Fact Checking: Rais Magufuli hukumteua Masilingi kuwa Balozi Marekani baada ya kumaliza Ubunge wa Muleba

Kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi wa mwaka huu wa 2020, Rais Magufuli alipopita katika mkoa wa Kagera wilayani Muleba, aliwaambia wananchi wa wilaya hiyo kuwa anafahamiana sana na mheshimiwa Masilingi na kwamba yeye ndiye aliyemteua Masilingi kuwa Balozi Marekani baada ya Ubunge wake huko Muleba.

Ukweli ni kwamba Masilingi aliteuliwa na Rais Mstaafu Kikwete kuwa Balozi wa Marekani mwezi AUGUST 2015, wakati huo Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini pia, Ndugu Masilingi hakuwemo kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la mwaka 2010 hadi 2015.

Ukweli ni kwamba ndugu Masilingi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Netherlands mwaka 2013, wakati huo Magufuli ni Waziri.

Tunaomba Wagombea Urais pindi wakijinadi mbele ya wananchi waseme ukweli, Wasidanganye wananchi.

Naiomba na Tume ya Uchaguzi, badala ya kukemea matusi peke yake ikemee wagombea kusema uongo majukwaani.

Wananchi wana haki ya kuambiwa ukweli na siyo kupigwa kamba!

Hapa chini ni video ya Magufuli huko Muleba:

View attachment 1572029

Wakati huo mtandao wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani unasema ifuatavyo kuhusu ubalozi wa Masilingi:

View attachment 1572036

TUNATAKA VIONGOZI WASEMA KWELI
Tatizo la chadema mmekuwa wajuaji mpaka mnajichanganya wenyewe, hivi mnajua kweli, mnajua mabalozi wanateuliwa na nani na wanahamishwa vituo na nani?? Balozi namba moja ni Rais, huteua wasaidizi yeye.kenge ni kenge tu
 
Kwenye course inayoitwa business communication nilikutana na neno audience analysis unapokuwa unafanya communication na hadhira kama hii lazima ufanye audience analysis,Huenda jiwe alifanya audience analysis akaona vilaza tu vimejazana kwamba hakuna watu makini ndio maana akaamua kuwalisha matango pori
 
Mkuu Missile of the Nation, kwanza Asante kwa bandiko lako la facts checking na asante kutuwekea video clip ya Magufuli alichosema Muleba, Magufuli is very right.

Amesema Masilingi aliteuliwa balozi baada ya kumpisha jimbo Mama Tibaijuka, hata kama mwanzo aliteuliwa na JK, baada ya Serikali mpya kuingia madarakani, Rais mpya anawateua upya mabalozi wote, ma RC wote na ma DC wote, hata kama mwanzo waliteuliwa na mtangulizi wake, re appointment amefanya yeye, hivyo he is right Magufuli amemteua Masilingi.

Moja ya sifa za ziada za Magufuli ni Mkweli Daima!.

Nawashauri Watanzania wenzangu, Wazalendo wa kweli wanaolitakia mema taifa hili, October 25 tusifanye malisa!.
P
Hapa umechemka kaka mkubwa hebu chutama ufiche nyeti zako.
 
Inaelekea hujaisikiliza hiyo clip vizuri, au kama umeisikiliza umeamua kuweka pamba masikioni.

Magufuli anasema alimteua Masilingi kuwa balozi baada ya kumaliza ubunge wake, ukweli ni kwamba Masilingi alikuwa balozi Netherands kuanzia mwaka 2013 hadi 2015, wakati huo Magufuli ni waziri katika serikali ya Kikwete

Kisha Masilingi akateuliwa na Kikwete mwaka 2015 mwezi Agosti kuwa balozi wa Tanzania Marekani. Kwa hiyo JPM anavyodai kuwa alimteua Masilingi kuwa balozi baada ya ubunge wake siyo kweli. Ni kikwete ndiye aliyemteua.

Tunataka Raisi msema kweli
Serikali mpya inapoaingia madarakani kila kitu kinaanza upya kiserikali, Balozi namba moja ni rais, wanaowakilisha nchi wanamwakilisha rais, mwakilishi wa rais anateuliwa na rais mwenyewe.Shida yenu Tund lissu ameshika mpaka ufahamu wenu.
 
Mkuu Missile of the Nation, kwanza Asante kwa bandiko lako la facts checking na asante kutuwekea video clip ya Magufuli alichosema Muleba, Magufuli is very right.

Amesema Masilingi aliteuliwa balozi baada ya kumpisha jimbo Mama Tibaijuka, hata kama mwanzo aliteuliwa na JK, baada ya Serikali mpya kuingia madarakani, Rais mpya anawateua upya mabalozi wote, ma RC wote na ma DC wote, hata kama mwanzo waliteuliwa na mtangulizi wake, re appointment amefanya yeye, hivyo he is right Magufuli amemteua Masilingi.

Moja ya sifa za ziada za Magufuli ni Mkweli Daima!.

Nawashauri Watanzania wenzangu, Wazalendo wa kweli wanaolitakia mema taifa hili, October 25 tusifanye malisa!.
P
Kwa hiyo Masilingi alimpisha Tibaijuka siyo kuwa alipigwa chini .....!!?
 
Kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi wa mwaka huu wa 2020, Rais Magufuli alipopita katika mkoa wa Kagera wilayani Muleba, aliwaambia wananchi wa wilaya hiyo kuwa anafahamiana sana na mheshimiwa Masilingi na kwamba yeye ndiye aliyemteua Masilingi kuwa Balozi Marekani baada ya Ubunge wake huko Muleba.

Ukweli ni kwamba Masilingi aliteuliwa na Rais Mstaafu Kikwete kuwa Balozi wa Marekani mwezi AUGUST 2015, wakati huo Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini pia, Ndugu Masilingi hakuwemo kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la mwaka 2010 hadi 2015.

Ukweli ni kwamba ndugu Masilingi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Netherlands mwaka 2013, wakati huo Magufuli ni Waziri.

Tunaomba Wagombea Urais pindi wakijinadi mbele ya wananchi waseme ukweli, Wasidanganye wananchi.

Naiomba na Tume ya Uchaguzi, badala ya kukemea matusi peke yake ikemee wagombea kusema uongo majukwaani.

Wananchi wana haki ya kuambiwa ukweli na siyo kupigwa kamba!

Hapa chini ni video ya Magufuli huko Muleba:

View attachment 1572029

Wakati huo mtandao wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani unasema ifuatavyo kuhusu ubalozi wa Masilingi:

View attachment 1572036

TUNATAKA VIONGOZI WASEMA KWELI
Kuna mjadala mahali fulani ulifanyika,
Watu wakaulizana, kwani huyu mtawala ni mkali sana na mwongo?

Imekuwa hakuna hata anayeweza kumkabili!
Waliangalia maeneo mengi, mwisho wakahitimisha kuwa mtawala anatumia sana uchawi kuwafanya wapumbae na kuwafanya lolote atakalo.

Wakasema kabla ya 2015 kufanyika uchaguzi alienda kwa Tb Joshua na ndiyo ikawa sababu Tb kuja.

Tb ni freemason member, wakamaliza mjadala kuwa basi huyu nae ni member.

TAFAKARINI MTAONA UKWELI

Siyo kitu cha kawaida mtu mmoja tu aseme atakavyo, atukane atakavyo, aamue kila kitu yeye na hakuna wa kumgusa, kila mtu anatetemeka!!!
SIYO KITU CHA KAWAIDA
 
Muulize anaewateua.
wewe ndiye ulisema kwamba amemuongezea muda. kitu ambacho hujui mpumbavu mkubwa we
ki ukweli hakuna kitu kuongezewa muda kwa balozi.
Kwenye Ubalozi kuna kuteuliwa kuwa Balozi, Kuhamishwa Ubalozi, na Kutenguliwa Ubalozi tu
AKUNA HICHO KITU ULICHOSEMA ETI KUONGEZEWA MUDA WA UBALOZI
Masilingi aliteuliwa na JK , hata credentials zake za ubalozi zina saini ya JK.
Magufuli kadanganya kuhusu yeye kumteua Masilingi ni angeseama niliamua kuendelea naye angeeleweka sio kama alimteua yeye.
 
Tatizo la chadema mmekuwa wajuaji mpaka mnajichanganya wenyewe, hivi mnajua kweli, mnajua mabalozi wanateuliwa na nani na wanahamishwa vituo na nani?? Balozi namba moja ni Rais, huteua wasaidizi yeye.kenge ni kenge tu

Unajua maana ya kuteua?
 
wewe ndiye ulisema kwamba amemuongezea muda. kitu ambacho hujui mpumbavu mkubwa we
ki ukweli hakuna kitu kuongezewa muda kwa balozi.
Kwenye Ubalozi kuna kuteuliwa kuwa Balozi, Kuhamishwa Ubalozi, na Kutenguliwa Ubalozi tu
AKUNA HICHO KITU ULICHOSEMA ETI KUONGEZEWA MUDA WA UBALOZI
Masilingi aliteuliwa na JK , hata credentials zake za ubalozi zina saini ya JK.
Magufuli kadananya kuhusu yeye kumteua Masilingi ni angeseama niliamua kuendelea naye angeeleweka sio kama alimteua yeye.
Huko kumuongezea muda sio kumteua tena? Au lugha ndio inakuchanganya?
 
Serikali mpya inapoaingia madarakani kila kitu kinaanza upya kiserikali, Balozi namba moja ni rais, wanaowakilisha nchi wanamwakilisha rais, mwakilishi wa rais anateuliwa na rais mwenyewe.Shida yenu Tund lissu ameshika mpaka ufahamu wenu.

Nani kakwambia rais mpya akiingia madarakani kila kitu kinaanza upya?

Magufuli alivyoendelea na Makonda wakati huo Makonda akiwa ni mkuu wa wilaya ya kinondoni kabla Magufuli hajamteua ukuu wa mkoa wa DSM je hiyo inahesabika kuwa Magufuli ndo alimteua Makonda ukuu wa wilaya ya kinondoni?

Uraisi ni taasisi ipo, ila watu waitwao maraisi wanakuja na kuondoka.
 
Kuna mjadala mahali fulani ulifanyika,
Watu wakaulizana, kwani huyu mtawala ni mkali sana na mwongo?

Imekuwa hakuna hata anayeweza kumkabili!
Waliangalia maeneo mengi, mwisho wakahitimisha kuwa mtawala anatumia sana uchawi kuwafanya wapumbae na kuwafanya lolote atakalo.

Wakasema kabla ya 2015 kufanyika uchaguzi alienda kwa Tb Joshua na ndiyo ikawa sababu Tb kuja.

Tb ni freemason member, wakamaliza mjadala kuwa basi huyu nae ni member.

TAFAKARINI MTAONA UKWELI

Siyo kitu cha kawaida mtu mmoja tu aseme atakavyo, atukane atakavyo, aamue kila kitu yeye na hakuna wa kumgusa, kila mtu anatetemeka!!!
SIYO KITU CHA KAWAIDA
Duu inaonekana una taarifa nzuri Freemason ni kitu gani mkuu, funguka please
 
Huko kumuongezea muda sio kumteua tena? Au lugha ndio inakuchanganya?
wewe ni mhutu nini kama unayemtetea ? manake nawasiwasi na uelewa wako wa lugha ya kiswahili.
Hivi Kumteua mtu kwenye kazi ni sawasawa na kumuongezea Muda Mtu kwenye kazi?
Kweli kabisa ubongo wako unafikiria sawasawa we mburura?
 
Nani kakwambia rais mpya akiingia madarakani kila kitu kinaanza upya?

Magufuli alivyoendelea na Makonda wakati huo akiwa ni mkuu wa wilaya ya kinondoni kabla hajamteua ukuu wa mkoa inahesabika kuwa yeye Magufuli ndo alimteua Makonda ukuu wa wilaya?

Uraisi ni taasisi ipo, ila watu waitwao maraisi wanakuja na kuondoka.
Mkuu sasa hivi tuko kwenye uchaguzi mkuu ili kupata chama kitakachoshinda na kuunda serikali. Kubali yaishe tuuuuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom