F.T: NBC Premier League | Simba SC 3 - 0 Biashara United | Uwanja wa Benjamin Mkapa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,261
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC) Premier League kuendelea kuvurumishwa leo March 4, 2022 ambapo kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera Sugar wanakipiga na Namungo FC, saa 10: 00 Jioni, huku wakali wa CAF, Mnyama Mkali Mwituni, Simba SC wakikipiga na Biashara United kutoka mkoani Mara katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo wa Simba SC dhidi ya Biashara United unatarajiwa kuwa mkali na kusisimua hasa ukizingatia timu zote mbili kihitaji alama tatu muhimu.

Kocha wa Simba SC Pablo Franco, amesema kuwa mchezo utakuwa mgumu, Biashara United ni nzuri na ina wachezaji wazuri mmoja mmoja hata hivyo tunahitaji kushinda ili kupunguza idadi ya alama na anayeongoza, hivyo tunategemea ushindi.

Kwa upande wa Kocha wa Biashara United Vivier Bahati, amesema Tunaimani kwamba Mchezo utakuwa nzuri, na tutapata matokeo mazuri, tukitazama maandalizi yetu yapo vizuri.

Mara ya mwisho kukutana, Simba SC waliibuka kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Biashara United. Je? Nani kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo, dakika 90 za mchezo kuamua. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 Usiku. Usikose Ukaambiwa.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

....... Ghazwat.....


Naaam mpira umeanza uwanja wa Benjamin Mkapa.

00' Mpira umeanza kwa kasi huku Biashara United wakifanya jaribio la kwanza.

05' Umiliki wa Simba SC sasa huku lakini Biashara United wanazuia maridadi kabisa.

08' Sakho Goooooooooooooaaal gooal

Pape Sakho anaipatia Simba SC bao la kwanza kwa shuti kali akipokea pasi kutoka kwa Kapombe | Simba SC 1-0 Biashara United.

10' Biashara United alianza vizuri lakini sasa kasi yao inapungua sijui kwanini.

13' Mzamur Goooooooooooooaaal gooal
Mzamur Yasin akipokea pasi kutoka kwa Kapombe | Simba SC 2-0 Biashara United

Biashara United wanazidiwa hapa Uwanja wa Benjamin Mkapa. Haya wanakwenda Simba kutafuta bao la tatu, kwake Sahkooo anampasia chamaaaa

18' Chamaaaa Goooooooooooooaaal gooal

Chama anaipatia Simba SC bao la tatu kazi bomba kutoka kwa Sahko | Simba SC 3-0 Biashara United

Mpira unachezea katikati ya Uwanja huku Umeliki ukiwa kwa Simba, Biashara wanautafuta kwa tochi

25' Biashara wameamka wapeleka mashambulizi upande wa Simba SC walau sasa wanaamka.

30' Ametoka Shomari Kapombe baada kugongana mchezaji wa Biashara United hivyo kuumia na ameingia Patrick upande wa Simba SC.

35' Mkwaju wa mchezaji wa Biashara unatoka nje ya lango | Simba SC 3-0 Biashara United.

41' Biashara United wanapata Kona ambayo haikuzaa matunda, hakuna matumaini ya kupata bao kwa dakika hizi za mwanzo.

Bocco anashindwa kuandika bao la nne hapa, ilikuwa nafasi nzuri kwake baada ya kazi nzuri ya Sakho.

46+2' Kuelekea kuwa mapumziko Uwanja wa Benjamin Mkapa

Naaam mpira ni mapumziko ambapo Simba SC wanatoka wakiwa mbele ya mabao matatu kwa bila | HT: Simba SC 3-0 Biashara United

Kipindi cha pili kimeanza huku Simba SC wakifanya mabadikio, ametoka Bocco na ameingia Kagere.

50' Biashara United wanapata Free Kick, anapiga Lidondo shuti, lakini Simba wanaokoa.

53' Hussein anafanyiwa faulo, ni Free Kick kuelekea Biashara United, anapiga Chamaaa, lakini kichwa cha Inonga kinashindwa kulenga lango.

58' Boniface Maganga anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumchezea vibaya Sakho.

60' Peter Bandaaa looooo shuti kali linagonga mlingoti almanusura Simba wapate bao.

65' Biashara United wanafanya mabadikio ya wachezaji wawili huku Simba pia wakifanya mabadikio kwa kutoka Inonga, Sakho, na ameingia Morrison, Kennedy

75' Biashara wanakazi ya kurudi mambo lakini, Simba wanakaa vyema huku Nyoni akionyeshwa KADI ya Njano

Hatar sana lango la Simba, lakini Biashara United Jaribio lao linashindwa kuzaa matunda kwa mpira kupaa nje ya lango.

88' Baada ya gonga za hapa na pale Patrick anakosa nafasi nzuri ya kufunga ilikuwa nafasi sana lango la Biashara.

99+2' Kuelekea kumalizika kwa mchezo huku Simba wakipata Penalty baada ya Morrison kufanyiwa faulo eneo la 18.

Anakwenda kupiga mkwaju wa penalty ni Maddie Kagere anapiga anakosa Oooh anadaka Sstuba golikipa wa Biashara United

Naaam mpira umekwisha ambapo Simba SC wanaibuka na ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya Biashara United.

FT, NBC; Simba SC 3-0 Biashara United

...... Ghazwat.....
 
Yaliyojiri:

Mchezo kati Kagera Sugar na Namungo FC, umemalizika kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera kwa timu hizo kugawana alama baada ya kufungana bao moja kwa moja, Kagera Sugar wakitangulia kufunga kupitia kwa Mbaraka Yusuf wa kichwa 22' huku Namungo FC wakichomoa kupitia kwa Emmanuel Charles 26'

90+3'

FT: NBC' Kagera Sugar 1-1 Namungo FC
 
20220304_180145.jpg
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom