Fahamu kiasi cha pesa unacholipa kwa umeme unaotumia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fahamu kiasi cha pesa unacholipa kwa umeme unaotumia

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Baba Mtu, Aug 12, 2011.

 1. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Leo ndugu wanajamvi nimeonelea niwaletee maelezo kidogo kuhusu pesa tunazochangia kununua umeme, na hasa kwa wale tunaoishi katika nyumba za kupanga.
  Labda nianze na umeme tunaonunua toka tanesco. Tunanunua umeme toka tanesco katika kipimo cha UNITS, mfano tunanunua mafuta ya taa katika kipimo cha lita.
  UNIT maana yake ni nini? UNIT maana yake ni kiasi cha umeme unachotumia kwa muda wa dakika 60 yaani saa 1. Kiasi cha umeme tunaotumia kinapimwa katika kipimo cha WATT. Kipimo kikubwa ni KiloWatt. Mfano kipimo kidogo cha sukari ni gramu na kipimo kikubwa ni Kilogramu.
  Kwa hiyo:
  UNIT moja= Kilowatt Saa moja (1 Unit = 1 Kilowatt Hour). Kwa mfano tunaponunua unit moja ya umeme toka tanesco, tujue kuwa tunanunua kiliowatt moja ya umeme ambayo matumizi yatadumu kwa muda wa dakika 60 kutegemeana na aina ya kifaa cha umeme unachotumia. Kama kifaa chako cha umeme ni kikubwa basi utatumia hiyo kilowatt moja ya umeme chini ya muda wa dakika 60.
  Baada ya maelezo hayo sasa tuone jinsi tunavyodhulumiwa na baadhi ya wenye nyumba na wapangaji wenzetu pale kinapofika kipindi cha kuchangia umeme. Dhuluma inakuja pale wapangaji wote wanapotakiwa walipe/wachangie kiasi sawa cha bili ya mchango wa umeme. Kwa mfano mpangaji anaetumia tv, taa na redio tena kwa muda mchache anapotakiwa achangie kiasi sawa na mpangaji anaetumia pasi, taa, redio labda na friji.
  Kila kifaa kina matumizi yake yake ya umeme, na matumizi hayo ya umeme kwa kifaa husika huwa yanaandikwa nyuma, pembeni au juu kifaa husika. Ili ujue ni kiasi gani cha pesa unatakiwa uchangie basi ni lazima ujue kifaa chako kinatumia umeme kiasi gani. Kiasi cha umeme kitumiwacho na kifaa husika huonyeshwa kwa maandishi ya Watts (W), Kilowatts kW) au Volt ampere (VI).
  MUHIMU: Watt moja= volt moja X ampere moja (1 Watts = 1 Volt X 1 Ampere). Mfano hapa nina kifaa cha umeme kitumiacho kiasi cha umeme 5VA, hii maana yake ni kuwa kifaa hiki kinatumia umeme wa watts 5.
  Kwa mfano katika chumba ninachoishi mimi, natumia TV ambayo matumizi yake ya umeme ni 80Watts, natumia DVD Player ambayo matuimizi yake ya umeme ni 3Watts, natumia balbu ya eneji seva ya 18Watts. Pia nina pasi ya 1000Watts, maikrowevu oven ya Watts 2400, birika ya kuchemshia maji ya Watts 2000, na laptop ya Watts 45, feni ya darini ya Watts 75. Ili kujua jumla ya umeme niutumiao, najumlisha umeme toka vifaa vyote:
  80Watts + 3Watts + 18Watts + 1000Watts + 2400Watts + 45Watts + 75Watts + 2000Watts= 5621Watts. Kiasi hiki cha umeme ni sawa na Kiliowatts 5.621. Kama vifaa hivi vitatumia umeme kwa muda wa saa 1, hapo nitakuwa nimetumia Units 5.621 za umeme. Mimi nafanya kazi katika ofisi Fulani, huwa natoka nuymbani saa 12:30 asubuhi na kurejea saa 1:00 jioni na hulala saa 5:00 usiku.
  Mpangaji wa chumba cha pili ana maikrowevu ya Watts 2500, birika ya kuchemshia maji ya Watts 2000, tyubu laiti ya Watt 38, pasi ya Watts 1000, DVD Player ya Watts 5, feni ya darini ya Watts 90, friji ya Watts 500 na TV ya Watts 70. Huyu bwana, ukifanya hesabu kama hapo juu utaona kuwa anatumia umeme wa Watts 6122 sawa na kiliowatts 6.122. Kama vifaa hivi vitatumia umeme kwa muda wa saa 1, hapo atakuwa ametumia Units 6.122 za umeme.
  Mpangaji wa chumba cha tatu ana ofisi ya michezo (play station) yenye TV 8 kila moja ina Watts 85, DVD Player ya Watts 4 , kompyuta ya mezani na skirini ndogo , vyote ni Watts 220 Watts na feni ya darini ya Watts 90. Chumbani kwake kuna TV ya Watt 80, balb ya eneji seva ya Watts 11, feni ya darini ya Watts 75 na pasi ya Watts 1000. Ukifanya hesabu utaona kuwa matumizi yake ya umeme ni Watt 2160 sawa na kilowatts 2.160. Kama vifaa hivi vitawaka kwa muda wa saa 1, hapo atakuwa ametumia Units 2.160 za umeme. Huyu ndugu hufungua ofisi yake saa 2:00 asubuhi na kufunga saa 3:00 usiku.
  Banda la uani kuna msela amepanga, yee ni dereva wa daladala. Ana feni ya darini ya Watts 90, TV ya Watts 65, balbu ya eneji seva ya Watts 22, pasi ya Watts 1000 na DVD Player ya Watts 3. Kutokana na shughuli zake huyu bwana huwa anatoka saa 10:00 alfajir na hurejea saa 5:00 usiku na hulala kabla ya saa 6:00 usiku. Ukifanya hesabu utaona kuwa matumizi yake ya umeme ni Watt 1180 sawa na kilowatts 1.180. Kama vifaa hivi vitawaka kwa muda wa saa 1, hapo atakuwa ametumia Units 1.1800 za umeme
  Baba mwenye nyumba ana TV ya kioo bapa ya Watts 150, friji ya Watts 700, DVD Player ya Watts 5, balbu ya eneji seva ya Watts 18, hita ya Watts 1000, feni za darini mbili kila moja ni Watts 70, Brenda ya Watts 450 na oven ya Watts 2000. Ukifanya hesabu utaona kuwa matumizi yake ya umeme ni Watt 4463 sawa na kilowatts 4.463. Kama vifaa hivi vitawaka kwa muda wa saa 1, hapo atakuwa ametumia Units 4.463 za umeme. Baba mwenye nyumba muda wote yupo nyumbani, anauza juisi, maji baridi, aiskirim na barafu.
  Kasheshe ukifika muda wa kununua umeme, aidha Yule mwenye vifaa vingi ndio atahitajika kuchangia kiasi kikubwa cha pesa ama wapangaji wote watachangia kiasi sawa, hapo sasa ndio kuna kuibiana. Kiukweli mchango unatakiwa uendane na matumizi sahihi ya umeme na sio wingi wa vifaa vitumiavyo umeme. Kwa mfano hapo juu tunaona mpangaji ana TV 11 lakini bado anatumia umeme kidogo sana.
  Kuna watu wanaogopa kununua maikrowevu kwa kuhofia matumizi makubwa ya umeme. Ni kweli maikrowevu inakula umeme, lakini pia inategemea na muda uliotumia kufanyia shughuli husika. Mfano mimi hutumia maikrowevu ya Watts 2400 kupashia moto chakula kwa muda wa dakika 3. Je, huwa natumia umeme kiasi gani?. Kumbuka: 1 Unit = 1 Kilowatts Hour. Matumizi ya umeme ya maikrowevi ni Watts 2400, hii ni sawa na Kilowatts 2.4. Muda ninaotumia ni dakika 3, huu ni sawa na saa 3/60 au saa 0.05. Umeme utumikao (UNIT)= Kilowatts X Muda = Kilowatt 2.4 X saa 0.05 = Kilowatts +0.12 = Units 0.12.
  Linganisha na baba mwenye nyuma anaewasha friji ya Watts 700 kwa muda wa saa 24.
  Watts 700 ni sawa na Kilowatts 0.7. Kwa hiyo umeme anaotumia baba mwenye nyumba kwa friji la watts 700 linalowaka kwa muda wa saa 24 ni sawa na Kilowatts 0.7 X saa 24 = units 16.8
  Naomba niishie hapa. Maswali na marekebisho pale nilipokosea yanakaribishwa.
   
 2. G_crisis

  G_crisis JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 715
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Shukrani mkuu kwa elimu hii adimu,huwa tunaibiwa sana aisee
   
 3. Makbel

  Makbel JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 774
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  dah! kweli kabisa kaka.
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Way to go :]

  wateja kwenye nyumba ya kupanga wanatakiwa kulipia kwa mujibu wa matumizi yao plus an alpha (na zaidi kidogo) ili kukidhi service charge ya TANESCO ambayo hulipiwa mbali na bei za units.
   
 5. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2011
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  gud analysis, ila kwa huu mgao wa umeme ndio wizi unaongezeka zaidi maana matumizi ni kama yako pale pale wakati umeme hakuna
   
 6. pomo

  pomo JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  dah nyuma nyingi huwa wanafanya flat rate,,kuna jamaa yangu mmoja alikuwa analalamika walikuwa wamepanga na mtu mwenye ac na anaiwasha usiku wote,,,kwenye malipo wanapiga 20,000 kwa kila mpangaji kwa mwezi
   
 7. MataFire

  MataFire Member

  #7
  May 28, 2013
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Jamani naomba kujua gharama za kuzalisha UNIT moja ya umeme kwa TANESCO
   
 8. m

  moghaka JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2013
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Shukrani hii ni elimu ya maana sana kwa jamii
   
 9. bily

  bily JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2013
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 8,019
  Likes Received: 3,917
  Trophy Points: 280
  Well said mkuu thanks for your contribution.
   
 10. jajcom

  jajcom Senior Member

  #10
  May 28, 2013
  Joined: Jan 4, 2013
  Messages: 109
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  kaka ulisomea uchumi.?
  nimeipenda.
   
 11. M

  Mipale Steve JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2013
  Joined: Jan 26, 2013
  Messages: 387
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  muulize muhongo au simbachawene
   
 12. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2013
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Elimu nzuri ila hii ni dalili tosha kwamba maisha ya mtanzania yamekuwa magumu sana. Hadi tukokotoe simu nikichaji ni watt ngapi!
   
Loading...