Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,540
- 46,075
Uwezo wa akili kwa binadamu umetofautiana kwa viwango na hali mbalimbali, hili ni jambo linalotofautisha hali za maisha na nafasi zao katika mpango wa kijamii. Kuna madaraja kama manne ambayo binadamu wamegawanyika katika uwezo wa akili.
1. Daraja la juu kabisa,hawa mara nyingine huitwa ma-genius, ni watu wenye uwezo mkubwa sana ki akili, wanazaliwa wakiwa hivyo, hata wasiposoma sana wanaweza kufanya mambo ya kushangaza.
Wengi katika hili daraja ni wavumbuzi, composers, wachekeshaji nguli mfano wa George Carlin, waandishi nguli mfano Stephen King, waigizaji nguli mfani Mfano Morgan Freeman na DiCaprio,waandishi habari nguli mfano Mehdi Hasan na wanasayansi wote wakubwa. Wengine ni kina Newton, Galileo, Shaban Robert, Shakespeare, Mozart, Beethoven, Einstein, Bill Gates, Charlie Chaplin, Meryl Streep n.k
Wengi wao huwa hawajihusishi na siasa na vigumu sana kwao kuwa katika nafasi yoyote ya madaraka kwa sababu akili zao zimeegemea zaidi katika sayansi na facts na pia huwa ni vigumu kuvumulia uongo,vitu visivyo na logic, kujipendekeza na fitna za kisiasa.
2. Daraja la juu, hawa ni watu wenye akili za juu kupitia kujifunza na uzoefu, darasani ni wale ambao hupata ufaulu wa juu ya wastani mara nyingi. Huwa wana jitihada sana kupata maarifa zaidi na kujifunza mambo mengi. Uwezo wao mkubwa huwa unatokana na jitihada zao binafsi. Wanajua sana kusoma akili na moves za watu na kuzitumia kwa faida yao.
Wengi wao huwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza connections na madili na mara nyingi huwa ndio wanaofanikiwa zaidi maishani. Wengi wao huwa ndio viongozi wa juu kama Marais, majaji na wabunge. Wengine ni wachambuzi na wafanyabishara wakubwa
3. Daraja la kati, hawa ni wale wenye uwezo kawaida tu,huwa hawana mambo mengi sana, wanahitaji kupata mahitaji ya kawaida tu ya binadamu na wakaridhika. Wengi katika kundi hili ni waajiriwa wanaohitaji nyumba ndogo,mke au mume mzuri na gari ndogo ya kutembelea kisha wafurahie maisha.
Wengi wao ni watu ambao huwa hawapendi sana au hawana uwezo wa kufikiri nje ya mfumo wa maisha walioukuta, waliouzoea, wanaoujua au unaowalisha.
4. Daraja la chini, hawa ni watu ambao mara nyingi huwa na uwezo duni sana kiakili na hutegemea hayo makundi mengi yote kuendesha maisha yao. Kwenye maisha wengi wao huishia kufanya kazi zote zile zinazodharaulika na pia hutumika kama pawns na daraja la pili.