefu wa kinga za akili
You are stupid, nani katamka JPM? Wapi mahali nimeandika JPM? Kwani JPM ana pacemaker? You must be nuts! Stupid burger!
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
22,760
2,000
Unatakiwa uwe na Kabendera, umezidi
You are stupid! unadhani wewe hatukujui? Kuna siku utawekwa kitimoto! Utataja kwa ulimi wako uliowaua na kuwapoteza! Mnajulikana sana , the other side is just waiting for the time to click/tick!
 
Top Bottom