Fahamu kuhusu 10 Desemba, Siku ya Uhuru wa Zanzibar

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
14,986
2,000
December 10 na January 12 ni siku za kukumbukwa na kuadhimishwa


Tarehe 10 December siku nchi ya Zanzibar ilijipatia uhuru wake kutoka kwa mkoloni Muingereza. Kwa mnasaba wa siku hii na jirani zetu nchi ya Tanganyika pamoja na nchi nyengine duniani ni siku ya kukumbukwa halkadhalika kuadhimishwa.


Sambamba na tarehe, nchi ya Zanzibar imo katika hamkani ya kukumbuka na kuadhimisha kila ifikapo tarehe 12 January. Hii ni siku ya mapinduzi, ilipopinduliwa serikali ya kifalme kwa lugha nyengine Sultan.


Halipingi kwa kila Mzanzibar mwenye akili timamu matokeo mawili makuu haya, ambapo kila moja kwa tofauti ya wakati wa kutokea kwake yalileta mabadiliko makubwa kwa mustakbal wa nchi ya Zanzibar na watu wake. Hivyo yapasa kukumbukwa, kuadhinishwa na kuenziwa.


Kupatikana kwa uhuru hapo December 10 kulipelekea kuondoka kwa mkoloni Muingereza na kuifanya serikali ya Zanzibar kuwa chini ya uendeshaji wa wazanzibar wenyewe. Hali hii ilipelekea, kwa urahisi, waleokuwa hawakuridhika kuwa chini ya utawala wa mfumo wa kusultan kufanya mapinduzi. Kuwepo kwa mkoloni Muingereza ingekuwa vigumu kufikiria na kuchukuwa hatua kama hasa kwa nguvu walizokuwa nazo wakoloni.


Ilipofika January 12 haikuwa shida wala tabu mapinduzi yalifanyika na yakafanikiwa. Matokeo mawili haya hayawezi kupingika kutokana na utokeaji wake. Ubaya nikupitia matokeo hayo ndiko kulikoigawa Zanzibar kimtazo kwa kunasibisha wale waliopinga na kutotambua matokeo ya December 10, kwa upande mmoja na wale wanaoipinga yale yaliotokea January 12 kwa upande wa pili.


Ni wajibu wetu sisi kizazi kusicho shuhudia moja ya matokeo haya kujiweka pembeni na badala yake kuzikumbuka na kuziadhimisha tarehe mbili hizi kama urithi wa historia ya nchi yetu. Tunatakiwa tufanye reconciliation kwa kuzitambua December 10 na January 12 kama tarehe muhimu katika historia ya Nchi ya Zanzibar.


Je, ni sikukuu inayopewa uzito wake?! Upinzani waliwahi kuwasilisha hoja bungeni >> Uhuru na Mapinduzi ya Zanzibar
 

Bazazi

JF-Expert Member
Aug 18, 2008
2,797
2,000
Ni kweli!
Zanzibar ilipata uhuru wake tarehe 10/12/1963
Uhuru ulikuwa ni kuondoka kwa mzungu na kuchukua madaraka mwarabu
Hakuna tofauti na Afrika Kusini kupata uhuru mwaka 1910 toka mwingereza na kumpatia mkaburu
Ndio sababu hawasemi siku ya uhuru bali mapinduzi

Bazazi
 

kwamwewe

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,621
1,500
December 10 ni siku Ya kukumbukwa na kuadhimishwa
Leo ni tarehe 10 December siku nchi ya Zanzibar ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa mkoloni Muingereza.
Kwa mnasaba wa siku hii na jirani zetu nchi ya tanganyika pamoja na nchi nyengine duniani ni siku ya kukumbukwa halkadhalika kuadhimishwa.
Sambamba na tarehe, nchi ya Zanzibar imo katika hamkani ya kukumbuka na kuadhimisha kila ifikapo tarehe 12 January. Hii ni siku ya mapinduzi, ilipopinduliwa serikali Waziri Mkuu Muhammed Shamte iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrsia na kulazimishwa kuondoka kwa Mfalme Jemshid.
Halipingi kwa kila Mzanzibar mwenye akili timamu matokeo mawili makuu haya, ambapo kila moja kwa tofauti ya wakati wa kutokea kwake yalileta mabadiliko makubwa kwa mustakbal wa nchi ya Zanzibar na watu wake. Hivyo yapasa kukumbukwa, kuadhinishwa na kuenziwa.
Kupatikana kwa uhuru hapo December 10 kulipelekea kuondoka kwa mkoloni Muingereza na kuifanya serikali ya Zanzibar kuwa chini ya uendeshaji wa wazanzibar wenyewe.
Hali hii ilipelekea, kwa urahisi, waliokuwa hawakuridhika kuwa chini ya utawala wa mfumo wa kidemokrasia na chini ya nguvu za Tanganyika walifanya mapinduzi. Kuwepo kwa mkoloni Muingereza ingekuwa vigumu kufikiria na kuchukuwa hatua kama hasa kwa nguvu walizokuwa nazo wakoloni.
Ilipofika January 12 haikuwa shida wala tabu mapinduzi yalifanyika na yakafanikiwa kwa msaada wa majeshi kutoka Tanganyika. MAPINDUZI YALIPELEKEA PIA KUKAMATWA KWA WAZIRI MKUU SHAMTE PAMOJA NA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI NA KUFUNGWA KATIKA MAJELA YA Tanganyika BILA HATA KUPELEKWA MAHAKAMANI KABLA HATA KUFIKIRIWA HUO MUUNGANO ULIOITWA TANZANIA .
Matokeo mawili haya hayawezi kupingika kutokana na utokeaji wake.
Ni wajibu wetu sisi kizazi kusicho shuhudia moja ya matokeo haya kujiweka pembeni na badala yake kuzikumbuka na kuziadhimisha tarehe mbili hizi kama urithi wa historia ya nchi yetu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom