Facebook yaamua kutomfungulia Tump akaunti yake

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Facebook imeamua kutofungulia akaunti ya aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump baada ya kufungiwa kwa kudaiwa kuchochea vurugu katika Jengo la Bunge la Marekani Januari 6 mwaka huu.

Uamuzi huo unafuata baada ya Kampuni hiyo kuifungia akaunti za Trump za Facebook na Instagram kwa muda wa saa 24 baada ya Trump kuchapisha maudhui yanayoonekana kuwasifia wanaofanya vurugu katika Jengo la Bunge, kisha kampuni hiyo ikaendelea kuzifungia akaunti hizo hadi atakapoondoka madarakani.

Uamuzi wa Facebook wa kutoifungulia akaunti hiyo ulitajwa na Mkuu wa Kampuni hiyo, Mark Zuckerberg kuwa umechangiwa na kuona hatari kubwa ya kumwacha Trump kuendelea kutumia mtandao huo kwa wakati huo.

Uamuzi huu wa Facebook umelaumiwa na baadhi ya watu kwa kudai kuwa Facebook imeshindwa kuchukua hatua yenyewe hadi kutegemea uamuzi wa Bodi Huru.

Uamuzi wa leo unatokana na kikao cha marejeo cha Bodi ya Kujitegemea iliyoundwa mwaka 2020 kwa lengo la kufanya maamuzi kuhusu maudhui yaliyo katika majukwaa ya Facebook na Instagram, na inapaswa kufanya kazi bila ushawishi wa uongozi wa Facebook. Bodi hiyo ndiyo iliyotangaza kuwa itaangalia kuzuiwa kwa akaunti za Rais Trump na kuwa inapokea maoni ya umma kuhusu suala hilo.

Wakosoaji wanadai kuwa Bodi hiyo si huru kama inavyojiita, na kuwa imeundwa na kufadhiliwa na Facebook, wakitilia shaka utendaji wake wa kujitegemea.

Trump, hata hivyo, ametangaza kuanzisha mtandao wake wa kijamii, na amefungua tovuti yake kwa lengo la kuchapisha taarifa zake saa kadhaa kabla ya maamuzi ya Bodi hiyo ya Facebook.

Chanzo: The Guardian
 
Donald Trump's ban from Facebook and Instagram has been upheld by Facebook's Oversight Board.

But it criticised the permanent nature of the ban as beyond the scope of Facebook's normal penalties.

It has ordered Facebook to review the decision and "justify a proportionate response" that is applied to everyone, including ordinary users.

The former president was banned from both sites in January following the Capitol Hill riots.

The Oversight Board said the initial decision to permanently suspend Mr Trump was "indeterminate and standardless", and that the correct response should be "consistent with the rules that are applied to other users of its platform".

Facebook must respond within six months, it said.

At a press conference, co-chair Helle Thorning-Schmidt admitted: "We did not have an easy answer."

She added that she felt Facebook would "appreciate the decision".

"We are telling Facebook to go back and be more transparent about how it assesses these things. Treat all users the same and don't give arbitrary penalties."

In response, Facebook said it would "consider the board's decision and determine an action that is clear and proportionate".
 
Back
Top Bottom