Swet-R
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 5,613
- 8,041
Asante sana mkuu. Nimeshiba sasaHuo usaidizi ama kwa kitaalamu 'Supportive care' unafanyika kwa wagonjwa wenye dalili za COVID-19 na hujumuisha mambo yafuatayo;
1. Uongezwaji wa maji ndani ya mwili ili kukabiliana na upungufu wa maji mwilini.
2. Usaidizi wa kupumua kwa kutumia vifaa maalumu (oksijeni).
3. Usaidizi katika viungo ama ogani za mwili (vital organs) zenye dalili za kushindwa kufanya kazi; mapafu, figo, ini, moyo n.k. kwa kutumia vifaa maalumu vya kitabibu.
4. Mchanganyiko wa dawa mbalimbali ili kutibu hizo dalili. Dawa zinazotumika ni zile zitumikazo kutibu maradhi mengine kama vile Ebola n.k.
Kinachotibiwa ni dalili tu ila kirusi kinaendelea kuwepo ndani ya mwili maana bado hakuna dawa ya kuweza kukiangamiza kabisa isipokuwa ni uwezo wa mwili wa mgonjwa kuweza kuvithibiti virusi hivyo ili visishambulie mwili na kuleta tena dalili.
Pia, kuna wanaopona dalili hizo lakini kwa mujibu wa tafiti zilizopo, wanaweza kubakia na matatizo mengine ya kudumu katika mifumo yao ya mwili ama ogani zao kutokana na madhara yaliyosababishwa na virusi hivyo isitoshe pia kuna visa vya watu kuambukizwa tena ama kwa mara nyingine.
Bado utafiti zaidi unaendelea kuhusiana na kirusi hiki pamoja na tabia zake maana kuna mambo mengi yahusuyo kirusi hiki bado hayajafahamika kitaalamu.
Sent using Jamii Forums mobile app