Face to Face with Zitto Kabwe: Kuhusu Kupika Data, "Namheshimu Sana Rais Magufuli ila Sio Mkweli!. Uchumi Umesinyaa!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,428
113,433
Wanabodi

Nimekutana na Mhe. Zitto Kabwe katika event ya Policy Forum pale British Council last week, nimefanya nae a short interview ya maswali mawili tuu.
1. Hoja ya yeye kupika data za kiuchumi kwa nini anatofaitiana na mamlaka rasmi za taarifa za makusanyo, nani kati ya serikali na yeye ndie mkweli, au yeye ndie anapika data for political mileage?.
2. Rais wa nchi ni kama baba kwenye familia, rais kasema makusanyo yameongezeka, kumbishia rais ili kuonyeshea rais anasema uongo, huu sio ukosefu wa adabu, heshima na nidhamu?.

Msisikilize Zitto Kabwe mwenyewe.



Paskali
Update
News Alert: - Serikali yamjibu Zitto Kabwe, yasema anapotosha kuhusu takwimu za pato la Taifa

Baada ya serikali kukanusha taarifa hii ya Zitto, hii I namaanisha Zitto amepika data, na kupika data ni kosa la jinai, hivyo sasa tunaisubiria serikali impandishe kizimbani Mhe. Zitto, malumbano haya yakafungwe rasmi.

Paskali
 
Inategemea huyo Baba yako amekuzoesha kumdanganya kwa kiwango gani! Kumbuka sio yeye aliezitengeza hizo Takwimu! Bali kapewa na wajanja wanaojua ni kitu gani anapenda kukisikia! Sitarajii Mzee kama akibebeshwa taka tutaacha kumwambia kwa vile ni baba! Huo utakuwa unafiki wa kufa MTU!
 
Tatizo Magu mwongo, au basi tuseme ni mbumbumbu wa masuala ya Uchumi...na sasa kateua Gavana wake kama alivyoteua, tutarajie KIAMA!
Screenshot_2017-10-29-10-36-18-1.png
 
Halafu upande wa serikali wala sijaona mtu anaeweza kujibu hoja za Zitto kwa kutumia facts and figures!!!

Zitto akisema uchumi umekua kwa 5% halafu ukaonesha Ripoti ya BoT kwamba uchumi umekua kwa 7% wakati ameshasema data zimepikwa; hapo unakua hujajibu hoja manake, ni sawa na Mwislam anayeamini Yesu sio Mungu halafu anataka kumthibitishia Mkristo kwamba ni kweli Yesu sio Mungu lakini reference anayotumia ni Quran!!
 
paskali,mtafute na yule mwanasheria aliyepewa ugavana atuambie atawezaje kujenga hoja za kiuchumi mbele ya wanauchumi wa Benki ya Dunia,IMF na mbele ya magavana wenzie,

na atuambie yale makabati ya accounts aliyasomea wapu au mara ya mwisho aligusa daftari la somo la uchumi
 
Raisi sio baba pascal raisi ni mtumishi wa umma he works for the people tena he is paid to do that its a job.the problem ni kwamba wakiwa maraisi wanajisahau totally just bcoz he is protected wanasahau why they r protected and from whom they are protected against hiki cheo sio cheo kizuri.baba ni kitu kikubwa sana kuliko uraisi no father is paid to be a father while its permanent once a father alwayz a father.tutake radhi kina baba kutufananisha na dhambi za ofisi ya uraisi...
 
paskali,mtafute na yule mwanasheria aliyepewa ugavana atuambie atawezaje kujenga hoja za kiuchumi mbele ya wanauchumi wa Benki ya Dunia,IMF na mbele ya magavana wenzie,

na atuambie yale makabati ya accounts aliyasomea wapu au mara ya mwisho aligusa daftari la somo la uchumi
Kwanza soma hii sheria ya kuhusu uteuzi wa gavana wa BOT especially hapo palipozungushiwa mduara mwekundu baada ya hapo naamini maswali yako mengi yatakuwa yamejibiwa. Ila kiufupi sheria haizuii sababu kumbuka yeye ni mkuu wa taasisi kiutawala ila wataalamu ni hao manaibu gavana watattu NA wengineo huko kwenye idara zao
 

Attachments

  • image.jpeg
    image.jpeg
    105.8 KB · Views: 40
Back
Top Bottom