Screenshot_20200226-104428-picsay.jpeg
 
Hapa bongo ukikutana na mtu hatakama hamjuani anaanza kukunyooshea limkono, tutakwisha wote.
Siogopi ugonjwa, naogopa kidogo hofu ya ugonjwa. Wengi wataambukizwa, nahisi pia TZ. Wengi sana wanaoambukizwa watapona, asilimia kubwa hata hawawezi kutambua waliingiwa na virusi.
Lakini wengine watagonjeka, na hao asilimia 2-3 watakufa. Au zaidi kidogo kama hospitali hazitoshi na watu hawatumii akili.

Muhimu ni tutunze akili njema. na hapa nasema: tunawe mikono mara kwa mara. Na pia virusi vitakapoingia - basi tuepukane kupeana mikono. Kwa Wairan nilikuta desturi njema (si wote wanafanya vile, lakini wengi kiasi); Unaweka mkono wa kiume kifuani juu ya moyo, unanama kichwa. Ni salamu ya heshima pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha ajab ni kuwa binadam hupenda kuwaza wakipendacho au kitachowapa furaha ya moyo
Ila ukweli ni kwamba ukweli una njia zake nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viko kabisa. Tangu mwaka 2004 picha zake zinapatikana kwa njia ya hadubini elekroniki. Angalia
hapa
hapa (wameongeza rangi) inaonyesha jinsi gani virusi vya HIV vinatoka kwenye seli iliyoathiriwa kutafuta seli mpya
Ahsante sana mkuu.
 
Hii thread mpya inarudia madai eti virusi vya corona ni salaha ya kibiolojia
Madai hayo hakuna msingi. Yameshajadiliwa kwa undani na makini hapa JF
The novo coronavirus: Could it have been genetically engineered for the Chinese race as a bio-weapon?

Mleta mada alichota kwenye blogu zisizo za kitaalamu ,a,eshinda kutetea hoja
 
Update:

Ukija bongo huu ugonjwa,,,kwa jinsi tunavopenda vya kunusa nusa,,tutakufa kama kuku wa mdondo.
Hapana. Hatutakufa kama kuku wa mdondo. Hadi sasa ni asilima 2-3 wanaokufa.
Wanaogonjeka vibaya: kama %5.
Kuna hatari kama watu wanasambaza fujo badala ya kutumia akili .
Maana mara ikifika Bongo -
tuzoee kunawa mikono mara kwa mara
tuepukane na msongamano wa watu (jambo gumu kwa hao wanaopanda mwendokasi... - sitaingia ikijaa)
tusali nyumbani, tusiende kanisani au msikitini ikijaa
nitacha kuwasalimu watu kwa kupeana mikono (isipokuwa kama sabuni na maji iko karibu)

jisomee hapa: Virusi vya corona - Wikipedia, kamusi elezo huru
 
Hii thread mpya inarudia madai eti virusi vya corona ni salaha ya kibiolojia
Madai hayo hakuna msingi. Yameshajadiliwa kwa undani na makini hapa JF
The novo coronavirus: Could it have been genetically engineered for the Chinese race as a bio-weapon?

Mleta mada alichota kwenye blogu zisizo za kitaalamu ,a,eshinda kutetea hoja
Kwahiyo mkuu, ukishindwa kutetea Hoja ni kwanini saa sita jua linakua utosini basi tunaafiki saa sita hakuna jua la utosi sio ??

Hahaha , aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iran

Maambukizi ya virus vya Corona 19 yafikia 139.

Idadi ya vifo imefikia 19

Serikali imesema kuwa haitawaweka miji yake katika uangalizi

Serikali yasema kuwa ni propaganda za Mabeberu

Iran ndiyo imekuwa msambazaji mkubwa wa virus hivi kwenye nchi za Mashariki ya Kati



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom