Face2Face With Shaka Ssali: Azungumzia African Democracy, Ukosefu wa Uhuru wa Maoni (Freedom of Expression) ni Umasikini Mbaya Kabisa!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,557
Wanabodi,
Heri ya Mwaka Mpya.

Nilikutana na mwandishi nguli wa Afrika, Shaka Ssali, alipokuja nchini Tanzania, kufanya research ya mambo ya demokrasia, amezungumzia mambo mengi yakiwemo, mafanikio yake katika tasnia ya habari na mambo ya demokrasia na uhuru wa kujieleza.

Amezungumzi kuwa yeye ni mzaliwa wa Uganda, mafanikio katika habari, yanapatikana kwa waandishi kufanya research ndipo waandike. Ili mwandishi aweze kufanya reseach, lazima kwanza huyo mwandishi aelimike na ku specialize, yeye ameelimika hadi kiwango cha Ph.D. Hili la elimu na specialization kwa waandishi wetu, nimelikubali ndicho kikwazo kikuu kwa media za Tanzania kushindwa kufanya critical analysis kuhusu habari za kimaendeleo, na mwelekeo wa nchi, angalau kidogo baadhi ya magazeti wanaandika, lakini katika vyombo vya electronics, redio na magazeti, ni almost nil, hakuna kabisa critical analysis, hivyo tv zetu na redia kubaki kufanya reportage na kuishia habari za ziara za viongozi, kujikomba na kuwasifu tuu viongozi na watawala, badala ya kujitika kwenye habari za kimaendeleo, tumetoka wapi, tuko wapi, na tunakwenda wapi, jee tufanye nini hapa tulipo ili tufike kule tunakotakiwa kufika!.

Pia amezungumzia African Democracy vs American Democracy, amesema Baba wa American Democracy Abraham Lincoln ndiye aliyesema "Demokrasia ni Serikali ya Watu, Inayoongozwa na Watu kwa Ajili ya Watu", yaani of the people, by the people and for the people, lakini African Democracy ni ni serikali za baadhi ya watu tuu, zinazoongozwa na baadhi ya watu tuu, kwa ajili ya baadhi ya watu tuu, ikiwemo wengi wa viongozi wa Africa, kuangalia matumbo zao zaidi.

Amemtaja Baba wa Taifa kuwa ni mfano wa viongozi bora kabisa wa Africa ambao waliitanguliza mbele Africa bila kujali matumbo yao, yaani selfless leader.

Pia amezungumzia umasikini kwa kum quote Obama alipozungumza na viongozi wa Africa jiji Accra Ghana, alisema, Umasikini sio umasikini wa mali tuu, bali ukosefu wa uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza ni mfumo wa umasikini mbaya zaidi kuliko umasikini wa mali.

Jee haya aliyoyasema Shaka Ssali yana ukweli kuhusu Tanzania yetu?.

Heri ya Mwaka Mpya.

Paskali
 
Watu wanaweza kuhoji kauli yake kwamba "Baba wa Taifa kuwa ni mfano wa viongozi bora kabisa wa Africa ambao waliitanguliza mbele Africa bila kujali matumbo yao, yaani selfless leader."

Kwa kauli hiyo kwenye RED, Shaka yupo 99% TRUE!! Nimeamua kuweka angalizo manake wengine wanaweza kuleta habari za demokrasia na udikteta wa Mwalimu. Hoja ya Shaka, Mwalimu ni kiongozi bora Afrika kuwahi kutokea kwa sababu, alitanguliza maslahi ya wengi na sio ya kwake mwenyewe!

Kwa kuangalia tulikotokea, Mwalimu alikuwa na uwezo wa kuhamishia Makao Makuu ya nchi Musoma; lakini hakufanya hivyo!!!

Mwalimu alikuwa na uwezo wa kujenga hospitali kubwa kuliko zote kule Musoma au Butiama, lakini hakufanya hivyo!!!

Mwalimu alikuwa na uwezo wa kujenga largest international airport and largest lake Victoria port in Musoma... lakini hakufanya hivyo!!!

Nasema alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo kwa sababu, mosi, enzi hizo kuhoji hoji kulikuwa sio kwingi kama ilivyo sasa!!!

So, kuhusu Nyerere, Shaka yupo sahihi kabisa!!!

Kuhusu demokrasia, nakubaliana nae kwa 95%. Nakubaliana na maelezo yake kwa 100% lakini nimepunguza 5% kwa sababu gari ni gari na bajaj ni bajaj. The so called African Democracy haina sifa ya kuitwa democracy because democracy is ALWAYS "of the people, by the people and for the people."

Hii ya Afrika sio Democracy bali Aristocracy kwa sababu, hata ukiangalia 4 Key Elements of democracy, zote zipo partially exercised.

Stanford University wanaorodhesha 4 Key Elements of Democracy as:
  1. A political system for choosing and replacing the government through free and fair elections.
2. The active participation of the people, as citizens, in politics and civic life.

3. Protection of the human rights of all citizens.

4. A rule of law, in which the laws and procedures apply equally to all citizens.

None of above elements is well exercised in Afrika!

Contrary to Element #1: Way of replacing the government ni ya kutaka kuifanya ruling class irudi tena madarakani

Contrary to Element #2: Only one side of political participation has no barrier to entry... kuchagua the same ruling class warudi tena madarakani.

Contrary to Element #3: Ni mwananchi gani wa kawaida anaweza kupita kifua mbele na kutamba kwamba haki zake za msingi zinalindwa?

Contrary to Element #4: Kuna yeyote anayeweza kuthubutu tumefikia japo 50% kwamba a rule of law applies equally to all citizens?
 
Kuna kiongozi alisema niheri Dr Silaa apate kuwa Rais kuliko TL kupata ubunge kweli yule mkuu aliona mbali leo tunayashuhudia tuombe uhai tutaona mengi
 
Kuna kiongozi alisema niheri Dr Silaa apate kuwa Rais kuliko TL kupata ubunge kweli yule mkuu aliona mbali leo tunayashuhudia tuombe uhai tutaona mengi
NI KWANINI ALITOA KAULI HIYO? INABIDI KUJIULIZA ALITOA KWA KUMDHARAU LISSU NA AMA ALITOA KWA KUWA NI MTU AMBAYE ALIKUWA NA UWEZO WA KUHOJI JUU YA MAMBO? DR. SLAA LEO YUKO WAPI NI BALOZI TENA AKIWAKILISHA NCHI LAKINI AKIWAKILISHA WALE WENYE MADARAKA AMBAO WANAJIONA WAO NDIO WAO NA KUTAMANI HATA KUWA VIONGOZI WA MALAIKA KULE MBINGUNI.
 
Kwa lugha nyepesi kuna mipango ya kimkakati wa uongozi ndani ya nchi yaani kuwepo kwa plan B ya viongozi kuwekwa upinzani exmp ACT na yule katibu wa wizara (Mkubwa mkubo)
 
Wanabodi,
Heri ya Mwaka Mpya.

Nilikutana na mwandishi nguli wa Afrika, Shaka Ssali, alipokuja nchini Tanzania, kufanya research ya mambo ya demokrasia, amezungumzia mambo mengi yakiwemo, mafanikio yake katika tasnia ya habari na mambo ya demokrasia na uhuru wa kujieleza.

Amezungumzi kuwa yeye ni mzaliwa wa Uganda, mafanikio katika habari, yanapatikana kwa waandishi kufanya research ndipo waandike. Ili mwandishi aweze kufanya reseach, lazima kwanza huyo mwandishi aelimike na ku specialize, yeye ameelimika hadi kiwango cha Ph.D. Hili la elimu na specialization kwa waandishi wetu, nimelikubali ndicho kikwazo kikuu kwa media za Tanzania kushindwa kufanya critical analysis kuhusu habari za kimaendeleo, na mwelekeo wa nchi, angalau kidogo baadhi ya magazeti wanaandika, lakini katika vyombo vya electronics, redio na magazeti, ni almost nil, hakuna kabisa critical analysis, hivyo tv zetu na redia kubaki kufanya reportage na kuishia habari za ziara za viongozi, kujikomba na kuwasifu tuu viongozi na watawala, badala ya kujitika kwenye habari za kimaendeleo, tumetoka wapi, tuko wapi, na tunakwenda wapi, jee tufanye nini hapa tulipo ili tufike kule tunakotakiwa kufika!.

Pia amezungumzia African Democracy vs American Democracy, amesema Baba wa American Democracy Abraham Lincoln ndiye aliyesema "Demokrasia ni Serikali ya Watu, Inayoongozwa na Watu kwa Ajili ya Watu", yaani of the people, by the people and for the people, lakini African Democracy ni ni serikali za baadhi ya watu tuu, zinazoongozwa na baadhi ya watu tuu, kwa ajili ya baadhi ya watu tuu, ikiwemo wengi wa viongozi wa Africa, kuangalia matumbo zao zaidi.

Amemtaja Baba wa Taifa kuwa ni mfano wa viongozi bora kabisa wa Africa ambao waliitanguliza mbele Africa bila kujali matumbo yao, yaani selfless leader.

Pia amezungumzia umasikini kwa kum quote Obama alipozungumza na viongozi wa Africa jiji Accra Ghana, alisema, Umasikini sio umasikini wa mali tuu, bali ukosefu wa uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza ni mfumo wa umasikini mbaya zaidi kuliko umasikini wa mali.

Jee haya aliyoyasema Shaka Ssali yana ukweli kuhusu Tanzania yetu?.

Heri ya Mwaka Mpya.

Paskali
Lisu anadai Mwalimu Nyerere alikua Dikteta. Tukiwaambi kua Lisu ni punguani watu awaamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante Pascal Mayalla wewe ni zaidi ya mwandishi wa habari hasa wakati huu tulio nao...

Tanzania inahitaji waandishi wa aina yako, wanasiasa aina ya Lissu ili kujikwamua na kuikwamua serikali hapa tulipo.
Tatizo mkuu Paskal haeleweki.
Anaweza kusifia pasipostahili na kuponda pasipostahili. Nilikuwa na matumaini sana kwako. Una bahati ulionana mwandishi nguli shaka anayefahamu vuzuri maana ya demokrasia. Kama ulimwelewa na unamsifia kwa unafumbia macho kuusema ukweli inapobidi?
 
Back
Top Bottom