Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,399
ichard, post: 29151363, member: 414"]Hivyo viwanda 3000+ mbona ni idadi ndogo sana ndugu yangu unaonekana hujatembea Tanzania sio?
Sasa, ukitaka kuthibitsha hivyo viwanda uende wizarani ila mimi nafahamu mkoa wa Pwani pekee una viwanda vidogo, vya kati na vikubwa.429 kwasababu mimi pia nina interest zangu huko.
Katika hivyo Kibaha pekee ina viwanda 76
Hiyo taarifa ipo mkoani nenda ukatembelee.
Sasa Tanzania ina mikoa mingapi? na ukifahamu hilo viwanda hivyo unavyotaja vinafika hiyo idadi.
Halafu, viwanda si tu vile unavyodhani kwamba ni lazima viwe viwanda vikubwa, kuna vidogo, vya kati na vikubwa.
Richard viwanda 3,000+ tunaambiwa viko mkoa wa Pwani peke yake. Tumewahi kuomba list yake hapa na mahali vilipo. Hilo halijawahi kutokea popote.
Kuna mtu anaitwa jingalao anajua nimeanza kufuatilia hili suala toka mwaka jana mwishoni na post zetu humu jukwaani za ufuatiliaji huo zipo. Nilimtaka aandae jedwali la hivyo viwanda 100@mkoa na vilipo ili tuhamasishe vijana wakaombe ajira. Na yeye amebaki kama ww kutaja idadi. Sikatai kwamba hakuna ujenzi wa viwanda, kwani ujenzi wa viwanda hakuanza enzi za Magufuli bali toka ukoloni. Ninachosema hivyo viwanda 3,000+ ni kweli vipo Pwani?.
Pwani hakuna viwanda 3000 ila kuna viwanda hivyo nilivyokutajia 429
Isipokuwa taarifa sahihi ya idara ya takwimu ambayo tulipewa na waziri Mwijage ni viwanda zaidi ya 50776 na hizo ni takwimu za 2015, vikijumuisha viwanda vidogo binafsi, vya kati na vikubwa.
Lakini tangu raisi Magufuli ameingia madarakani kuna viwanda zaidi ya 3000 ndo vimejengwa au kufufuliwa, na katika hivyo viwanda vikubwa ni 393 vyenye thamani ya dola 2,262 au trillioni shillings 5,198
Kuna viwanda vilivyofufuliwa kama kile cha Mang'ula na kile cha kuchambua Pamba huko Musoma na vingine kama cha MOPROCO na Morogoro Canvas Mills Ltd ambavyo viko Morogoro.
Viwanda vipya vinajengwa kama kile cha maziwa kule Simiyu na kiwanda cha chuma kule Kibaha.
Sasa ukitaka taarifa rasmi ingia wizarani au idara ya takwimu.
Au la tembea ujionee mwenyewe.
Mimi sasa hivi naelekea Dodoma kupata ule mvinyo wa Dodoma Wine made in Tanzania..