Fahamu immobilizer system kwenye gari

Brainze11

Senior Member
Sep 2, 2012
173
55
Je ulishawahi kusikia watu au fundi anakuambia gari limeingia kwenye immobilizer na ukashindwa kufahamu nini?

Immobilizer ni mfumo wa security ya funguo katika gari. Mfumo huu umewekwa ili kudhibiti wizi wa magari, kwani mtu akichonga funguo aina sawa na gari hawezi kuliwasha.

JINSI MFUMO UNAVOFANYA KAZI

Mfumo huu unafanya kazi kutokana na sensor(transponder) ambayo inakua kwenye funguo wa gari husika, sensor hii hutumika kama utambuzi wa funguo ni sahihi wa gari hilo au la,kama ni sahihi basi sensor hiyo hutoa signal kwenye immobilizer, na immobilizer huruhusu mfumo wa mafuta, spark na ignition kufanya kazi na kuwezesha gari kuwaka.

Kama funguo itakua ni tofauti, basi immobilizer hupata signal tofauti, hivyo basi huzuia mfumo wa mafuta, spark na starter kufanya kazi na kupelekea gari kuto kuwaka.

VITU VINAVYO SABABISHA GARI KUINGIZA FAULT YA IMMOBILIZER

Kwanza kabisa ni ufunguo wa gar kupotea, hii husababisha gari kutokuwaka hata pale utakapochonga ufunguo sawa na wa mwanzo. Kwani inahitajika kuprogram sensor nyingine ambayo itawekwa kwenye ufunguo ili kuwezesha gari kuwaka.

Kudondosha funguo mara kwa mara hii husababisha sensor kuvunjika kwa ndani, pia funguo kuingiliwa na maji kwani hua yanatengezeza unyevu ambao pia una haribu ile sensor na kusababisha gari kuto kuwaka.

BAADHI YA ALAMA ZA TAA KWENYE GARI ILI KUJUA GARI KAMA IMEINGIA KWENYE IMMOBILIZER
9626ce6e847a4927b56237fef894f6c9.jpg
8202bd9564cfe57ee09806a39af309e2.jpg
1330d3fd01797f349fd693096a9817a3.jpg

*KAMA UNA SWALI USISITE KUULIZA*
KWA MAWASILIANO ZAIDI;-
Phone:+255714704097
Email:info@wakudesahrt.com
Website:www.wakudesahrt.com
 
Gari iliyoundwa na immobilizer kuna uwezekano wa kutoa huo mfumo usifanye kazi ili utumie ufunguo wa kuchonga

Inawezekana,ila itahitaji mpaka ubadili mfumo mzima wa umeme wa gari na uweke mfumo mwingine kutoka kwenye gar ambayo haitumii immobilizer
 
Mueleweshe kuwa ukipoteza ufunguo kuna code wamekuandikia unaituma japan wanakuletea funguo nyingine. Kusema za ukweli hii ni ulinzi tosha wa gari na wengine imetusaidia sana
 
Sasa hivi haina haja ya kutuma japana,kwan hata hapa kwa dar inawezekana
 
Out of topic!nataka kubadilisha funguo na ikiwezekana vitasa vyote vya milango vya gari yangu inawezekana boss ...
 
Inawezekana,ila sisi hatu deal na kuchonga funguo. Sisi tunafanya Programming peke yake. Ila kuna fundi anechonga funguo yupo pale sinza anaweza kukusaidia hilo swala lako
 
Je ulishawahi kusikia watu au fundi anakuambia gari limeingia kwenye immobilizer na ukashindwa kufahamu nini?

Immobilizer ni mfumo wa security ya funguo katika gari. Mfumo huu umewekwa ili kudhibiti wizi wa magari, kwani mtu akichonga funguo aina sawa na gari hawezi kuliwasha.

JINSI MFUMO UNAVOFANYA KAZI

Mfumo huu unafanya kazi kutokana na sensor(transponder) ambayo inakua kwenye funguo wa gari husika, sensor hii hutumika kama utambuzi wa funguo ni sahihi wa gari hilo au la,kama ni sahihi basi sensor hiyo hutoa signal kwenye immobilizer, na immobilizer huruhusu mfumo wa mafuta, spark na ignition kufanya kazi na kuwezesha gari kuwaka.

Kama funguo itakua ni tofauti, basi immobilizer hupata signal tofauti, hivyo basi huzuia mfumo wa mafuta, spark na starter kufanya kazi na kupelekea gari kuto kuwaka.

VITU VINAVYO SABABISHA GARI KUINGIZA FAULT YA IMMOBILIZER

Kwanza kabisa ni ufunguo wa gar kupotea, hii husababisha gari kutokuwaka hata pale utakapochonga ufunguo sawa na wa mwanzo. Kwani inahitajika kuprogram sensor nyingine ambayo itawekwa kwenye ufunguo ili kuwezesha gari kuwaka.

Kudondosha funguo mara kwa mara hii husababisha sensor kuvunjika kwa ndani, pia funguo kuingiliwa na maji kwani hua yanatengezeza unyevu ambao pia una haribu ile sensor na kusababisha gari kuto kuwaka.

BAADHI YA ALAMA ZA TAA KWENYE GARI ILI KUJUA GARI KAMA IMEINGIA KWENYE IMMOBILIZER
9626ce6e847a4927b56237fef894f6c9.jpg
8202bd9564cfe57ee09806a39af309e2.jpg
1330d3fd01797f349fd693096a9817a3.jpg

*KAMA UNA SWALI USISITE KUULIZA*
Mkuu kama mtu anahitaji kuchonga ufunguo mwingine ni mpaka akawekewe hiyo sensor? ndo itaweza kuiwasha garihusika?
 
Kama ukichonga ufunguo mwingine itabidi uitoe sensor kwenye ufunguo wa zaman uweke kweny hio uliochonga. Ila kama uta taka kutumia funguo zote mbili hapo itabid upate sensor ingine na ifanyiwe program.
 
Je,kama nataka funguo ya spare
yenye sensor,kampuni yako inasaidiaje?
Naweza kuja na funguo ya kwangu original
mkanitengenezea au kuna utaratibu gani mkuu?
asante.
 
Hapo inabidi uje na gari,kuna kifaa cha kutoa ambacho ndio immobilizer ili kusoma data na kuongeza funguo ya pili ili itambulike kwenye gari.
 
Dah, hii ishu ilinitoka laki 3.5 hivi hivi kizembe zembe,..nilimrushia funguo muosha magari akashindwa kuidaka ikaanguka, utumbo wa ndani ukatoka. Kaiokota kairudisha fresh tu, kujakuiwasha gari ngoma haiwaki (inatekenyeka lakin haipokei). Kwenye dashboard kuna kialama cha funguo kina blink. Kumbe kuna kidude kidogo sana ndio sensa kimepotea funguo ilipo anguka. Laki3 na nusu hivi hivi zikanitoka ili fundi kuchokonoa control box na kuiprogram upya. Niliumia sana kwa uzembe wangu.
 
Pole sana mkuu,funguo hizi zinahitaji umakini na utunzaji, maana naona hata watu wengi wanapenda kuweka funguo ya gari ma simu pamoja,hii pia kwa muda mrefu husababisha sensor kuharibika sababu ya muingiliano wa mawimbi. Sema hua inachukua muda mrefu kwa haraka haraka huwez ona effect zake
 
Back
Top Bottom