Fahamu chanzo cha wasomi wengi kutokufanikiwa kimaisha na kiutendaji.

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,623
9,165
Habari wakuu,

Nimatumaini yangu mu wazima,
Husika na kichwa cha habari hapo juu cha jieleza,

Mala nyingi wasomi wengi hasa hasa wale waliokuwa wakifanya vizuri darasani kuliko wengine, wengi wao wanamaisha ya kawaida licha ya kuwa na mshahara mnono pamoja na marupu rupu ya kutosha,

Si hapo tu,

Bali hata katika utendaji ufanisi wao ni wa kawaida sana ukilinganisha na wale walio kua medium au moderate performers mashuleni au vyuoni,

Mifano ipo mingi sana but nitaweka michache tu,

Mzee BAKHRESA anautajiri mkubwa sana na kila kukicha anazidi kupanua wigo wake wa kibiashara kwa kuongeza biashara zingine . Alianzia kuuza unga wa ngano kisha kapanua wigo mpaka kwenye biashara ya vinywaji n.k,
Pale UDSM ambapo tunaaminishwa kuwa ndio chuo bora kabisa nchini kuna maprofesor waliobobea kwenye masuala ya biashara na masoko lakini bado wanamaisha ya kawaida wana pesa ya mboga tu, na wanategemea teuzi kutoka kwa viongozi wa serikali ambao miaka kadhaa iliyopita walikuwa ni moderate students,

Tizama taasisi zinazo simamiwa na watu waliokuwa vipanga mashuleni zina hali gani mpaka sasa,
(Utapata jibu sahihi tumia mifano hai),

Sababu ni hii hapa

Unatakiwa uelewe concept mbili ambazo ni MEMORY na THINKING
Memory ni kumbu kumbu na Thinking ni kufikiri/ kutafakari
Ili ufauru mtihani unahitaji MEMORY (kukumbuka kile ulichokisoma), vipanga hufaulu kwa kuwa na uwezo mzuri wa KUKUMBUKA kile walicho kisoma,
Pengine walikuwa vipanga kwa sababu walirudia rudia mara nyingi kusoma kile walichofundishwa,
THINKING (Kufikiri) ndiyo chanzo cha tatizo na ndio sababu inayofanya wasomi wengi kuwa na maisha ya kawaida na kipato cha chini ,

Matajiri wengi ni watu wenye elimu ndogo wanao umiza vichwa usiku na mchana kufikiria na kubuni mbinu za kuwaongezea kipato na kuboresha utendaji ,

Chukua muda kutafakari kwa nini watu wengi wenye GPA nzuri sana lakini hupigwa chini na watu wenye GPA ndogo ktk interview ,
Jibu ni kuwa kinacho angaliwa ni uwezo wa kufikiri na sio kumbu kumbu.

Tujijengee mazoea ya kufikiria na kutafakari.

HUU NDIO UGONJWA UNAO WASUMBUA WAHITIMU WA UDSM,

Karibuni tupigane kwa hoja.

--------------------------------------------------------- --------------------------------------------------------------------
Pata muda wa kutosha kaa peke yako sehemu tulivu, Tumia angalau lisaa limoja kwa siku kutafakari/kufikiria suruhisho la changamoto zinazo kukabili katika maisha na jinsi ya kuongeza kipato chako.
----------------------------------------------------- ------------------------------ --------

To be continue.........
 
Duckworth alitumia muda wake kujifunza kinachosababisha mtu afanikiwe. Alipopata majibu alishangaa. Sio IQ score wala sio GPA wala sio shahada ya chuo kikubwa duniani kinachosababisha mtu kufanikiwa.

La hasha, ila ni muunganiko wa ujasiri,uthubutu na hamu/passion ndio vilivyopo kwenye mioyo ya waliofanikiwa. Achievers they have GRIT.
 
Huyo Duckworth alifanikiwa?
 
Hivi ni kweli wasiosoma ndio wamefanikiwa sana kimaisha? Na mfano mnaoupenda ni SSB. Kuna akina SSB wangapi? Katika top five ya TZ wengine pia hawajasoma? Vipi Mo, RM,RA,Manji?
 
Huyo Duckworth alifanikiwa?
Kwa sehemu alipo naweza kusema amefanikiwa. Mtu ambaye ni Alma wa Havard, Oxford and pennyslvia na bado ana awards amefanikiwa. Japo mafanikio ni neno mtambuka.

Formula ya Grit ni moja kati ya formula zake na zinatumika worldwide mkuu.
 
Hapo kwa upande wangu kafanikiwa, nilifiki katuachia theory tu ila yeye mwenyewe mafanikio anayasikia kwenye bomba...
 
Watu
Hivi ni kweli wasiosoma ndio wamefanikiwa sana kimaisha? Na mfano mnaoupenda ni SSB. Kuna akina SSB wangapi? Katika top five ya TZ wengine pia hawajasoma? Vipi Mo, RM,RA,Manji?
watu wanamtolea mfano kwa sababu pesa katafuta mwenyewe yaani starting from scratch, Mo na manji wamekuta pesa wameziendeleza , mengi labda naye starting from scratch, halafu mwingine anaweza akawa tajiri kutokana na elimu yake ila ukichunguza saana unaona ni mwizi, utajiri wa bakhresa unaoneka ni halali zaidi ni mtu ambaye biashara zake zina interaction kubwa na watu WA kawaida kuliko serikali , wengine kupanda tenda za serikali ambazo zinamagumashi
 
Kwa hiyo
Duckworth alitumia muda wake kujifunza kinachosababisha mtu afanikiwe. Alipopata majibu alishangaa. Sio IQ score wala sio GPA wala sio shahada ya chuo kikubwa duniani kinachosababisha mtu kufanikiwa.

La hasha, ila ni muunganiko wa ujasiri,uthubutu na hamu/passion ndio vilivyopo kwenye mioyo ya waliofanikiwa. Achievers they have GRIT.
Mkuu kwa hiyo makaratasi ya shule hayawezi kukupa utajiri mkuu, ukiangilie mavyeti mengi halafu mfukoni una kitu , unasema bora michael jordan au zidane ambapo walishindwa shule halafu wakatoba maisha, lakini mbona tunaaminishwa shule ndio kila kitu , mi uwa najiuliza hivi kujua calculus au purchasing power parity (PPp) kuna relate hivi na maisha ya kawaida ? Yaani ya maisha pesa
 
Mbona ana degree mbili na yuko level nyingine??

Vipi rostam aziz??? Unadhan hawa wameishia la saba?
 
Watu
watu wanamtolea mfano kwa sababu pesa katafuta mwenyewe yaani starting from scratch, Mo na manji wamekuta pesa wameziendeleza , mengi labda naye starting from scratch, halafu mwingine anaweza akawa tajiri kutokana na elimu yake ila ukichunguza saana unaona ni mwizi, utajiri wa bakhresa unaoneka ni halali zaidi ni mtu ambaye biashara zake zina interaction kubwa na watu WA kawaida kuliko serikali , wengine kupanda tenda za serikali ambazo zinamagumashi
Point yangu ni hii, mfano wa thread kama hizi ni huo huo. Halafu hao unaosema hela wamezikuta uliza walikuta kiasi gani na sasa hivi wameziongeza kiasi gani.
 
Kwa hiyo
Mkuu kwa hiyo makaratasi ya shule hayawezi kukupa utajiri mkuu,?
ukiangilie mavyeti mengi halafu mfukoni una kitu , unasema bora michael jordan au zidane ambapo walishindwa shule halafu wakatoba maisha, lakini mbona tunaaminishwa shule ndio kila kitu , mi uwa najiuliza hivi kujua calculus au purchasing power parity (PPp) kuna relate hivi na maisha ya kawaida ? Yaani ya maisha pesa
Makaratasi hayakupi utajiri ila uthubutu wa kuyatumia. Na ndicho alichosisitiza huyo mmama. Unaweza kuwa na makaratasi mazuri yenye credits kubwa ila usipokuwa na shauku na uthubutu wa kutenda yatakuwa kazi bure.
 
Hivi ni kweli wasiosoma ndio wamefanikiwa sana kimaisha? Na mfano mnaoupenda ni SSB. Kuna akina SSB wangapi? Katika top five ya TZ wengine pia hawajasoma? Vipi Mo, RM,RA,Manji?
Ni njia ya watu kutaka kuhalalisha ujinga. Elimu ni muhimu na wengi wenye standard life Duniani wana elimu hata kama sio filthy rich. Na matajiri wengi pia Wana elimu tofauti na wale wachache ambao hawana elimu
 
Point yangu ni hii, mfano wa thread kama hizi ni huo huo. Halafu hao unaosema hela wamezikuta uliza walikuta kiasi gani na sasa hivi wameziongeza kiasi gani.
Mkuu PRONDO,
Achilia mbali huo mfano, vipi kuhusu utendaji kazi wa wasomi wetu hawa maprofesa kwa jamii nzima especially mawaziri,

TUMIA MUDA WAKO KIDOGO KUTAFAKARI
 
Back
Top Bottom