Fadhla za Saumu siku ya Ashuraa

njia ya saada

JF-Expert Member
Sep 3, 2018
317
250
b4ecf89eee431776e0dc55cfef0ac617.jpg

Fadhla za Saumu
Asema Mwenyezi Mungu { Enyi mlo Amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andkikwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kucha mungu.(Mfunge) siku maalumu za kuhisabika.na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimiza hisabu katika siku nyingine. Na wale wasio weza watoe fidiya kwa kumlisha masikini na atakaye fanya wema kwa kujitolea, Basi ni bora kwake na Mkifunga ni bora kwenu kama mnajua.} (Al-Baqarah- Aya 183: 185)

Saumu ina fadhila kubwa sana, na thawabu nyingi mno tena maradufu, na kwa hakika Mwenyezi Mungu ameinasibisha saumu kwake yeye kwa ajili ya kuipa utukufu na kuitukuza. Katika Hadithi Al-Qudsy iliyopokewa na swahaba Abu Hurayrah, t Anasema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ: “kila tendo la mwanadamu huongezwa malipo ya wema wake mara kumi ya mfano wa jema hilo alilolitenda mpaka hufikia kuongezwa (huku kwa malipo ya wema huo) hadi nyogeza mara sabiini. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Isipokuwa saumu, kwani hiyo saumu ni yangu mimi, na mimi ndiye mwenye kutoa malipo yake; (mja wangu) anaacha matamanio yake na chakula chake kwa ajili yangu. Katika kufunga saumu kuna furaha mbili: furaha (ya kwanza) ni pale anapofungua saumu aliyefunga, na furaha (ya pili) ni wakati (aliyefunga) atakapokutana na Mola wake. Na harufu inayotoka kwenye kinywa cha aliyefunga ni nzuri sana mbele ya Mwenyezi Mungu kushinda harufu ya miski”.[Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
https://www.al-feqh.com/sw/fadhila-za-saumu-na-hukumu-zake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom