Fadhila za Mwezi wa Ramadhani

njia ya saada

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2018
Messages
280
Points
250

njia ya saada

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2018
280 250
1. Kufunga na kusimama usiku katika mwezi wa Ramadhani hali ya kuwa mtu ana imani na kutaraji malipo basi husamehewa madhambi yake yote yaliyopita. Amesema Mtume Mtume (saw): “Atakayefunga mwezi wa Ramadhani hali ya kuwa ana imani na kutaraji malipo husamehewa yote yaliyotangulia katika madhambi aliyoyafanya” [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Na akasema Mtume Mtume (saw): “Atakayesimama (kuswali usiku) katika mwezi wa Ramadhani hali ya kuwa na imani na kuridhia atasamehewa yote yaliyotangulia katika madhambi aliyoyafanya” [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

2. Ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna ‘Lailatu Al-Qadr’ – ‘Usiku wenye hishima kubwa’ ambao kwamba Mwenyezi Mungu. U amesema kuhusu usiku huu: <> (Al-Qadr – Aya 3).

Atakayesimama usiku huu basi atasamehewa madhambi yake yote yaliyotangulia. Amesema Mtume Mtume (saw): “Yoyote atakayesimama usiku wa cheo hali ya kuwa na imani na kuridhia atasamehewa yote yaliyotangulia katika madhambi yake” [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

3. Kufanya U’mrah ndani ya mwezi wa Ramadhani ni sawa na kuhiji pamoja na Mtume Mtume (saw). Amesema Mtume Mtume (saw): “Kufanya U’mrah ndani ya Ramadhani ni sawa na kuhiji pamoja nami” [Imepokewa na Muslim.].

4. Mwezi wa Ramadhani hufunguliwa milango ya peponi, na hufungwa milango ya motoni, na hutiwa minyororo (hufungwa) mashetani, na nafsi huelekea katika kufanya mambo ya kheri. Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtume (saw): “Unapoingia mwezi wa Ramadhani hufunguliwa milango ya mbinguni, na hufungwa milango ya motoni, na hutiwa minyororo mashetani” [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

5. Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa Qur’an, na ndiyo mwezi ulioteremshwa Qur’an, kwa hivyo inafaa kuzidisha kusoma Qur’an ndani ya mwezi huu, Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwezi wa Ramadhani ni mwezi ambao imeteremshwa Qur’an katika mwezi (huo)} [Al-Baqarah – Aya 185]

6. Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa ukarimu na kutoa sana sadaka. Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas t akisema: “Alikuwa Mtume (saw) mkarimu sana kushinda watu wote katika kufanya mambo ya kheri, na alikuwa mkarimu zaidi wakati wa mwezi wa Ramadhani, hakika Jibril alikuwa akikutana na Mtume kila mwaka katika mwezi wa Ramadhani mpaka uishe mwezi, basi ikawa Jibril wakati kama huu anampitishia Mtume (anaregelea kusoma pamoja na Mtume) Qur’an, basi pindi Mtume anapokutana na Jibril alikuwa Mtume mkarimu sana katika mambo ya kheri kushinda upepo mkali uliotumwa”[Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Kitu gani kitathibitishia kuingia kwa Mwezi wa Ramadhani?
Inathibiti kuingia mwezi wa Ramadhani kwa kuonekana kwa mwezi, utakapoonekana mwezi baada ya kuzama kwa jua siku ya ishirini na tisa katika mwezi wa shabani, basi itakuwa umeshaingia mwezi wa Ramadhani, na ikiwa haukuonekana mwezi baada ya kuzama kwa jua siku ya thelathini ya mwezi wa shabani, au hali ikatanda wingu bila kuonekana mwezi, au kukawa na vumbi kali, au kukawa na moshi (wa umande wa baridi), itakamilishwa mwezi wa shabani siku thelathini; kwa kauli ya Mtume Mtume (saw): “Fungeni kwa kuonekana kwa mwezi na fungueni kwa kuonekana kwa mwezi, na ikiwapitikieni kwamba hamuuoni mwezi basi hisabuni siku thelathini (kukamilika shabani)” [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Fadhla za Saumu na Hukumu zake- Al-feqh
Capture.PNG
 

Forum statistics

Threads 1,389,959
Members 528,065
Posts 34,039,785
Top