Fahamu Alama ya Mwanga Juu ya Watukufu na Wenye Hekima ina maana gani

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,920
3,217
Mada hii haipo kidini bali ipo ki-kisayansi na ki-intelectual zaidi.

Kutoka Jitambue Sasa Blog.

Unaweza ukawa uliwahi kuona watakatifu, walimu wenye hekima, walimu wa imani, watawa, Miungu/dieties mbalimbali katika imani mbalimbali duniani wamekuwa wakiwekewa alama ya duara juu ya kichwa chao. Je unafahamu alama hii ina maana gani?


Ulimwengu na elimu yetu inazidi kubadilika. Leo hii tunaweza tukawa tunaona ina maana ya michoro tu au ni style ya kuchora kama aina nyingine za kuchora lakini ningependa sana leo hii kuweza kuielezea katika upande wa nje ya imani ili kusaidia mtu kuelewa vyema. Ninaposema ni kwa upande wa nje ya imani ni kwa maana ya kuwa tutaangalia alama hii ina maana gani katika kila imani. Lengo ni kuweza kufahamu maana hii ambayo leo hii imesahaulika lakini kwa vizazi vya zamani sana vyenye hekima walikuwa na maana kubwa sana juu ya kuweka alama hii.

Kwanza ufahamu kuwa alama hii inaitwa Halo, au Aurola. Ni kama alama ya mwanga, pete ya mwanga, au sahani ya mwanga au kama moto juu ya utosi wa mtu/Miungu/Mtakatifu. Kila jamii ilikuwa inapenda kutumia alama hii kwa maana yake lakini wote walikuwa na maana moja. Inashangaza sana kwani kila imani na kila tamaduni ina maana kuu moja na ilikuwa inatumia kwa watu wa aina moja au wenye sifa zinazoelekea kufanana. Na ndio maana nikapenda leo kuelimisha ufahamu huu ambao niliutafuta kwa kina kutokana na upenzi wangu wa kusoma elimu ya kale kwa lengo la kufahamu busara za zamani ambazo hivi sasa tumezisahau.



Kihistoria.

Hakuna anayefahamu alama hii ilianzia katika jamii gani kiuhakika lakini zipo imani mbalimbali kama vile wagiriki, wamisri na wahindi wamekuwa wakitumia tangu zamani sana hata kabla ya ukristu kuingia.

Alama hii kwa wamisri ilikuwa na maana ya Utakatifu, Usafi, Uungu, na Busara kubwa. Ilikuwa ikipewa alama sawa na Jua kuashiria Mwanga uondoao giza la Ujinga kwa Mwanga wa Elimu ya Juu zaidi.

Wakristu.
Picha ya kale kabisa ya Yesu iliyokuwa imechorwa ilimchora katika Halo juu yake kumaanisha utakatifu, utukufu, Uungu ndani yake.


Yesu akiwa amechorewa Halo nyuma yake.

Yesu pamoja na Wanafunzi wake.


Mbali na kutumika kwa Yesu pamoja na mitume wake, pia alama hii iliendelea kutumika kuonyesha watakatifu, watukufu na wanadamu ambao waliweza kuishi njia ya Mungu au walioweza kuwa mifano kwa wanadamu pia kwa wenye hekima na busara na baraka ya upekee.


Mtakatifu Fransis


Mtakatifu Leo


Mt. Klara
Na wapo watakatifu wengi sana nao wanawekewa alama hiyo juu ya utosi mwao. Wote ni kwa maana moja.

Uislam

Katika Uislam alama hii imetumika hasa sio katika hali ya duara tu bali kama duara la moto katika utosi wa kichwa. Alama hii nayo tangu zamani imekuwa ikiwekwa katika aina ya watu au walimu wenye elimu, busara sawa na maisha sawa na wanadamu wengine waliowekewa kwenye imani nyingine kama uyahudi na ukristu.




Mfalme mtakatifu wa Jahangiri akichorwa na Halo. Mfalme aliyeaminika ni mtakatifu wa Kisufi




Katika uislam maana ya Moto au duara la Moto kwenye utosi wa watakatifu, watukufu na walimu wa imani ilikuwa inamaana inayoendana na wengine. Nayo pia ilikuwa inawekwa kwa wenye sifa moja na sifa sawa kwa maana sawa. Kwa anayetaka kusoma maana yake zaidi asome kapa The Manifestation of Fire and Lightin the Icons of Mir-Heidar?s Miraj Nameh.

Uhindi
Hinduism ni imani ya kale sana kuliko imani nyingi za sasa na ni imani iliyoanza miaka 5500BC kabla ya Yesu, katika Bonde la Mto Hindu. Ni imani inayofahamika kwa kuwa na kitabu cha kwanza cha imani na imani iliyojenga na kusaidia hekima imani nyingi. Nao tangu zamana Walimu wao, Dieties na watakatifu wao walikuwa wanawekewa alama hiyo ya duara kwenye kichwa.


Guru na mwalimu wa Kihindi


Guru akiwa na wanafunzi wake.


Shiva akiwa na Halo juu kichwani


Mtawa aliyeacha maisha ya kawaida na kuishi maisha ya kitakatifu kutafuta KUAMKA.


Mwalimu ALIYEAMKA.
Katika Hinduism maana ya Mwanga huo ni kumaanisha kuwa ni mwanadamu aliyeweka kutumia safari yake ya maisha kuamka. Kuamka ni kuweza kufahamu uhalisia wa maisha. Inaaminika kuwa kuna sehemu kuu saba za Energy ya mwili wa mwanadamu. 1) Chini kabisa kwenye mkia wa uti wa mgongo, 2) Kwenye sehemu ya Uzazi, 3) Kwenye kitofu, 4) Katikati ya kifua na Moyoni, 5) Kwenye Koo/Shingo, 6) Kwenye paji la uso yaani nyuma na Macho mawili yalipo 7) na juu ya Utosi. Hizo ni sehemu kuu zinazozungusha energy ya uhai wa mwili na kuungana na Ufahamu wako. Mtu aliyeweza kuishi katika usahihi, mkamilifu, mwenye busara, aliyeweza kujidhibiti Tamaa za mwili, Ujinga na mwenye upendo kwa wanadamu wote anakuwa na energy flow(upitaji wa nguvu ya uhai) mpaka kwenye utosi na energy hiyo au nguvu hiyo hutoka juu na kuungana na Nguvu kuu ya ulimwengu (Mungu/Ufahamu Mkuu wa ulimwengu) na kukunganisha wewe na yeye. Uhindi huchora alama hiyo kwa Yesu, Mitume na mwanadamu yeyote atakayeweza kuunganisha ufahamu wake na Ufahamu Mkuu.


Ubuddha.

Ubuddha ni imani iliyoanzishwa na Sidharta Guatama aliyeamka na kuwa Mwalimu Buddha (Aliyeamka) Sanamu ya kwanza kabisa ambayo inaonyesha mwalimu Buddha akiwa amechongwa na alama ya Duara nyuma yake.




Hii ni mojawapo ya sanamu ya kale sana iliyopatikana katika kijiji mwalimu Buddha alipoishi kuonyesha Sidharta aliyekuja kuwa Buddha baada ya kuamka.
Mchoro uliomchora Siddharta baada ya kuamka na Kuwa Buddha (Mtu aliyeamka na kupata majibu ya undani wa maisha ulivyo au mwalimu).


Sanamu ya Mwalimu Buddha akiwa na alama ya Halo
Katika Buddhism ni tofauti sana, Buddha alikuwa ni mwanadamu wa kawaida kama wanadamu wengine lakini aliacha kuwa mfalme na kuishi maisha ya kuzurura msituni na walimu wa imani mbali mbali kupata majibu ni kwanini wanadamu wanateseka. Katika maisha yake mpaka anafikisha miaka 29 alikuwa anaishi maisha ya raha katika kasri ya kifalme North India, alikuwa hajui shida wala taabu. Alililewa katika kasri akiwa mtoto wa mfalme na alitegemewa angekuwa mfalme mtarajiwa baada ya baba yake. Lakini siku moja aliona mtu amezeeka, akaona mwingine amekufa na mwingine anaumwa na ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuona hali hizo katika maisha yake, kutokana na alikuwa kwenye kasri ya kitajiri na yenye raha. Akakosa amani na akawa anajiuliza ni kwanini mwanadamu anateseka. Aliamua kutoroka kwani baba yake hakutaka mwanaye awe mwalimu wa imani bali alitaka awe mfalme. Baada ya Budha kutoroka usiku akaenda kuishi porini, akakata nywele zake nzuri, akatoa nguo zote nzuri na kuishi kwa kuvaa mashuka, akawa anaishi maisha ya kuteseka ili tu apate majibu yake kwa kudhibiti tamaa na hamu za kimwili. Alizunguka katika kila imani akitaka kupata majibu ya maisha. Alikutana na walimu waliowahi kuwa watakatifu kwa miaka ile wakamuambia akitaka kupata majibu atafute jibu ndani mwake na sio nje. Akajifunza meditation kufahamu akili ilivyo, akafahamu kufanya meditation kwa muda mrefu na akaishi maisha ya kudhibiti hamu na tamaa zote za mwili. Baada ya miaka sita ya kutafuta majibu siku moja akakaa chini ya mti wenye kivuli (Unaitwa Bodhi), akasema atafanya meditation kuhakikisha anaondoa mawazo yote yaliyopo akilini kwani aliambiwa mwanadamu akiongoza akili na kuondoa mawazo yote akilini na kuwa tulivu kwa muda mrefu anakuwa katika hali ya hekima na atapata majibu yake. Akakaa siku sita bila kutikisika wala kufungua macho wala kuwaza chochote akilini akiweka akili yake kwenye pumzi bila kuwa na wazo lolote. Baada ya akili yake kurudi ndani ya siku ya sita ikarudi na majibu yote na akapata majibu ya maisha na kufahamu kila swali alilokuwa nalo. Akagundua kuwa jibu la maisha lipo ndani ya kila mwanadamu lakini sio kila mwanadamu anaweza kufahamu hilo kutokana na Chuki, Ujinga, Tamaa, Mazoea na Hamu mbaya hupelekea mwanadamu kujitenga na chanzo kikuu ndani mwake. Na Siddharta akaitwa Buddha kumaanisha aliyeamka.

Je Maana ya Halo ni NINI?

Halo katika kila jamii imetumika kumaanisha Utukufu. Kila mwanadamu ana utukufu. Wanadamu wenye Halo hawana tofauti na wewe. Ila tofauti ni kuwa walikuwa kama mwanadamu wa kawaida na wenye akili ya mwanadamu wa kawaida, lakini kutokana na kudhibiti Ujinga kwa kujifunza zaidi, Kutokana na kuongeza hekima, kutokana na kuishi katika utiifu na kushinda tamaa na hamu mbaya hasa za kuupa furaha mwili na kufurahia maisha ya kidunia yaliyo mafupi, na kuweza kuelimisha watu wameweza kuamka na kuungana na chanzo kikuu cha Ufahamu baada ya wao kufahamu ukweli. Mwanadamu ni mchanganyiko wa Ufahamu na Mwili. Mwili huu unapita lakini ufahamu wetu utazidi kuwepo. Kama vile mwili unavyokua na ufahamu nao unakua. Ufahamu hauna mwanzo na wala hauna mwisho lakini mwili huu una mwisho. Wanadamu walioweza kuamka wameweza kuuboresha ufahamu wao na hata baada ya mwili huu kutengana na ufahamu wao, wao watarudi katika chanzo kikuu cha ufahamu. Ufahamu mkuu ndio chanzo cha ufahamu wote. Ndio chanzo cha Kila matter na Energy. Ufahamu mkuu hauna mwili, hauna umbo wala haushikiki wala kuonekana, hauelezeki mpaka wewe mwenyewe uungane nao. Hata ndani yako unao. Kila mwanadamu ameungana nao. Maisha ni ndoto, utakapoamka utagundua mengi tunayatengeneza sisi lakini kiuhalisia ulimwengu ni Empty space. Ni sawa na ndoto. Katika ndoto unaona nikama kweli lakini ukiamka unaona kumbe ilikuwa ni ndoto. Kila mwanadamu ni mtoto wa Muumba. Muumba hana form, hana mwili, hana hali yoyote inayofahamika katika ulimwengu wa milango ya ufahamu (Macho, pua, masikio, ngozi, wala ladha) bali ni zaidi yake.



Ili kuweza kuhakikisha unatumia vyema safari yako ya maisha, dhibiti tamaa zako mbaya, dhibiti hamu mbaya, dhibiti mazoea mabaya, kuwa huru kujifunza chochote na usiamini chochote unachoambiwa au unachosoma katika jamii kwani kila jibu unalo ndani yako, Utambue ufalme wa muhimu sana ndani yako na mwisho tambua kuwa Ndani mwako kuna Ufalme mkuu kuliko falme zote duniani na mali zote duniani. Na upo kwa kila mtu na kila chenye uhai. Ukimtendea mwenzako unajikosea wewe mwenyewe.




Hata wewe unaweza ukawa na Halo/Aurola na unayo tayari juu ya Utosi wako. Una utukufu ndani mwako.




Ubarikiwe sana.
 
Mie sina elimu ya astrology lakini kwenye hili naona kuna vitu vya msingi hujavigusa hususani chanzo cha hiyo halo, uhusiano wake na sayari fulani hivi.....
Na nilizani uvaaji wa earrings, rings, mataji ya kifalme/crowns yanahusiana na haya mambo ya halo?
 
Mie sina elimu ya astrology lakini kwenye hili naona kuna vitu vya msingi hujavigusa hususani chanzo cha hiyo halo, uhusiano wake na sayari fulani hivi.....
Na nilizani uvaaji wa earrings, rings, mataji ya kifalme/crowns yanahusiana na haya mambo ya halo?
Asante.

Sipo katika elimu ya nyota wala sayari. Hivyo sikubaliani na mtazamo huo. Lakini pia nakukaribisha kuelezea. Pia hakuna anayejua alama hii ilianzia wapi, lakini kama nilivyosema, imeonekana Europe, Misri, Middle East, Asia na Maeneo mengi ya jamii za kale. Napenda kuelezea kitu chenye uhakika katika mtazamo wa kweli hivyo kusema alama ilipoanzia, hakuna ajuaye.

Pia hiyo ring ya mwanga/Halo sio Crown/Kofia za kifalme. Hiyo ipo kwenye imani zaidi na ni symbol/Alama na sio kitu cha kushikika wala kutazamika katika milango ya ufahamu ya kimwili (kuonekana, kugusika, etc)
 
Mie sina elimu ya astrology lakini kwenye hili naona kuna vitu vya msingi hujavigusa hususani chanzo cha hiyo halo, uhusiano wake na sayari fulani hivi.....
Na nilizani uvaaji wa earrings, rings, mataji ya kifalme/crowns yanahusiana na haya mambo ya halo?

Hebu mwaga Yale ambayo mdau kasahau au hajaya elezea.
 
Nimejifunza kitu apa asante . ila sijui kwann hii elimu ya kujitambua inakuja kwa kasi sana hasa umu jf

Kitu cha msingi ni wewe kujitambua haijalishi elimu imepatikana wakati gani, na kwanini, hapa hapa JF kuna watu wengi sana ila kumbuka sio wote watakaoiona hii post na kuielewa. Itapendeza zaidi kama utatatafakari na kuchukua hatua
 
Nimejifunza kitu apa asante . ila sijui kwann hii elimu ya kujitambua inakuja kwa kasi sana hasa umu jf

Asante.

Ni kweli kabisa hata nami nimeona mada nyingi za ufahamu na kujitambua. Ni vyema. Ila Elimu hii haijakua Jamii Forums tu. Ni elimu inayochukua nafasi kubwa sana kwa sasa. Zamani ilikuwa ni elimu ya siri sana na waliijua wachache na wakidhubutu kuzungumza wengine walikuwa wanachomwa na kuadhibiwa adhabu ya kifo na makanisa na tawala za kale. Lakini hivi sasa Evolution/Mapinduzi ya akili yanazidi kuwa makubwa na ufahamu wa mwanadamu unazidi kuongezeka na anazidi kuuliza maswali mengi na mwishowe anakuwa huru kutafuta majibu hata nje ya mipaka aliyowekewa na jamii.

Ni vyema mtu kujifunza na kufahamu, ili kuchunguza pande zote na kupata majibu sahihi. Hii ni karne ya Ufahamu. Karne ya mwanadamu huru anayependa kufahamu. Internet, Books, Documentaries na elimu nyingi zipo free kwa sasa. Ila bado ni rahisi mwanadamu kupotoka lakini pia ni rahisi kuiona KWELI. Sio kama zamani. Hivyo ni kuwa makini katika utafutaji wa KWELI na kuipima kila nadharia ili kujua uhakika wake.
 

Asante kwa Link.

Ila ningependa sana kukusaidia ufahamu mada hii haipo katika Aura bali ipo katika Halo. Japokuwa kuna wanaofikiri ni kitu kimoja na kupelekea kutumia jina moja. Na ndio maana katika Link uliyonipatia nimesoma, lakini inazungumzia Aura na sio Halo.

Kila chenye uhai na akili kina Aura lakini sio HALO. Halo ni tofauti na Aura. Halo ipo tu kwa waliofunuliwa, walioamka, God Realized Beings, Divine Beings, Miungu, Watakatifu au watukufu. Halo inahitaji ufahamu kuwa katika Level ya Juu zaidi ndipo unakuwa na Halo. Aura ni low kulinganisha na Halo. Mwenye halo tayari yupo katika level ya God-Realization au God-Consciousness na Muunganiko na Mungu (Ameamka) lakini sio Aura. Aura kila mwanadamu anayo lakini sio kila mwanadamu amefikia hali ya kuwa na Halo.

Ningeomba upitie link utafahamu kwa undani zaidi kwani hujanielewa vyema. Pia nashukuru kwa mchango wako.

Meher Baba: The Aura And The Halo

https://www.facebook.com/notes/chakra-chakra-chakra/the-halo-the-crown-chakra/311086132762

http://avatarmeher.org/the-aura-and-the-halo/

http://the-difference-between.com/halo/aura

[url]https://en.wikipedia.org/wiki/Halo_%28religious_iconography%29

[/URL]
 
Asante kwa Link.

Ila ningependa sana kukusaidia ufahamu mada hii haipo katika Aura bali ipo katika Halo. Japokuwa kuna wanaofikiri ni kitu kimoja na kupelekea kutumia jina moja. Na ndio maana katika Link uliyonipatia nimesoma, lakini inazungumzia Aura na sio Halo.

Kila chenye uhai na akili kina Aura lakini sio HALO. Halo ni tofauti na Aura. Halo ipo tu kwa waliofunuliwa, walioamka, God Realized Beings, Divine Beings, Miungu, Watakatifu au watukufu. Halo inahitaji ufahamu kuwa katika Level ya Juu zaidi ndipo unakuwa na Halo. Aura ni low kulinganisha na Halo. Mwenye halo tayari yupo katika level ya God-Realization au God-Consciousness na Muunganiko na Mungu (Ameamka) lakini sio Aura. Aura kila mwanadamu anayo lakini sio kila mwanadamu amefikia hali ya kuwa na Halo.

Ningeomba upitie link utafahamu kwa undani zaidi kwani hujanielewa vyema. Pia nashukuru kwa mchango wako.

Meher Baba: The Aura And The Halo

https://www.facebook.com/notes/chakra-chakra-chakra/the-halo-the-crown-chakra/311086132762

The aura and the halo – AvatarMeher.org - Avatar Meher Baba Hyderabad Center

Aura vs Halo - What's the difference? | the-difference-between.comhttps://en.wikipedia.org/wiki/Halo_(religious_iconography)
Mkuu nimefuatilia hizo link zako,unajua elimu ni pana sana ningependa kujua kwa kifupi who is Meher Baba,alikuwa ni kiongozi wa kiroho,mwalimu wa imani au?

Kuna vitu hapa vinajenga kuhusu kumpenda Mungu
[h=1]HOW TO LOVE GOD[/h][h=2]Meher Baba[/h]​

To love God in the most practical way is to love our fellow beings. If we feel for others in the same way as we feel for our own dear ones, we love God.

If, instead of seeing faults in others, we look within ourselves, we are loving God.
If, instead of robbing others to help ourselves, we rob ourselves to help others, we are loving God.
If we suffer in the sufferings of others and feel happy in the happiness of others, we are loving God.
If, instead of worrying over our own misfortunes, we think ourselves more fortunate than many many others, we are loving God.
If we endure our lot with patience and contentment, accepting it as His Will, we are loving God.
If we understand and feel that the greatest act of devotion and worship to God is not to hurt or harm any of His beings, we are loving God.
To love God as He ought to be loved, we must live for God and die for God, knowing that the goal of life is to Love God, and find Him as our own self.
 
kuna haja ya kuijua kwa undani zaid hii iman ya Ubuddha, na jins ya ku_meditation. sijui naweza kupata elim kutoka kwako Apollo
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom