Fact Check: Chuo kilichompa udaktari wa heshima Mbunge Musukuma ni cha kitapeli, hakiko authentic

Inasikitisha sana tunapoona viongozi waandamizi wa nchi hasa wabunge wakikubali kununua cheap doctorates kutoka vyuo vya kitapeli(rogue colleges). Hiyo inakupa picha kwamba hawa viongozi wetu hawajui hata kuangalia authenticity wakati kila kitu kipo online.Kwanza hiki sio chuo maana hakina address, hakina majengo na wala hakina makao makuu yanayoeleweka. Ni taasisi ya kijanjajanja tuu iliyoanzishwa na matapeli kwa ajili ya kuwatapeli watu wanaotaka umashuhuri nafuu hasa wa udaktari bila kutumia jasho.

Hiki chuo kilichowapa udaktari wa heshima Mbunge Musukuma na wenzake kina kashfa ya siku nyingi ya kuuza hizi degree za heshima. Ukweli ni kwamba wanauza na sio wanatoa bure ama kulingana na mafanikio uliyonayo katika nyanja husika, wakati vyuo vyenye heshima zake na vinavyotambulika huwa vikitoa degree za heshima basi vinatoa na kiasi cha pesa ambayo kwa hapa Tanzania huwa ni pesa ndefu sana.

View attachment 2034779


View attachment 2034780

Soma hii habari iliyoandikwa mwaka 2018 na C-HUB MAGAZINE ambapo walielezea namna hiki chuo cha kitapeli kinavyouza hizi degree za heshima kwa waafrika.


"Baadhi ya Wanigeria mashuhuri huko London, ambao wengi wao ni viongozi wa jamii, wanasheria na waigizaji wa Nollywood wamenaswa katika udaktari bandia wa heshima kwani uhalisi wa taasisi hiyo na tuzo zake zimetiliwa shaka.

Heshima hiyo iliyofahamika kwenye jamii mwaka jana imeuza zaidi ya tuzo 20 kwa Wanigeria wengi kati ya mwaka wao wa mwisho na sherehe ya mwaka huu. Wasomi wanaojali walitilia wasiwasi tuzo hizo wakati picha zilipoibuka za wapokeaji wa tuzo ya heshima ya mwaka huu zilikuwa na umuhimu wa kutiliwa shaka. Wakati hadithi hiyo ikiendelea kuibuka, inakadiriwa kwamba waliopokea zawadi walikuwa wamelipa kila mmoja, kiasi cha pauni 2500 (karibu shilingi milioni 8 za kitanzania) kupokea heshima hiyo.

Wasomi wanaendelea kuhoji uhalisi wa shirika linalotoa heshima kama hiyo na kwa nini lazima iwe Wanigeria wengi. Kwa mujibu wa mwanataaluma mmoja, kutokana na kulitazama gauni hilo, cheti ambacho kina mihuri mbalimbali na jina la chuo, mtu yeyote mwenye chembe yoyote ya uungwana atafanya uchunguzi wa kina kabla ya kukubali upuuzi huo.

Chuo hicho, Academy of Universal Global Peace ambacho kinadai kuidhinishwa na serikali ya Uingereza, Marekani, na India pamoja na Umoja wa Mataifa kinasemekana kuanzishwa na 'Mtukufu' wake Dk. Madhu Krishan mwaka wa 1985, ambaye inadaiwa kuwa pia ni Rais wa Asia 'Power Ministries Intl, Inc. Marekani na anashikilia nyadhifa kadhaa katika mashirika mengi ya kimataifa, baina ya serikali. Dai la heshima kwa jina la mwanzilishi linaendelea na kuendelea, hata hivyo, swali ambalo bado halijajibiwa ni je, ni chuo kikuu gani kimeidhinisha taasisi hii kutoa udaktari wa heshima?

Inakuwa mbaya zaidi kadri maelezo yanavyojitokeza. Ingawa chuo kikuu hicho kinadai kuwa na uhusiano na Umoja wa Mataifa, Tume ya Athari za Kielimu za Umoja wa Mataifa, Tume ya Ulaya, Power Ministries International na Shirika la Amani Ulimwenguni, hata hivyo madai haya yaligunduliwa kuwa sio kweli. Inayoitwa AUGP pia haihusiani na Tume ya Ruzuku ya Chuo Kikuu (UGC) au taasisi yoyote ya kitaaluma ya India.

AUGP, inadai kuwa na makao yake makuu Amerika, hata hivyo haijafahamika ni wapi Marekani makao makuu yapo, wanadai sasa yamehamishiwa Chennai. Mwenyekiti wa Kimataifa wa AUGP, Dk Madhu Krishan, husafiri kimataifa. Hapo awali alikuwa anakaa Amerika kwa miaka kadhaa lakini sasa ana makazi huko Chennai, kwa hivyo makao makuu yako Chennai kwa sasa.

Wakati uchunguzi wetu ukiendelea, ukweli unabakia kuwa, sifa za "chuo" kinachotoa udaktari huu, ziko chini ya wingu la tuhuma. Kufuatia baadhi ya machapisho yao ya mitandao ya kijamii ambayo yanadaiwa kuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Westminster, tumefikia Chuo Kikuu cha London kwa maoni kuhusu uhusiano wao na AUGP na ikiwa wanajua kuhusu udaktari unaouzwa."


View attachment 2034758

View attachment 2034760



View attachment 2034762


Chuo Kikuu kilichopo Japan kinachoitwa United Nations University kiliwahi kukanusha pia madai ya AUGP baada ya kuadai wana ubia kati yao. Hii yote inazidi kuthibitisha kwamba hii ni taasis ya kitapeli.


View attachment 2034765


Hakuna anayepinga hawa waheshimiwa wetu kupata hizo degree za heshima, ila ziwe zinatoka kwenye taasisi zenye heshima na halali. Hizi degree za heshima zinazitolewa na mtu mmoja, tena amesafiri kutoka huko alipo eti kuja kutoa udaktari wa heshima ni utapeli na ni aibu kwa taifa kuwa na viongozi wa namna hii.

Rais Kikwete mwaka 2015 alitunukiwa udaktari wa heshima katika sheria kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle cha nchini Australia, na ukiangalia authenticity yake na hii ya akina Musukuma utagundua ni mbingu na ardhi.


View attachment 2034771


View attachment 2034772


View attachment 2034773




View attachment 2034774



View attachment 2034775



View attachment 2034776

Soma zaidi hapa: Chhattisgarh minister laps up fake honour

Sasa kwanini kina wawakilishi waliosajiriwa Tanzania?

Tatizo ni wajinga wanaojali sana mtu kuitwa Dr sasa mpaka wa Darasa la 4 wataitwa Dr baada ya hapo wananchi wataanza kujali utendaji sio PHD. Vilevile PHD ni kwasababu ya utafiti kwenye eneo tu haina maana yeyote kwa utekelezaji zaidi ya kufundisha/kuwa mwalimu wa chuo mfano Magufuli alipata PHD kuhusu reseach ya Korosho lakini alishidwa na kuaribu soko mpaka sasa wanatapa kurekebisha!
 
Akina Kamala mbona walipeta tu tena baada ya uwaziri akapewa Ubalozi huko kwa TL Belgium? Na mwenzake Nchimbi akapewa ubalozi Brazil...na mpaka leo wanajiita madokta...

Nchi hii wewe ukipata kanafasi katumie. Hutafanywa cho chote. Hakuna uwajibikaji...
Screenshot_20211205-221556_Chrome.jpg
 
kuna miaka mitume na manabii walikuwa wakiponda sana degree, sayansi na usomi kwa ujumla - eti "mbele ya Mungu yote ni bure tu!". Walipopata namna ya kuhitimu bila jasho, siku hizi wote ni madokta au maprofesa wenye hata PhD 3! Na jaribu kuwataja bila kugusia hizo sifa uone kama mtaelewana.

Miaka ya nyuma zaidi walipokuwa hawana pesa, walikuwa wakiwaponda sana matajiri na wenye hali njema kwa vifungu kadhaa kwenye biblia. Walipoanza kutajirika kwa sadaka na mafungu ya kumi mahubiri yakabadilika kuanza kuwaponda wakristo wa muda mrefu ambao bado wanahudhuria vituo vya daladala badala ya kudrive. Kwamba wajichunguze uimara wa imani zao!

Ndio tabia ya "mswahili" kuponda kitu cha maana asichokuwa nacho badala ya kujikubali na kufanya juhudi kukipata.

Fikiria jinsi Watanzania tulivyoanza kujidai kukidharau kiingereza na kuanza kampeni ya kipropaganda ya kuenzi Kiswahili kwa sababu tu tumeshindwa kuimarisha vijana wetu katika lugha hiyo muhimu kwa taifa. Kumbe hata Kiswahili chenyewe tumeshakuwa weak kulinganisha na miaka iliyopita na hata na majirani zetu. Viongozi wanaponda kiingereza huku wanasomesha watoto wao kwenye English medium au International schools!
Mkuu mwenyewe naponda English Ila mwanangu nawaza nimuanzie naseri kule kwa mu7 ili apate real English even Ghana iko poa Sana .Mana ndo best country kwa br English
 
Ndio hawa waliokuwa wakituaminisha kuwa kupiga Nyungu na kunywa kile kinywaji cha Madagaskar kinaponyesha Kirusi hatari cha Covid19

Na yule alieokotwa Jalalani na yule Marehemu mwenye Phd ambae jata hata Kiinglish tu ilikuwa ni shiida

Tanzania yangu imepitia kipindi kigumu sana.
Na yule alieokotwa Jalalani na yule Marehemu mwenye Phd ambae jata hata Kiinglish tu ilikuwa ni shiida

Tanzania yangu imepitia kipindi kigumu sana.
 
Back
Top Bottom