Face to Face with Zitto Kabwe: Kuhusu Kupika Data, "Namheshimu Sana Rais Magufuli ila Sio Mkweli!. Uchumi Umesinyaa!.

Mtani asante sana. Umempa Mh. Zitto nafasi nzuri ya kujieleza. Na kama mwanahabari nguli hukumuingilia katika maelezo yake.

Mimi sio mwana-habari lakini najiuliza, Mh. Zitto anataka kutueleza nini hapa (what is the NEWS content)?

Serikali imetuambia kitu kimoja na yeye anatuambia kingine. Serikali inatuambia uchumi unaimarika na yeye anasema uchumi unasinyaa. These are finer points for the Economists to ponder.

Je, kutokana na mchakato wake:
☆ Serikali imeiba hela za wananch?

☆ Kuna mchezo mchafu unaofanywa na serikali kuwadhulumu wananchi?

☆ Serikali ina malengo maovu juu ya wananchi wake kutokana na matamshi yake?

☆ Na mengineyo mengi.

Kama serikali inajaribu kwa uwezo wake wote kuwahudumia wananchi wake na kuleta maslahi mema ya taifa letu, kwa nini Mh. Zitto anajaribu kuivua nguo (embarrass) hii serikali?

Kuna mengine mengi ya kujiuliza. Kama anachosema ni kweli:
* Anataka serikali ifanye nini sasa?

* Kuna kitu tofauti ambacho kingepaswa kufanyika nchini hapo nyuma kama anachosema kingejulikana awali?

* Ni kitu gani tofauti kingefanyika leo kama anachokisema Mh. Zitto kikibainika ni kweli?

Sitaki kukuingilia katika taaluma yako mtani lakini haya ndio yangekuwa maswali yangu kwa mgeni wako Mh. Zitto Kabwe.
Kati ya Serikali na Zito nani ni kichwa kigumu zaidi ya jiwe!!???

Hili jambo ni jepesi lakini serikali inatumia nguvu nyingi kutaka kila mmoja aiamini, kumbuka kila mtu ana akili ya kupambanua mambo ndio maana hoja zinaibuka juu ya jambo hili.

Zito ameituhumu Serikali na Serikali ilitakiwa kumjibu Zito kwa uthibitisho ambao utatengua hojabza Zito na kuonekana ni za kupika, lakini ninyi watetezi wa serikalina kuja na hoja eti bwana mkubwa kasema uchumi unakuwa na tuaamini hivyo hivyo bila kuzingatia vigezo vyote vinavyopelekea uchumi kukua kama vipo sahihi au la.

Huyo bwana mkubwa wenu kwani hakosei? (Sadam Husein alikuwa Rais wa Libya, hapana alikuwa Rais wa Kuwait)

Jibuni hoja za Zito kwa data zote ambazo Zito kasema zimepikwa ili wananchi tujiridhishe ukweli ni upi na uongo ni upi!

 
Sasa Paskali mbona ndio umemuumiza zaidi president wetu? Yaani ni kama umempa Zitto nafasi ya kushindilia vizuri msumari, Lol!!

Nishawaambia Zitto asipewe nafasi ya kujieleza, bado hatuna mtu wa kujibishana nae kwa hoja na data. Atatuumbua zaidi

Mark my words:

BoT, TRA, National Statistics na CAG sasa hivi watakatazwa kupublish tena data kwa jamii. Vyote vitakuwa vinaishia kwenye makabati.

Hizi data zinaleta uchochezi na kuharibu usalama wa nchi.

Zitto anatumia kamba zao kuwanyongea.
 
Wanabodi

Nimekutana na Mhe. Zitto Kabwe katika event ya Policy Forum pale British Council last week, nimefanya nae a short interview ya maswali mawili tuu.
1. Hoja ya yeye kupika data za kiuchumi kwa nini anatofaitiana na mamlaka rasmi za taarifa za makusanyo, nani kati ya serikali na yeye ndie mkweli, au yeye ndie anapika data for political mileage?.
2. Rais wa nchi ni kama baba kwenye familia, rais kasema makusanyo yameongezeka, kumbishia rais ili kuonyeshea rais anasema uongo, huu sio ukosefu wa adabu, heshima na nidhamu?.

Msisikilize Zitto Kabwe mwenyewe.



Paskali

Teeeeeeh teeeeeeh teeeeeweh Pasco hadi unaweka hadi nambari ya simu ili upigiwe?hawana time na wewe ndugu yangu
 
Raisi sio baba pascal raisi ni mtumishi wa umma he works for the people tena he is paid to do that its a job.the problem ni kwamba wakiwa maraisi wanajisahau totally just bcoz he is protected wanasahau why they r protected and from whom they are protected against hiki cheo sio cheo kizuri.baba ni kitu kikubwa sana kuliko uraisi no father is paid to be a father while its permanent once a father alwayz a father.tutake radhi kina baba kutufananisha na dhambi za ofisi ya uraisi...
umeandika kwa busara sana
 
Raisi sio baba pascal raisi ni mtumishi wa umma he works for the people tena he is paid to do that its a job.the problem ni kwamba wakiwa maraisi wanajisahau totally just bcoz he is protected wanasahau why they r protected and from whom they are protected against hiki cheo sio cheo kizuri.baba ni kitu kikubwa sana kuliko uraisi no father is paid to be a father while its permanent once a father alwayz a father.tutake radhi kina baba kutufananisha na dhambi za ofisi ya uraisi...
Mungu akuzidishie kila lenye kheri na maisha marefu mkuu
 
Back
Top Bottom