Naomba tujadili kuhusu Ada ya upimaji viwanja

shilla de sam

Member
Jan 7, 2013
8
3
Habari Wadau wa JamiiForums, leo nawaletea hoja ambayo imekuwa changamoto hasa kwa wananchi kuhusu tozo ya upimaji wa ardhi katika maeneo mengi Tanzania.

Kuna maeneo ambayo yamepimwa na Halmashauri na baada ya Halmashauri husika kushindwa kulipa fidia kwa Wananchi, Uamuzi ulitolewa wananchi wauze viwanja na atakayenunua akalipe gharama za upimaji Halmashauri.

Kinacholeta changamoto ni mchanaganuo wa gharama ambazo mnunuzi wa Kiwanja anaenda kulipa Halmashauri, Mfano unakuta Tozo ya Upimaji inatozwa kwa Square Meter 1 labda Shilingi 700, hivyo kama umenunua kiwanja chenye Square Meter 800, utatakiwa kulipia Shilingi 560,000, kama tozo ya upimaji.

Kiwango hiki ni tofauti na Agizo la Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, aliposema kuwa Tozo ya Upimaji isizidi Shilingi 200,000 kwa Kiwanja Kimoja cha ukubwa wowote. Sasa ninapata changamoto kujua hizi Halmashauri huo utaratibu wanaoutumia wameutoa wapi?

Wananchi wanaendelea kuonewa hasa katika Masuala ya ardhi. Nauliza utaratibu wa kutoza ada ya upimaji kiwanja kwa SQM umetoka wapi katika Baadhi ya Halmashauri, Wanatuumiza sana!
 
Ulivyoandika kichwa cha mada "Fahamu kuhusu ada ya upimaji viwanja" nikadhani wewe ndiye umekuja kutuelimisha wadau kuhusu hizo ada kumbe sivyo. Pia gharama za upimaji alizosema Lukuvi ni 200,000/= uliyotaja au 150,000/=?
 
Back
Top Bottom