hydroxo
JF-Expert Member
- Oct 19, 2015
- 3,247
- 6,767
Damu ni tishu(tissue) iliyo katika hali ya majimaji.
Inakadiliwa kila binadamu aliye kijana anamiliki ujazo wa lita tano za damu ndani ya mwili wake.
Damu ya mwanadamu imetengenezwa na vitu vikuu viwili ambavyo ni;
1.utegili(plasma) na 2.seli za damu(blood cells).
1.Utegili au plasma ni sehemu ya maji maji ya damu yenye rangi umanjano inayochukua 55% ya damu yote.90% ya utegili ni maji na 10% ni glukosi(glucose), ayoni za madini mbalimbali kama sodiamu,maginiziamu na kloraidi,homoni,vimeng'enya(enzymes) na kadhalika.
2.Seli za damu(blood cells) huchukua 45% ya damu yote na zipo za aina tatu kama zifuatazo;
(1)chembe nyeupe za damu(leucocytes)
(2)chembe nyekundu za damu(erythrocytes)(3)na chembe sahani za damu(platelets).
Kuelezea kwanini damu ni nyekundu tutazungumzia chembe nyekundu za damu pekee,damu uonenakana nyekundu kwa sababu zina kiwango cha juu cha seli nyekundu (milion 500 kwa milimita moja ya ujazo) kuliko seli nyeupe ambazo zipo kama 700 kwa milimita moja ya ujazo.