101 East
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 1,040
- 2,118
Kwa miaka mingi mainjinia na maprofesa wa ubunifu wa miundo ya ndege wamekuwa wakimmezea mate bundi arukaye usiku.
Je ni kwanini Bundi amekuwa akimezewa mate kutokana na uwezo wake wa ajabu wa mbawa zake.
Hii ni kwasababu mbawa zake hazipigi kelele pale anaporuka.
Wataalam kutoka national geographic wanasema hakuna ndege yeyote duniani anayeruka kimya kimya hivyo. Ndege wengi wanaporuka wao hutokeza kelele wakati upepo unapopita juu ya manyoya yao. Lakini manyoya ya bundi hayafanyi hivyo.
Manyoya yake ya nyuma yana miisho ya kipekee ambayo hutawanya mawimbi ya sauti yanayotokeza pindi upepo unapopita juu ya manyoya yao.
Anapopiga mbawa zake chini wakati wa kuruka. Manyoya mengine husaidia kufyonza kelele yoyote inayotokea.
Mainjinia wa vyombo vya angani bado wanaendelea kutafiti uwezo huo wa kuruka bila kelele ili hatimaye watengeneze ndege yenye uwezo huo wa kuruka bila kelele.
Kuwa na ndege za aina hiyo vitasaidia viwanja vya ndege vilivyo na sheria kali kuhusu kelele nyingi viruhusu ndege kutua usiku sana na mapema sana asubuhi.
Profesa Geofrey Lilley ambaye ni profesa aliyestaafu wa vyombo vya angani chuo kikuu cha Southampton Uingereza anasema "tumeanza sasa kuboresha ndege kwenye njia hiyo na huenda ikachukua miongo kadhaa kabla ya ndege inayo ruka kimya kimya kutengenezwa.
View attachment 1588802View attachment 1588801