FACT CHECK: Aliyekuwa Mgombea Ubunge wa CHADEMA katika Jimbo la Nachingwea, Dkt Mahadhi Mmoto hajauawa, yupo Mahabusu Gereza la Lindi

Kwa hiyo polisi wakitumia wasiojulikana walimteka siku ya kuamkia uchaguzi?
Mimi nahisi kama naota,
Hii sii kweli ile nchi ya Nyerere.
Naomba iwe ni ndoto na sii kitu halisi.
angalia lakini ukiona choo kwenye ndoto usikitumie sawa
 
Sasa ndugu yangu mtu yuko jela toka tarehe 27, hizo ofisi alichoma lini. Au hata kusoma hujui?! Ndugu yangu acha mihemko ambayo haina tija.
Acha upuuzi, watu wamejichukulia sheria mkononi kwa kuharibu mali ya umma unawatetea! Kwa nini wachome ofisi za serikali na kuharibu mali za wananchi. Hawajui mahakama iko wapi?
 
37 elfu kwa 26 elfu! Duhh! hapo kuna jambo letu limefanyika, hapo mshindi ameshafahamika, Dk omba uzima tu 2025 Mungu atakupa haki yako.
 
Asante kwa ufafanuzi huu,

Umeondoa taharuki iliyoletwa kilaghai.
 
Hivi we unajua gharama na taharuki walioifanya kwa kuharibu vitu vya gharama kubwa na kujeruhi vibaya wewe??
umeielewa ripoti ,mgombea alikamatwa tarehe 27 siku moja kabla ya uchaguzi, fujo zilifanyika tarehe 28 baada ya matokeo kutowaridhisha wananchi,kwa hiyo alitoroka gerezani au kituoni akaenda akaharibu mali za serikali baadae akarudi tena mikononi mwa polisi wakamshitaki kwa kosa la kuharibu mali za umma,ubambikaji mwingine unamfanya mtu anaumia roho hata kama sio ndugu yako anaetendewa hivyo sijui lakini mpandacho ndicho mtakachovuna,
 
Kama ni muhalifu achukuliwe hatua maana hatuwezi kuvumilia vitendo vya kihuni kwenye jamii iliyostaharabika.

Uchaguzi umeisha sasa tuijenge nchi
URT - JPM
SMZ - Mwinyi

CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Back
Top Bottom