Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,444
- 7,799
Mbunge wa Biharamulo, Ezra Chilewesa akiwa Bungeni ametambua juhudi za Hayati Magufuli kwenye jimbo lake kwa kuhakikisha anawatoa kwenye pori la Burigi ambalo lilitumika kwenye utekaji na unyanyasaji wa watu wa Biharamulo kwa muda mrefu na kuwa sehemu ya kujivunia.
Mbunge Ezra amesema pamoja na hayo, hifadhi hiyo imekuwa na kelele kidogo kwa wakazi wa Biharamulo kutokana na jina la hifadhi. Amedai wakazi hao wameona jina limeifanya kuwa chini ya Chato ilhali sehemu ya mbuga hiyo iko Biharamulo.
Ameomba sehemu yenye neno Burigi ibadilike na liwepo neno Biharamulo na kusomeka Biharamulo-Chato Ntaional Park.