Fahamu jinsi unavyoweza kujua hali ya uchumi kwa kuangalia Deni la taifa

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
666
Moja kati ya kitu ambacho huzungumzwa kwenye uchumi ni deni la taifa, umuhimu wake na ubaya wake.

Deni la taifa huja kutokana na serikali kukopa kwa vyanzo vya ndani au vya nje. Kila serikali duniani imekuwa ikikopa na ili kui-finance miradi yake na kuendelea.

Kukopa sio shida, ila kiwang unachokopa kinaweza kuonyesha nafasi ya uhuru wako kwa wadeni wako. Yaani kama nchi itategemea mikopo kwa zaidi ya 50% hapo lazima nhi hiyo inakuwa ni tegemezi ambayo haiwezi kuwa huru.

Moja kati ya kitu baadhi ya watu wanasema ni kuwa hata nchi zilizoendelea kama Marekani zinakopa.

Tuangalie usahihi watu hao:

Deni la taifa linaweza kutokana na kukopa ndani au kukopa nje.

Deni la Taifa la Marekani kwa data za Mei 28 ni $ Trilioni 25.683, deni la ndani likiwa ni $ Trilioni 19.765 ambayo ni takribani 76.95% deni la nje likiwa ni $ Trilion 5.917 sawa na 23.04%.

Kwa mujibu wa tathmini ya awali ya utekelezaji wa bajeti ya 2019/2020 imeonyesha hadi tarehe 30 Novemba 2019, deni la Serikali lilifikia Tshs. 54.84. Kati ya kiasi hicho, deni la nje ni Tshs. trilioni 40.39 sawa na 73.59% na deni la ndani ni Tshs. trilioni 14.44 sawa na 23.33%

Kwa takwimu hizo utaona nchi gani inautegemezi mkubwa na inaonyesha soko la fedha la ndani haliko vizuri au watu wa ndani hawana ukwasi wa kutosha kushiriki katika soko la pesa.

Hence kwa wale wanaosema hata marekani wana madeni wahakikishe wanajua kuwa deni la Marekani sio la utegemezi kama deni la nchi zinazoendelea, na tukienda mbali kuangalia ratio ya deni la taifa kwa GDP inaweza kuwa shida zaidi.

Sisi bado masikini

Signed

Oedipus
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom