Fahamu kiasi cha pesa unacholipa kwa umeme unaotumia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fahamu kiasi cha pesa unacholipa kwa umeme unaotumia

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Baba Mtu, Aug 12, 2011.

 1. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Leo ndugu wanajamvi nimeonelea niwaletee maelezo kidogo kuhusu pesa tunazochangia kununua umeme, na hasa kwa wale tunaoishi katika nyumba za kupanga.
  Labda nianze na umeme tunaonunua toka tanesco. Tunanunua umeme toka tanesco katika kipimo cha UNITS, mfano tunanunua mafuta ya taa katika kipimo cha lita.
  UNIT maana yake ni nini? UNIT maana yake ni kiasi cha umeme unachotumia kwa muda dakika 60 yaani saa 1. Kiasi cha umeme tunaotumia kinapimwa katika kipimo cha WATT. Kipimo kikubwa ni KiloWatt. Mfano kipimo kidogo cha sukari ni gramu na kipimo kikubwa ni Kilogramu.
  Kwa hiyo:
  UNIT moja= Kilowatt Saa moja (1 Unit = 1 Kilowatt Hour). Kwa mfano tunaponunua unit moja ya umeme toka tanesco, tujue kuwa tunanunua kiliowatt moja ya umeme ambayo matumizi yatadumu kwa muda wa dakika 60 kutegemeana na aina ya kifaa cha umeme unachotumia. Kama kifaa chako cha umeme ni kikubwa basi utatumia hiyo kilowatt moja ya umeme chini ya muda wa dakika 60.

  Baada ya maelezo hayo sasa tuone jinsi tunavyodhulumiwa na baadhi ya wenye nyumba na wapangaji wenzetu pale kinapofika kipindi cha kuchangia umeme. Dhuluma inakuja pale wapangaji wote wanapotakiwa walipe/wachangie kiasi sawa cha bili ya mchango wa umeme. Kwa mfano mpangaji anaetumia tv, taa na redio tena kwa muda mchache anapotakiwa achangie kiasi sawa na mpangaji anaetumia pasi, taa, redio labda na friji.
  Kila kifaa kina matumizi yake yake ya umeme, na matumizi hayo ya umeme kwa kifaa husika huwa yanaandikwa nyuma, pembeni au juu kifaa husika. Ili ujue ni kiasi gani cha pesa unatakiwa uchangie basi ni lazima ujue kifaa chako kinatumia umeme kiasi gani. Kiasi cha umeme kitumiwacho na kifaa husika huonyeshwa kwa maandishi ya Watts (W), Kilowatts kW) au Volt ampere (VI).
  MUHIMU: Watt moja= volt moja X ampere moja (1 Watts = 1 Volt X 1 Ampere). Mfano hapa nina kifaa cha umeme kitumiacho kiasi cha umeme 5VA, hii maana yake ni kuwa kifaa hiki kinatumia umeme wa watts 5.

  Kwa mfano katika chumba ninachoishi mimi, natumia TV ambayo matumizi yake ya umeme ni 80Watts, natumia DVD Player ambayo matuimizi yake ya umeme ni 3Watts, natumia balbu ya eneji seva ya 18Watts. Pia nina pasi ya 1000Watts, maikrowevu oven ya Watts 2400, birika ya kuchemshia maji ya Watts 2000, na laptop ya Watts 45, feni ya darini ya Watts 75. Ili kujua jumla ya umeme niutumiao, najumlisha umeme toka vifaa vyote:
  80Watts + 3Watts + 18Watts + 1000Watts + 2400Watts + 45Watts + 75Watts + 2000Watts= 5621Watts. Kiasi hiki cha umeme ni sawa na Kiliowatts 5.621. Kama vifaa hivi vitatumia umeme kwa muda wa saa 1, hapo nitakuwa nimetumia Units 5.621 za umeme. Mimi nafanya kazi katika ofisi Fulani, huwa natoka nuymbani saa 12:30 asubuhi na kurejea saa 1:00 jioni na hulala saa 5:00 usiku.

  Mpangaji wa chumba cha pili ana maikrowevu ya Watts 2500, birika ya kuchemshia maji ya Watts 2000, tyubu laiti ya Watt 38, pasi ya Watts 1000, DVD Player ya Watts 5, feni ya darini ya Watts 90, friji ya Watts 500 na TV ya Watts 70. Huyu bwana, ukifanya hesabu kama hapo juu utaona kuwa anatumia umeme wa Watts 6122 sawa na kiliowatts 6.122. Kama vifaa hivi vitatumia umeme kwa muda wa saa 1, hapo atakuwa ametumia Units 6.122 za umeme.

  Mpangaji wa chumba cha tatu ana ofisi ya michezo (play station) yenye TV 8 kila moja ina Watts 85, DVD Player ya Watts 4 , kompyuta ya mezani na skirini ndogo , vyote ni Watts 220 Watts na feni ya darini ya Watts 90. Chumbani kwake kuna TV ya Watt 80, balb ya eneji seva ya Watts 11, feni ya darini ya Watts 75 na pasi ya Watts 1000. Ukifanya hesabu utaona kuwa matumizi yake ya umeme ni Watt 2160 sawa na kilowatts 2.160. Kama vifaa hivi vitawaka kwa muda wa saa 1, hapo atakuwa ametumia Units 2.160 za umeme. Huyu ndugu hufungua ofisi yake saa 2:00 asubuhi na kufunga saa 3:00 usiku.

  Banda la uani kuna msela amepanga, yee ni dereva wa daladala. Ana feni ya darini ya Watts 90, TV ya Watts 65, balbu ya eneji seva ya Watts 22, pasi ya Watts 1000 na DVD Player ya Watts 3. Kutokana na shughuli zake huyu bwana huwa anatoka saa 10:00 alfajir na hurejea saa 5:00 usiku na hulala kabla ya saa 6:00 usiku. Ukifanya hesabu utaona kuwa matumizi yake ya umeme ni Watt 1180 sawa na kilowatts 1.180. Kama vifaa hivi vitawaka kwa muda wa saa 1, hapo atakuwa ametumia Units 1.1800 za umeme

  Baba mwenye nyumba ana TV ya kioo bapa ya Watts 150, friji ya Watts 700, DVD Player ya Watts 5, balbu ya eneji seva ya Watts 18, hita ya Watts 1000, feni za darini mbili kila moja ni Watts 70, Brenda ya Watts 450 na oven ya Watts 2000. Ukifanya hesabu utaona kuwa matumizi yake ya umeme ni Watt 4463 sawa na kilowatts 4.463. Kama vifaa hivi vitawaka kwa muda wa saa 1, hapo atakuwa ametumia Units 4.463 za umeme. Baba mwenye nyumba muda wote yupo nyumbani, anauza juisi, maji baridi, aiskirim na barafu.

  Kasheshe ukifika muda wa kununua umeme, aidha Yule mwenye vifaa vingi ndio atahitajika kuchangia kiasi kikubwa cha pesa ama wapangaji wote watachangia kiasi sawa, hapo sasa ndio kuna kuibiana. Kiukweli mchango unatakiwa uendane na matumizi sahihi ya umeme na sio wingi wa vifaa vitumiavyo umeme. Kwa mfano hapo juu tunaona mpangaji ana TV 11 lakini bado anatumia umeme kidogo sana.

  Kuna watu wanaogopa kununua maikrowevu kwa kuhofia matumizi makubwa ya umeme. Ni kweli maikrowevu inakula umeme, lakini pia inategemea na muda uliotumia kufanyia shughuli husika. Mfano mimi hutumia maikrowevu ya Watts 2400 kupashia moto chakula kwa muda wa dakika 3. Je, huwa natumia umeme kiasi gani?. Kumbuka: 1 Unit = 1 Kilowatts Hour. Matumizi ya umeme ya maikrowevi ni Watts 2400, hii ni sawa na Kilowatts 2.4. Muda ninaotumia ni dakika 3, huu ni sawa na saa 3/60 au saa 0.05. Umeme utumikao (UNIT)= Kilowatts X Muda = Kilowatt 2.4 X saa 0.05 = Kilowatts +0.12 = Units 0.12.

  Linganisha na baba mwenye nyuma anaewasha friji ya Watts 700 kwa muda wa saa 24.
  Watts 700 ni sawa na Kilowatts 0.7. Kwa hiyo umeme anaotumia baba mwenye nyumba kwa friji la watts 700 linalowaka kwa muda wa saa 24 ni sawa na Kilowatts 0.7 X saa 24 = units 16.8

  Naomba niishie hapa. Maswali na marekebisho pale nilipokosea yanakaribishwa.
   
 2. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Mkuu hongera kwa uchambuzi,,,ila ukileta ujuaji huwa kwa wapangaji wenzako itakua ugomvi kila siku.

  pia ni ngumu kujua vifaa vyote vya mpangaji mwenzako. Haiwezekani mfano baada ya miaka 2 akawa anavifaa vilevile.
   
 3. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />


  Asante kwa uchambuzi umesahau nishilingi ngapi ilimhgalim kupata huo umeme mf nguzo mita waya nk mlichangia sh ngapi?
   
 4. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,377
  Trophy Points: 280
  Ninavyojua mimi units hazipimwi kwa kuangalia dakika 60, wanaangalia watts zinazotumika per seconds..
   
 5. Paje

  Paje JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2011
  Joined: Apr 24, 2010
  Messages: 1,198
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  umetumia neno zuri sana. "nijuavyo mimi" ila ukweli ni kuwa ujuavyo weye sio sahihi. mtoa mada ameongea usahihi katika suala la kupima unit za umeme. huangaliwa dakika 60.
   
 6. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,377
  Trophy Points: 280
  je kama unatumia umeme mdogo kuliko watts zilizopangwa katika dakika 60 itakuwaje?
   
 7. mojoki

  mojoki JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 1,333
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  mambo mengine unachukulia poa tu ...unamuuliza baba mwenye nyumba umeme kiasi gan kwa mwezi? Akisema 10000 unampa 10000 yake unapotezea ukianza kufanya hayo mahesabu yako unauchosha ubongo kwa sababu zisizo za msingi...
   
 8. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  umeona eeee
   
 9. Loyal_Merchant

  Loyal_Merchant JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 589
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ila ningependa kuchangia kwamba watts na voltage ampere haviko sawa. Ingawa wengi wanaamini ni vipimo sawa.
   
 10. Loyal_Merchant

  Loyal_Merchant JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 589
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />
  zitajiacumulate mpaka zifike kw1 then ndo meter itapunguza 1 unit. Katika reading zake. Ila tukirudi darasani ni kwamba 1unit sawasawa na 1kwh. Na tukija ktk dimension, unit ni energy sema inabidi uzidishe kwa 3600 sec ili iwe na unit ya joule.
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Physics@wek
   
 12. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,377
  Trophy Points: 280
  wow, thanx mkuu, wengine tupo Arts.. Heheee
   
 13. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Haya tunashukuru mmetukumbusha physics lakini ukihoji yote hayo utakuta unajicomplicate for nothing, just take it easy na maisha yanakwenda, simping mtoa maada ila kuna vitu vingi sana tunauziwa unfairly hasa ukiangalia nchi yetu hatuna tendency ya kudai risit. Lakini serikali inatuibia kwenye kodi, mshahara unakatwa kodi afu kila unachonunua wanakata kodi. Hebu tuanze kudai haki zetu kutoka huku kwanza ndo tuanze maeneo minor kama haya. Nawasilisha
   
 14. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2011
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Rejea What is volt-ampere (VA)? Definition from WhatIs.com - see also: VA


  Kumbuka kuwa 3600 seconds = 1 hour
   
 15. chama2chawa

  chama2chawa JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2016
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 488
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  mtoa mada umenikumbusha mbali sana hesabu zangu hizo wakati nasoma hakuna aliyenugusa wakati huo. Hongera umefafanua vizuri mno
   
 16. DEOD 360

  DEOD 360 JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2016
  Joined: Jun 30, 2016
  Messages: 2,070
  Likes Received: 2,838
  Trophy Points: 280
  Kwenye nyumba ya kupanga hayo maesabu hayana mafasi labda kama nyumba yako
   
 17. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2016
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Huyu Jamaa alifia Wapi?
   
 18. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2016
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  mkuu umeadimika sana kitambo sijakuona vipi mabo yetu yale yapo guru
   
 19. shushushu VIP

  shushushu VIP JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2016
  Joined: Jul 24, 2016
  Messages: 4,516
  Likes Received: 3,738
  Trophy Points: 280
  nmekupata kaka
   
 20. SANCTUS ANACLETUS

  SANCTUS ANACLETUS JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2016
  Joined: Mar 5, 2016
  Messages: 1,546
  Likes Received: 1,772
  Trophy Points: 280
  Hapa kwa mtu anayeona mbali hii biashara.Migogoro ya nani ametumia nini katika umeme ni fursa.Ngoja tuzame tutaleta ufumbuzi
   
Loading...