Facts za Wasomi ambao Hawachanganyi Elimu na Siasa


PATIGOO

PATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Messages
10,626
Likes
8,996
Points
280
PATIGOO

PATIGOO

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2012
10,626 8,996 280
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, yeye alisema haamini kama alichosema Waziri Ndalichako ni tamko na uamuzi wa Serikali, kwani suala hilo haliko kwenye sera ya elimu na kuonya kuwa alifute haraka kwani hiyo si njia sahihi ya kuboresha elimu nchini.
Dk. Bana alikwenda mbali zaidi kwa kutoa mfano wa jinsi yeye alivyosoma kupitia mfumo huo unaopingwa na Ndalichako hadi hapo alipofikia.
“Kama kachukua uamuzi huo, nafikiri amekurupuka, kama anafikiria kidato cha sita ndiyo njia pekee, ameshauriwa vibaya na huo uamuzi aufute haraka sana na ni kinyume na utaratibu wa elimu kote duniani… utakuwa ni uamuzi wa dhambi ya asili na dhambi ya ubaguzi. Kama anataka njia ya kuboresha elimu aje tumfundishe.
“Mimi binafsi sikupitia kidato cha sita na kuna maprofesa zaidi ya 20 au 40 ninaowafahamu, yupo Profesa Baregu (Mwesiga Baregu) hakusoma kidato cha sita, kuna Profesa Mathew Luhanga ambaye alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa miaka 14, yupo pia Profesa Cuthbert Kimambo ambaye alikuwa Mkuu wa Taaluma UDSM na wengine wengi, ni watu wanaoheshimika kote duniani,” alisema.

PROFESA BAREGU
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Profesa Mwesiga Baregu, hakutofautiana na Dk. Bana. Yeye alisema mfumo uliopo unakubalika duniani kote na ndio ulioleta msemo wa ‘elimu haina mwisho’.
“Kauli ya waziri imeonyesha umuhimu wa kuwa na tume ya kitaifa ya kushughulikia suala la elimu, kwa sababu kweli kuna tatizo la ubora wa elimu yetu na halipaswi kunyamaziwa, lakini hii si njia sahihi ya kulitatua.
“Sijamwelewa waziri kwanini ameona diploma kwenda chuo kikuu ndiyo tatizo na kusema kuwa watu wote wana haki ya kujengewa mazingira ya kujiendeleza kielimu,” alisema Profesa Baregu.

PROFESA MPANGALA
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ruaha mkoani Iringa (RUCO), Profesa Gaudence Mpangala, alisema anapinga uamuzi huo wa Profesa Ndachako kwani utawanyima watu uhuru wa kujiendeleza.

Profesa Mpangala naye aliwataja baadhi ya maprofesa anaowafahamu ambao hawakupitia kidato cha sita na akasema wamekuwa msaada mkubwa kwa taifa.
“Profesa Kimambo alikuwa mwalimu wangu wa Kiswahili, yeye alikuwa na elimu ya ualimu ‘Grade’ C wa shule ya msingi lakini amejiendeleza hadi amekuwa Profesa yupo pia Profesa Ndunguru na wengine wengi na waliopitia mfumo wa Cheti-Stashahada wanakuwa na uzoefu mkubwa kuliko wa kidato cha sita na wanafanya vizuri wakifika chuo kikuu,” alisema Profesa Mpangala.
 
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Messages
15,114
Likes
5,356
Points
280
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2008
15,114 5,356 280
Maprofesa hao wameongea ukweli kabisa. Unajua profesa Baregu na Mpangala hawana njaa kali kama maprofesa wengine wanaochumia tumbo.
 
tikatika

tikatika

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2011
Messages
2,239
Likes
3,664
Points
280
tikatika

tikatika

JF-Expert Member
Joined May 6, 2011
2,239 3,664 280
Hao wanajifanya wanatetea ni kwa vile wameguswa waliko pitia lakn kama dr Bana ni mmoja kati ya wasomi ambao siasa zimetawala kwenye vichwa vyao.

Inatakiwa ajitambue kwa yote na si kwa jambo moja la huo mfumo wa Elim
 
PATIGOO

PATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Messages
10,626
Likes
8,996
Points
280
PATIGOO

PATIGOO

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2012
10,626 8,996 280
Maprofesa hao wameongea ukweli kabisa. Unajua profesa Baregu na Mpangala hawana njaa kali kama maprofesa wengine wanaochumia tumbo.
Umeona mkuu...kila kitu nchi hii wanafanya siasa..hata mambo muhimu ambayo yanagusa jamii kama hili la elimu ..unaamka asubuhi unataka u make headlines unajiuliza leo utamke kitu gan ili uwe kwenye headlines bila kukaa na kutafakar hili nalolisema lina maana yoyote
 
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
25,231
Likes
2,519
Points
280
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
25,231 2,519 280
Acehni undezi wenu,kudanganya watu ktk magazeti hakuwafanyai wapuuzi kuwa watu wenye maana.
 
mlimilwa

mlimilwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
2,091
Likes
1,394
Points
280
mlimilwa

mlimilwa

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
2,091 1,394 280
Nasema hiviii... utawala huu hakuna hata mmoja ambae hata fikiwa,hata wale wanaoshangiliaga bila ya kuhoji,wanajikuata wakiludi makwao wanakuta paka kalala kwenye jiko.lakin pia bado hawajiulizi.watz ni shida sana.
 
PATIGOO

PATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Messages
10,626
Likes
8,996
Points
280
PATIGOO

PATIGOO

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2012
10,626 8,996 280
Acehni undezi wenu,kudanganya watu ktk magazeti hakuwafanyai wapuuzi kuwa watu wenye maana.
Mkuu utajipa jibu mwenyewe kwa kauli yako hii na kauli za maprofesa wanaoheshimika tanzania na hata duniani wanaotoa facts nani ni ndezi kati yao ama wewe.
 
dudus

dudus

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Messages
9,681
Likes
10,098
Points
280
dudus

dudus

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2011
9,681 10,098 280
HUYU DR BANA HIL SUALA LISINGEMGUSA ANGEKAA KIMYA
Yowe limesikika kutokea kichakani; jiwe limegonga penyewe! Na huu ni unafiki mbaya sana; kukaa kimya simply wewe hujaguswa ila kupiga makelele pale wewe unapoguswa na suala ambalo kimsingi ni la kijamii.
 
LebronWade

LebronWade

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
1,618
Likes
1,059
Points
280
LebronWade

LebronWade

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
1,618 1,059 280
HUYU DR BANA HIL SUALA LISINGEMGUSA ANGEKAA KIMYA
Mkuu upo sahihi sana...huyu Bana has always been a suspect,he is never real....

Japokua hoja ni ya kweli ila Bana has always been a fraud to public...hatutetei kabisa...kissing ccm butt kila wakati!
 
DUBULIHASA

DUBULIHASA

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2016
Messages
1,861
Likes
1,892
Points
280
DUBULIHASA

DUBULIHASA

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2016
1,861 1,892 280
Mkuu upo sahihi sana...huyu Bana has always been a suspect,he is never real....

Japokua hoja ni ya kweli ila Bana has always been a fraud to public...hatutetei kabisa...kissing ccm butt kila wakati!
NI MSOMI UCHWARA KABISA
 
DUBULIHASA

DUBULIHASA

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2016
Messages
1,861
Likes
1,892
Points
280
DUBULIHASA

DUBULIHASA

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2016
1,861 1,892 280
Yowe limesikika kutokea kichakani; jiwe limegonga penyewe! Na huu ni unafiki mbaya sana; kukaa kimya simply wewe hujaguswa ila kupiga makelele pale wewe unapoguswa na suala ambalo kimsingi ni la kijamii.
HE IS ONE OF THE OUTSTANDING UNEDUCATED BABOON IN THIS COUNTRY
 
Job K

Job K

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Messages
8,286
Likes
4,445
Points
280
Job K

Job K

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2010
8,286 4,445 280
Wakuu hebu ngoja kwanza nishangae!!

Yaani Dr. Banna naye amekuwa na akili kubwa namna hii siku hizi? Nani amemfua jamani mpaka anapatikana mtu mwenye busara kiasi hiki? Bado siamini kama mwandishi amemhoji Dr. Banna kweli au labda amemfananisha?
 
R

Regnald Patrick Almasi

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2016
Messages
316
Likes
146
Points
60
Age
46
R

Regnald Patrick Almasi

JF-Expert Member
Joined Nov 13, 2016
316 146 60
Mzimu wa matamko unaila nchi kila mwenye dhamana anatamka na inakuwa sheria au serikali imesema....
 
Exaud

Exaud

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2007
Messages
248
Likes
163
Points
60
Exaud

Exaud

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2007
248 163 60
Madaraka sometimes hulevya na kujiona wewe ndio wewe, hata wengine tumeshuhudia wakilitaja bure jina la Mungu.
 
Gaspare Mbile

Gaspare Mbile

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2016
Messages
1,419
Likes
1,345
Points
280
Age
31
Gaspare Mbile

Gaspare Mbile

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2016
1,419 1,345 280
Ilo tamko la elimu lingetamkwa na Rais ni profesa wachache ambao wangekosoa huo mpango, sasa wameona waziri hata wakiongea sawa tu,sasa wawe wajasiri kukosoa yeyote hata Rais pale anapotoa matamko ambayo hayana tija katika jamii,sio wanakuwa waoga na kupindisha ukweli.
 

Forum statistics

Threads 1,274,224
Members 490,631
Posts 30,505,344