fahamu jinsi unavyoweza kutumia elimu yako katika kujia ajiri na kupata pesa ukiwa na mtaji mdogo

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,182
3,547
habari zenu wadau leo nimeuleta uzii huu jinsi unavyoweza kutumia elimu yako na kupata pesa na huu umekuja baada ya kufanya utafiti...hata kama una mtaji mdogo unaweza ukafanya kazi ambayo itakutoa na kupata pesa ndogo ndogo

1.kwa mtu ambae umemaliza chuo na una uwezo wa kuandika project,kuandaa repoti...basi wewe ni kampuni tosha unaweza ukafungua ofisi yako ukawa unawaandikia na unawasaidia nwanafunzi wengi kuwaandalia final projects kuna wanafunzi wengi hawawezi kuandika projects soo watu wengi huwa wanawandalia final projects na hii unaweza ukakuta cost zao si chini ya laki moja,elfu 80,40, na ukaendelea na maisha kwa kutumia ujuzi

2.kwa mtu ambae ana degree ya accounts plus CPA wengi ya hawa hufungua makapuni ya ukaguzi wa fedha na pia hata kama una mtaji mdogo unaweza ukanunua viti na ubao ukawa unatoa mafunzo kwa wanafunzi wanaosemea masomo ya nabe,atec na mafunzo ya cpe na utapata sana pesa ...ndogo ndogo za kujikimu maana walimu wa haya masomo ni wachache sana.

3.kwa mtu ambae una uwezo wa kutunga stori..una uwezo wa kuandika stori ukatoa kitabu chako na ukapeleleka sokoni mfano wa vitabu ambavyo vipo sokoni ni kama mama yangu anakula nyama za watu, gamboshi hii huwa inalipa sana au kama una stori nzuli yoyote unaweza ukawauzia watu kama kina erick shigongo,rose ndauka huwa wananunua stori na kuzitungia stori kwenye magazeti na unaweza stori moja unauza si chini ya elfu hamsini..

4.kwa wale ndugu zangu mliosoma computer science,IT, na mko fit kwenye programming mnaweza mkafungua ofisi mkawa mnawatengenezea madent wengi final projects ambazo huwa mwisho wa semister huwa wana presents kazi zao infront of lectures so kuna wanafunzi wengine huwa zinawashindaga kufanya soo kama una uwezo unakuwa unawatengenenezea na unaweza kupata pesa kidogo za kujikimu.

5.kwa wale waliopiga computer science,it,compute engineering kama una uwezo kidogo unaweza unaweza ukafungua ofisi yako na kama una computer kama tano au sita unaweza ukafungua college ya kutoa mafunzo ya short course ya computer,IT CONSULTANCY,COMPUTER MAINTANANCE AND REPAIR NA MAISHA YA SONGA.

6.kwa wale ndugu zangu mliosoma degree ya law pia unaweza ukafungua ofisi ya wakili wa kujitegemea nina uhakika kesi haziishi mahakamani utapata sana shavu na pesa ukatumia

7.kwa wale wa clearing and forwarding mliosoma kwa kutumia elimu zenu mnaweza kutumia katika kusaidia kufungua makampuni ya clearing and forwading kwa sababu sasa ivi serikali imekuja na sheria bila mtu kwenye kampuni kuwa na cheti cha clearing from hairuhusiwi kufungua kampuni

8.kwa wale mliosoma mambo ya procurement and suppy na una professional certificate from psptp unaweza ukatumia kufundisha vijana wanaonza kujifunza procurement certifications za psptp either home au sehemu nyingine na ukatoka tuu

9.kwa wale mliosoma mambo ya insuarance pia unaweza ukafungua ofisi na uka act kama broker na ofisi yako ukawa unawapa unasaidia watu kupata huduma yako.

10.pia kwa mtu ambae hana kitu na hana kitu but as longer as your educated unaweza ukafungua tution kwa wanafunzi ukawa unawapiga pindi na siku zikawa zinakwenda....

11.pia na mtu mwingine kama una utaalamu wa mambo ya usafi wa maofisini unaweza ukafungua ofisi yako ukaajiri vijana wengine kama proffesional cleaner cha umuhimu ukawa unajua ni jinsi gani ya kupata madawa ya usafi na vifaa vya kazi....

12.kama wewe ni mtaalamu wa kupika menu nzuli na mwaminifu na una mtaji kidogo unaweza ukaingia mkataba na vyuo kwa ajili ya kutoa huduma ya vyakula,pia kwa mwingine unaweza ukajipanga ukawa unaandaa chakula au chai kwa ajili ya kupeleka maofisini,au mwingine mashuleni ukawa unapata pesa tuu za kujikimuu..

13.kwa wale wa civil enginering,artectures na una utalamu wa kuchora ramani unaweza ukawa una design ramani na kuuza na kampuni yako ikawa ni ndogo ndogo...ukapate mashavuu...

14.kwa wale watalamu wa electronics and telecommunications unaweza ukaweza ukawa unatengeneza vifaa vya electonics kama t.v,passi,computer,laptops,mafridi na vitu vingine na siku zikaenda

15.kwa wale wenye internet full time kama mimi unaweza ukafungua blog,website ukawa una toa taarifa za habali tofauti kwa jamii na kupitia blog yako makampuni yanaweza kuja kutangaza kupitia blog yakoo.

16.pia kwa kutumia internet unaweza ukafungua kampuni yako ambayo inafanya kazi za udalali online mfano unaweza ukafungua website online ya magali ambapo uka sajili customer online ambapo customer anaweza aka order online wewe kazi yako ni kukutana na customer na kumpeleka kwenye hiyoo kampuni na kununua gali....

17.pia kama wewe ni mbunifu sana wa mambo unaweza kwenda kwenye redio au t.v yoyote ukahost kipindi chochote na kama kipindi hikoo kikionekana kina mvuto..basi makampuni mengi huwa yanakuja kudhamini kipindi soo kupitia hivi unaweza ukasonga mbele......

ni hayo tuu kwa leo najua kozi zipo nyingi sana ila nimetaja hizoo chache....ningependa kuanalyse zote ila space na muda but huu ni ushauli wangu tuu...unaweza kuupokea au kutokuupokea but haya ni maujanja natoa ambayo yanaweza yakakupa wewe pesa ndogo za kujikimu huku unafanya mambo mengine... mie nimemaliza chuo bado sijaliwa but me dalali wa magali tuu huku nafanya mambo ya kusaidia vijana wanaopenda kujifunza computer na wananilipa pesa kidogo nina laptop tatu hapa home na life linakwenda
 
MKUU TENA MIMI NINA UHITAJI SANA NA HAO ULOWATAJA NAMBA MBILI,HV NTAWAPATA WAP TUITION PROVIDERS KWA KOZI za NBAA KWA HAPA MOROGORO?
 
Back
Top Bottom