Fahamu haya kama unajiandaa na ndoa au tayari upo katika ndoa

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
2,007
2,000
★1. Ukitaka ambacho hakijamilikiwa na mtu yoyote ni lazima ufanye jambo ambalo halijafanywa na yoyote.

★2. Mungu akitaka kukubadili hukuletea mtu na shetani akitaka kukuangamiza pia huleta mtu.

★3. Bora Uishi mwenyewe kuliko kuishi na mtu ambaye si sahihi katika maisha yako.

★4. Kuoana kabla ya kuwa marafiki ni kama gari bila mafuta hamfiki popote.

★5. Aina Tano za wanaume wakuepuka.
Mlevi
Wazinzi
Wagomvi
Wavivu
Wachawi
★6. Aina 5 za Wanawake wa kuepuka.
Walevi
Wazinzi
Wachawi
Wasiotii
Wagomvi

★7. Maneno matatu (3) yanayojenga Amani ni:
Nakupenda
Samahani
Asante

★8. Usiweke kipaumbele chako kwa muonekano na kwamba hutooa/Kuolewa na Mtu Mwenye sura mbaya Bali fahamu kila kitu ni Matunzo.

★9. Asili ya Mikono inayojari ni Moyo Unaothamini na Kujari.

★10. Usioe / Kuolewa na Pesa au Mali , Oa / Olewa na mtu maana Pesa au Mali hufirisika lakini UTU Hudumu milele.

Mwenyezi Mungu Akubariki sana
 

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
5,062
2,000
Kungwi umejitahidi bt ujue ndoa haijawahi pata fomula, chakushangaza zaidi nyie akungwi ndo mnaongoza kuachika/kuachwa
 

Nas Jr

JF-Expert Member
May 15, 2018
4,579
2,000
Mkuu mapenzi ni freestyle

Hakuna kanuni wala sheria,, wala guideline yoyote... Ni mtindo huru..

Alisikika boss wa TFF akisema
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom