Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,439
- 50,961
Kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi wa mwaka huu wa 2020, Rais Magufuli alipopita katika mkoa wa Kagera wilayani Muleba, aliwaambia wananchi wa wilaya hiyo kuwa anafahamiana sana na mheshimiwa Masilingi na kwamba yeye ndiye aliyemteua Masilingi kuwa Balozi Marekani baada ya Ubunge wake huko Muleba.
Ukweli ni kwamba Masilingi aliteuliwa na Rais Mstaafu Kikwete kuwa Balozi wa Marekani mwezi AUGUST 2015, wakati huo Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lakini pia, Ndugu Masilingi hakuwemo kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la mwaka 2010 hadi 2015.
Ukweli ni kwamba ndugu Masilingi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Netherlands mwaka 2013, wakati huo Magufuli ni Waziri.
Tunaomba Wagombea Urais pindi wakijinadi mbele ya wananchi waseme ukweli, Wasidanganye wananchi.
Naiomba na Tume ya Uchaguzi, badala ya kukemea matusi peke yake ikemee wagombea kusema uongo majukwaani.
Wananchi wana haki ya kuambiwa ukweli na siyo kupigwa kamba!
Hapa chini ni video ya Magufuli huko Muleba:
Wakati huo mtandao wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani unasema ifuatavyo kuhusu ubalozi wa Masilingi:
TUNATAKA VIONGOZI WASEMA KWELI