Facebook yafungia akaunti za viongozi wa serikali ya Uganda

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Zikiwa zimebaki siku chache kuelekea uchaguzi mkuu nchini Uganda, mtandao wa Facebook umefungia akaunti za viongozi wa serikali kwa tuhuma za kushawishi maamuzi ya umma, mtandao wa AFP umeripoti.

Mkuu wa Mawasiliano wa Facebook wa Ukanda wa Nchi za Kusini mwa Sahara, Kezia Anim-Addo amesema kuwa Facebook imechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa baadhi ya akaunti za mtandao wa Facebook zimejihusisha katika jaribio la makusudi la kushawishi maamuzi ya umma, wakilenga mdahalo unaotarajiwa kufanyika kabla ya uchaguzi.

"Wametumia akaunti feki kuendesha kurasa na kuandika maoni katika machapisho ya watu, wakijivika uhusika wa watu wengine na kusambaza machapisho katika makundi na kuyafanya kuwa maarufu kuliko yalivyotakiwa kuwa," Kezia Anim-Addo alisema katika barua pepe, akiongeza kuwa mtandao wa akaunti hizo unahusishwa na Wizara ya Habari na Mawasiliano ya Uganda.

Hatua hiyo ya Facebook imelaumiwa na wahanga, akiwamo Katibu wa Mawasiliano wa Rais Museveni, Don Wanyama ambaye akaunti zake za Facebook na Instagram zimefungwa, akisema kuwa mitandao hiyo mikubwa inaingilia uchaguzi wa nchi yake.

"Aibu kwa nguvu za kigeni zinazodhani kuwa zinaweza kusimika vibaraka wao kwa kufungia akaunti za wafuasi wa NRM," aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.

"Hamtaweza kumwondoa Rais Kaguta Museveni," aliongeza.



Mitandao ya kijamii imelaumiwa katika siku za hivi karibuni kutokana na kuwapo kwa viashiria vya kuzuia baadhi ya taarifa na kuwafungia watu wanaoonekana kukiuka sera zao za uendeshaji, akiwamo Rais wa Marekani, Donald Trump.
 
Tena wafunge hadi search engine ya Google huko na huduma zote za google. Haiwezekani mtu atake kufilia madarakani.
 
Wamem block Trump mbona nyie ni watu wadogo sana why kulia kulia mmh?
 
Back
Top Bottom