Fact Checking: Rais Magufuli hukumteua Masilingi kuwa Balozi Marekani baada ya kumaliza Ubunge wa Muleba

Saizi Masilingi yupo USA kwa approval ya nani? Sikiliza hyo clip vzr usikae kwenye sentesi moja. Afu usilazimishe Magufuli awe na matamshi/mpangilio wa maneno uupendao wewe. La msingi pata maana ya jumla ya Maelezo yake ndio ulete kwa jamii.

Kwa nn mnapenda kudonoa ka punje ka chuya kwenye gunia la mchele na kufanya ndio sifa ya mchele wote. Wewe huna tongue sleepary?.

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app

Kasema kuwa alimteua Masilingi ubalozi baada ya ubunge wake siyo kweli. Kikwete ndiye aliyemteua kuwa balozi baada ya muda wake

Masilingi amekuwa balozi kabla ya Magufuli kuwa raisi

Kuextend muda wa utumishi wa balozi kwenye ubalozi uliomkuta nao haimaanishi kuwa wewe ndo umemteua, bali unaendelea kubariki uteuzi uliokwisha fanywa na aliyemteua
 
Mkuu Missile of the Nation, kwanza Asante kwa bandiko lako la facts checking na asante kutuwekea video clip ya Magufuli alichosema Muleba, Magufuli is very right.

Amesema Masilingi aliteuliwa balozi baada ya kumpisha jimbo Mama Tibaijuka, hata kama mwanzo aliteuliwa na JK, baada ya Serikali mpya kuingia madarakani, Rais mpya anawateua upya mabalozi wote, ma RC wote na ma DC wote, hata kama mwanzo waliteuliwa na mtangulizi wake, re appointment amefanya yeye, hivyo he is right Magufuli amemteua Masilingi.

Moja ya sifa za ziada za Magufuli ni Mkweli Daima!.

Nawashauri Watanzania wenzangu, Wazalendo wa kweli wanaolitakia mema taifa hili, October 25 tusifanye malisa!.
P
Ona na wewe unatudanganya eti Oct 25!!!. Utetezi wa mtu mwongo haukubaliki hata kidogo. Hangaikia teuzi hizi zinatutoa akili.
 
Mkuu Missile of the Nation, kwanza Asante kwa bandiko lako la facts checking na asante kutuwekea video clip ya Magufuli alichosema Muleba, Magufuli is very right.

Amesema Masilingi aliteuliwa balozi baada ya kumpisha jimbo Mama Tibaijuka, hata kama mwanzo aliteuliwa na JK, baada ya Serikali mpya kuingia madarakani, Rais mpya anawateua upya mabalozi wote, ma RC wote na ma DC wote, hata kama mwanzo waliteuliwa na mtangulizi wake, re appointment amefanya yeye, hivyo he is right Magufuli amemteua Masilingi.

Moja ya sifa za ziada za Magufuli ni Mkweli Daima!.

Nawashauri Watanzania wenzangu, Wazalendo wa kweli wanaolitakia mema taifa hili, October 25 tusifanye malisa!.
P
Magu anaomba hisani kwa Wana Kagera.
 
Ukweli ni kwamba Masilingi hajateuliwa na Magufuri ,Masilingi aliteuliwa na kikwetw, labda hatuambie ni lini Masilingi uteuzi wake ulitenguliwa na Magufuri akaja kumwokota na kumteua. Kwa hyo ukweli ni kwamba Magufuri alichokifanya ni kuendeleza uteuzi wa Kikwete
 
Kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi wa mwaka huu wa 2020, Rais Magufuli alipopita katika mkoa wa Kagera wilayani Muleba, aliwaambia wananchi wa wilaya hiyo kuwa anafahamiana sana na mheshimiwa Masilingi na kwamba yeye ndiye aliyemteua Masilingi kuwa Balozi Marekani baada ya Ubunge wake huko Muleba.

Ukweli ni kwamba Masilingi aliteuliwa na Rais Mstaafu Kikwete kuwa Balozi wa Marekani mwezi AUGUST 2015, wakati huo Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini pia, Ndugu Masilingi hakuwemo kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la mwaka 2010 hadi 2015.

Ukweli ni kwamba ndugu Masilingi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Netherlands mwaka 2013, wakati huo Magufuli ni Waziri.

Tunaomba Wagombea Urais pindi wakijinadi mbele ya wananchi waseme ukweli, Wasidanganye wananchi.

Naiomba na Tume ya Uchaguzi, badala ya kukemea matusi peke yake ikemee wagombea kusema uongo majukwaani.

Wananchi wana haki ya kuambiwa ukweli na siyo kupigwa kamba!

Hapa chini ni video ya Magufuli huko Muleba:

View attachment 1572029

Wakati huo mtandao wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani unasema ifuatavyo kuhusu ubalozi wa Masilingi:

View attachment 1572036

TUNATAKA VIONGOZI WASEMA KWELI
Huyo MEKO (Magufuli) ni muongo siku zote, haelewi anachosema
 
Licha ya kumteua pia amekuwa akimuongezea muda wa kuendelea kuwa balozi huko USA. Nalo pia mtoa post unapingana nalo?

Ivi Magu adanganye kuhusu ubalozi wa Masilingi akiwa anatafuta nn?

Nimegundua haters wa JF walipenda sana JPM apate upinzani BUKOBA ktk kampeni zake cha ajabu Wazirankende wame show love ya kupitiliza kwa mgombea JPM. Watoto wakienda kampeni za Lissu wanakuwa maarufu lkn watoto haohao ktk kampeni kumlaki JPM Bukoba wanakuwa wanatumika. My friends opp politicians jiangalieni na hoja zenu kwetu. Kimsingi huwa mnakosa strong points to stand on. Inawaondolea credibility kwa jamii ya waelewa wa mambo na kuwaona nanyie ni walewale na tena hamna agenda zenye mashiko zaidi ya kuwa haters tu.

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app

Umewahi kuona Masilingi anakula kiapo cha ubalozi mbele ya Magufuli?
 
Huyo MEKO (Magufuli) ni muongo siku zote, haelewi anachosema
Ukimsikiliza Tundu Lissu anaongea zaidi kwa huzuni kuliko hasira sio kama anavyofanya mpinzani wake meko.

Tundu Lissu anaendelea KUSEMA Watanzania wamepoteza maisha yao na kazi zao:kutokana na rais ambaye hasemeleki hataki kukosolewa, analaumu wengine, anakataa ushirikiano na mpenda chuki.
 
Ukweli ni kwamba Masilingi hajateuliwa na Magufuri ,Masilingi aliteuliwa na kikwetw, labda hatuambie ni lini Masilingi uteuzi wake ulitenguliwa na Magufuri akaja kumwokota na kumteua. Kwa hyo ukweli ni kwamba Magufuri alichokifanya ni kuendeleza uteuzi wa Kikwete
Kwa hali ilivyo ipo siku magufuli atatuambia ni yeye aliyemteua profesa Juma Assad, na wapuuzi kama Paskali Mayala watakuja kumtetea.
 
Umewahi kuona Masilingi anakula kiapo cha ubalozi mbele ya Magufuli?
Kama anafanyiwa extension kiapo cha nn? Tambua Magufuli alikuwa na uwezo kikatiba wa kutengua uteuzi wa Masilingi toka siku Magufuli alipo apa kuwa Rais wa JMT 2015.

MASILINGI yupo USA kwa appointment ya JPM huo ndo ukweli aliosema JPM jana kwa ujumla wake. Nakusisitiza kuelewa general concept ya maneno ya JPM Jana na si sentesi moja tu. Otherwise una nia yako tofauti ktk hili.

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Mleta mada anaangalia website tu na kuanza kurusha makombora,

Haelewi jinsi mambo yanavyokwenda.
 
Kampeni zinatoa nafasi ya kuonyesha fikra za ndani za mtu, kama bado kuna aliyekuwa haoni. Ahadi za vyeo kwa bei ya kuombewa kura, kinachosemwa kuhusu amri ya kuwekwa ndani waliokuwa na mawazo kinzani Kagera.

Baada ya miaka 5 ya matumizi mabaya ya vyombo vya sheria, miaka 5 ya yanayosemekana kuwa ni manunuzi ya wabunge wa upinzani japo wangependa kukuaminisha yote hayo yalikuwa ni uungwaji mkono juhudi, mwenye macho haambiwi ona.
 
Mkuu Missile of the Nation, kwanza Asante kwa bandiko lako la facts checking na asante kutuwekea video clip ya Magufuli alichosema Muleba, Magufuli is very right.

Amesema Masilingi aliteuliwa balozi baada ya kumpisha jimbo Mama Tibaijuka, hata kama mwanzo aliteuliwa na JK, baada ya Serikali mpya kuingia madarakani, Rais mpya anawateua upya mabalozi wote, ma RC wote na ma DC wote, hata kama mwanzo waliteuliwa na mtangulizi wake, re appointment amefanya yeye, hivyo he is right Magufuli amemteua Masilingi.

Moja ya sifa za ziada za Magufuli ni Mkweli Daima!.

Nawashauri Watanzania wenzangu, Wazalendo wa kweli wanaolitakia mema taifa hili, October 25 tusifanye malisa!.
P

October 25 kuna nini? au ndio siku ya kuiba kura huko MACCM ? Pascal Mayalla
 
Kama anafanyiwa extension kiapo cha nn? Tambua Magufuli alikuwa na uwezo kikatiba wa kutengua uteuzi wa Masilingi toka siku Magufuli alipo apa kuwa Rais wa JMT 2015.

MASILINGI yupo USA kwa appointment ya JPM huo ndo ukweli aliosema JPM jana kwa ujumla wake. Nakusisitiza kuelewa general concept ya maneno ya JPM Jana na si sentesi moja tu. Otherwise una nia yako tofauti ktk hili.

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app

Naona makada mko busy kupiga kinyesi pafyumu.

Nguo ikiwavuka mchutame! .

Raisi mpya anaweza kuendelea kufanya kazi na mtu aliyeteuliwa na rais mwingine aliyestaafu, hii haimaanishi kuwa mtu huyo kamteua yeye.

Magufuli alipomkuta Sefue kama Katibu mkuu kiongozi akafanya naye kazi kwa miezi ile michache haimaanishi kuwa alimteua yeye

Alipokuta baadhi ya wakuu wa Wilaya aliowateua Kikwete akaendelea nao kwa muda, haimaanishi kuwa aliwateua yeye

Alipokuta makatibu wakuu walioteuliwa na Kikwete akaendelea nao haimaanishi kuwa kawateua yeye.

Kwa hiyo, Magufuli hajawahi kumteua Masilingi kuwa balozi wa nchi yoyote ila tu anabariki uteuzi uliofanywa na Kikwete
 
Ukweli ni kwamba Masilingi aliteuliwa na Rais Mstaafu Kikwete kuwa Balozi wa Marekani mwezi AUGUST 2015, wakati huo Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hapana. Inaweza kuwa kipindi cha uteuzi ule wa kwanza uliofanywa na Kikwete kiliisha, halafu JPM akaamua kumuongezea. Ni kiswahili tu badala ya JPM kusema kuwa alimbakiza ili aendelee kuwa Balozi, akaishia kusema alimteua
 
Hapana. Inaweza kuwa kipindi cha uteuzi ule wa kwanza uliofanywa na Kikwete kiliisha, halafu JPM akaamua kumuongezea. Ni kiswahili tu badala ya JPM kusema kuwa alimbakiza kwa kumteua mara pili ili aendelee kuwa Balozi, akaishia kusema alimteua

Umewahi kuona Masilingi akila kiapo cha uteuzi mbele ya Magufuli?
 
Back
Top Bottom