Facebook moja wapo ya visababishi vya mahusiano mengi ya kimapenzi kuvunjika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Facebook moja wapo ya visababishi vya mahusiano mengi ya kimapenzi kuvunjika

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Michael Amon, Feb 5, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikifanya tafiti mbali ili kubaini mambo mbali mbali ambayo yanayochangia mahusiano mengi ya kimapenzi kuvunjika. Nadhani wengi wetu tunatambua ya kuwa yapo mambo mengi sana yanachongia mahusiano mengi ya mapenzi kuvunjika ikiwemo usaliti. n.k. lakini tukiachana na yote hayo leo nitaongelea kitu kimoja ambacho kutokana na utafiti nioufanya nimegundua kuwa ni kitu kimoja wapo ambacho kinasabisha mahusiano mengi ya kimapenzi kuvunjika nayo ni Facebook. Natambua ya kuwa zipo social network nyingi lakini hapa nitaongelea facebook kwa sababu ndiyo social network maarufu, inayoongoza, inayopendwa na kutumika na watu wengi duniani.

  Utafiti nilioufanya unaonyesha kuwa facebook imekuwa ni chanzo kimoja wapo cha mahusiano mengi ya kimapenzi kuvunjika na hii ni kutokana na sababu zifuatazo:-
  1. Kutumia muda mwingi kuwa facebook - Sababu moja wapo ambayo inasababisha mahusiano mengi ya kimapenzi kuvunjika ni kutumia muda mwingi kuwa facebook hali inayopelekea kujisahau, kuwasahau wapenzi wao na kutowajali wapenzi wao hali iliyopelekea wao kujikuta wakipoteza wapenzi wao kutokana na wao kutumia muda mwingi kuwa facebook na kuipa attention facebook zaidi kuliko wapenzi wao hali inayosababisha mapenzi kupungua kati ya hao wapendanao. Mfano: Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa na mpenzi wangu ambaye alipenda sana kutumia facebook mara kwa mara hata nyakati ambazo tulikuwa pamoja yeye alikuwa hapay antettion sana na mimi na badala yake attention yake yote ilikuwa kwenye facebook. Nilijaribu sana kumueleza kuhusu tabia yake hiyo lakini hakunisikia hali iliyopelekea kuchukua uamuzi wa kumkataza kutumia facebook na kuidisable account yake permanently. baada ya kufanya hivyo nilishangaa sana kwani mapenzi yake kwangu yaliongozeka ghafla kuliko siku za nyuma na akawa ananipigia simu na kunijulia hali hadi usiku wa manane tofauti na siku za nyuma ndipo nilipogundua kuwa kumbe facebook ndio ilikuwa inamkeep busy na kumfanya yeye aione facebook ni bora zaidi kuliko mimi.
  2. Kulewa sifa - sababu nyingine ambayo inapelekea mahusiano mengi ya kimapenzi kuvunjika kutokana na matumizi ya facebook ni kulewa sifa amabazo huzipata kutoka kwa watu mbali mbali jambo linalomjengea mtu kiburi na kujiona yeye yuko juu na hata kama akiachana na mpenzi wake leo kesho atapata mwingine
  3. Ku Flirt- Sababu nyingine ambayo inapelekea mahusiano mengi kuvunjika kutokana na matumizi ya facebook ni kuflirt. Kutokana na uchunguzi nilioufanya asilimia kubwa ya wanawake na wanaume wengi huwa na wapenzi zaidi ya mmoja kwenye mitandao na hii yote huchangiwa na kuflirt. Watu wengi husema kuwa eti kuflirt ni kitu cha kawaida na haiwezi kusababisha mpenzi wako kukusaliti jambo ambalo si la kweli. Kwa nini ninasema hivyo? Ngoja niwatoleeni mfano huu; Miaka kadhaa iliyopita niliwahi kuflirt na msichana mmoja katika facebook ambaye alikuwa na mpenzi wake. At first nilichukulia kama utani but as time went on mapenzi yalizidi kunoga hadi siku ya siku tukakutana na kuvunja amri ya sita. Kutoka ma mapenzi mazito niliyompa, dada huyo alijikuta akimwacha mpenzi wake na kunifuata mimi pasipo kujali mwenzake anaumia vipi wala ametoka naye wapi.
  Hizi ni baadhi tu ya sababu ambazo zinaweza kuchangia mahusiano ya kimapenzi kuvunjika kutokana na matumizi ya facebook. Ninaomba wanaJF wenzangu tafadhali achaneni na facebook ili msije mkajikuta mnaingia majaribuni na kuwapoteza muwapendao. Waswahili walisema akwambiaye usikombe mboga ujue anataka ushibe na asiyesikia la mkuu huvunjika guu.

  Prepared by:
  Young Master
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kisababishi ni HULKA ya mtu!!!
  Facebook, sijui simu ni virahisishaji tu.
   
 3. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Lakini ukiviendekeza vitakupeleka pabaya
   
 4. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Hilo nalo neno. Ila inategemea na utashi wa mtu, umakini wake na kujitambua kwake.
   
 5. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #5
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Usemayo ni kweli kabisa mkuu.
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ndio maana inabidi uelewe kwamba yenyewe haishababishi mtu awe tofauti na alivyokua, bali inamrahisishia mtu kuwa alivyo.
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  mwanafunzi bado upo?
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  tabia ndo chanzo
   
 9. K

  Kilaza Flani Member

  #9
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Facebook bana..unajichukulia tu,km ulivozipanga..unatumia muda mwingi..unamsifia sana..unamalizia na kuflirt,ushabeba chombo!!so sio kuvunja tu,pia kuanzisha mapya!!

   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Basi mwenyewe unaona umepaaaata kumchukua mtu ambae yeyote akimsifia sifia anamchukua?
   
 11. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #11
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  ujue ninaposema inasababisha inamaana kwamba kama hicho kitu kisingekuwepo basi ujue kisingekuwa kisababishi cha mahusiano mengi ya kimapenzi kuvunjika. Mfano: Kama mbu wasingekuwepo nani angeugua malaria?
   
 12. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #12
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Ni kweli tabia ndio chanzo lakini pia facebook ni kichochezi kwa sababu kinashawishi. Kama facebook isingekuwepo unadhani nani angeflirt? Nani nagepata wa kumtongoza mwenzake online?
   
 13. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #13
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  wewe kweli haufai.
   
 14. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #14
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Nani mwanafunzi?
   
 15. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Lakini pia inajenga mahusiano mapya mkuu, we huoni kama hlo zuri?

  Mtu mpuuzi ni mpuuzi tu hata bila FB!

  Hapa JF pia kuna wapuuzi na malimbukeni wa hizi social networks.
   
 16. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #16
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Anaongea ukweli, mtu kama kakaa mkao wa kubebwabebwa kwanini usimbebe kama wewe mbebaji?
   
 17. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #17
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Ni kweli inasaidia kujenga mahusiano mapya lakini kila kilichokuwa na uzuri hakikosi kuwa na ubaya wake
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Feb 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ndoa zimeanza kuvunjika leo?Watu wameanza kucheat leo?Facebook ndio inayowapeleka watu mpaka guest?
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Feb 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Acha kuechekesha wewe. . .
  Watu wanaflirt maofisini, mabarabarani, madukani, mitaani, safarini leo hii unauliza bila facebook nani angeflirt? Au huo msamiati nao ni mpya?
   
 20. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #20
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hapana mkuu, inasaidia kuonyesha rangi zetu halisi...
  Hivyo ukipata girl na akaweza kusimama kwenye "mapito" hayo ya fb na mitandao mingine (kama ndio kipimo chako) basi utakuwa umejitwalia chaguo bora kwamba pamoja mitandao hyo ila bado anakupa furaha yako.
  So tuiombee zaidi fb.
   
Loading...