Fahamu haya katika Lugha ya Kiswahili

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
28,074
37,545
Najua unajua lakini napenda upate kujua zaidi!
  1. Irabu tano za Kiswahili zina uwezo wa kutengeneza neno kamili pasi na matumizi ya consonant, maneno haya mf ua, oa, au. Kiswahili pekee kinakidhi takwa hili!
  2. Kinadharia JUMATANO inatafsirika katika Kiswahili kuwa ni siku ya Tano katika wiki, cha kustaajabisha zaidi ni kwamba, ALHAMIS (siku ya sita ya wiki katika Kiswahili) ambalo ni neno lenye asili ya Kiarabu, linamaanisha ni siku ya tano katka wiki katika lugha ya Kiarabu!
  3. Katika wimbo wa Marehemu Michael Jackson “liberian girl” kuna maneno ya Kiswahili yanasikika "Naku-penda pia-naku-taka pia-mpenzi wee,". Kwa kukujuza Zaidi, sauti ya maneno haya ni sauti ya Mwanadada, Mwimbaji wa Ki- South Africa Letta Mbulu, na sio maneno ya The Wacko Jacko kama wengi wanavoamini!
  4. Lugha ya Kiswahili ina sauti kuu 5 ambazo ni a, e, i, o na u! kukuongozea Maarifa ni kwamba sauti hizi zinatamkwa sawa na zinavyotamkwa sauti katika Lugha za Kijapan na Kispaniola!
  5. Lugha ya Kiswahili inafundishwa kama Somo katika Vyuo vikuu vikubwa duniani vikiwemo (nitataja vichache) Harvard, Yale, Stanford, Princeton, Pennsylvania. Kwa kukuongezea, Kiswahili kinafundishwa S.O.A.S. ndani ya Chuo Kikuu cha London tangu miaka ya 1930.
  6. Dunia haiishi maajabu. Naomba ujue ukweli huu. Kwa wazungu, neno refu kuliko maneno yote katika lugha ya Kiswahili ni neno: Kipikikusikitishacho! Lakini wanakiri kuwa neno hilo unaweza kulivunja!
  7. Kuna tofauti nyingi za kilugha kati ya Kiswahili na Kiingereza. Nitaweka hapa mbili tu. Mosi ni kwamba, Kiswahili kinatumia herufi zote za lugha ya Kiingereza isipokuwa Q na X! pia katika Kiswahili, kitenzi (verb) kinaunganishwa na kiambishi cha nafsi tofauti na kiingereza ambako kiambishi cha nafsi (pronoun) husimama pekee kama neno! Mfano: KISW: ni-na-kupenda - ni ni kiambishi awali (kinamuwakilisha msemaji) cha nafsi ya kwanza umoja, huku na ni kiambishi kingine cha wakati (kinaonyesha wakati). Katika Kiingereza, i love you! i ni Kiwakilishi (pronoun) kinachosimama chenyewe na love ni verb (kitenzi) nacho chasimama pekee!
  8. Kwa macho na akili za wazungu, msemo maarufu wa Kiswahili ni “Hakuna matata” Msemo huu ulipata umaarufu wake baada ya kutumika katika MOVIE ya The Lion King ambamo humo ndani kuna maneno (majina) mengi ya Kiswahili yametumika. Ukipata wasaa, pitia library upate kuitazama Movie hii!
  9. Inaaminika, maandishi ya kale Zaidi kuwahi kurekodiwa katika lugha ya Kiswahili ni andiko la Mwaka 1711 katika mji maarufu wa Kilwa, andiko hili lilitumwa kwa wareno waliokuwepo Msumbiji, andiko hili katika uhalisia wake linapatikana katika Historical Archive ya Goa nchini India. Kazi ya Sanaa ya kale Zaidi katika Kiswahili ilikuwa ni utenzi uliokuwa ukijulikana kama UTENZI WA TAMBUKA, wa Mwaka 1728. Kwa namna yoyote ile, maandiko yote mawili hayawezi kusomeka na kueleweka kwa wazungumzaji wa leo wa Kiswahili!
  10. Kiswahili ndio lugha nyepesi Zaidi kwa waongeaji wa Kiingereza ama Kiarabu kujifunza katika lugha nyingi za Kiafrika za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kiswahili kinasomeka vile vile kinavyoandikwa! Ukiacha Kiarabu, Kiswahili ndio lugha yenye wazungumzaji wengi barani Afrika.
Naamini umejifunza kitu juu ya lugha yako pendwa!
 
siku hizi wabongo tunatumia x kuandika kiswahili
hayo ni maajabu
 
Naomba ufafanuzi wa namba 6 kwamba KIPIKIKUSIKITISHACHO ni neno moja?
Nijuavyo mimi hayo ni maneno mawili tofauti
 
Naomba ufafanuzi wa namba 6 kwamba KIPIKIKUSIKITISHACHO ni neno moja?
Nijuavyo mimi hayo ni maneno mawili tofauti
Uko sahihi, nimesema kwa mtazamo wa Wazungu wengi! Soma tena Na. 6
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom