Eyes on Kenya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eyes on Kenya

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by Rev. Kishoka, Dec 4, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Eeehh hii mitu ya gibande ya gaskazini mwa inji yetu inatuzidi marifa!

  Ati wamefanya promosheni kwenye Televisheni huku Marikani wakijitanga-tangaza.

  Masaa mawili vile nakaa natazama Televisheni kuiangalia Kenya. Yuko yule mjamaa alichezaga James Bond, Sir Roger Moore, yuko yule Mniga wa An Officer and Gentlemen Louis Gossett na hata kuna kabinti moja wa American Pie nafikiri vile Shannon Elizabeti.

  Hawa jamaa watembea kwa Kenya kwa vijiji na porini waongelea Kenya. Jamani nasikia farijika twasifika namna hii.

  Najivuniaga Ukenya wangu ati tumetoa mbegu ambayo ndio yaja kuwa Raisi wa Marekani.

  Wale jamaa zangu wa Kiswahili mirefu kazi yao kuji-bosti tuu na yule myanki President wao anayecheka. Jamaa kaendaga kwa Bush kuliko safari zote za Moi na Kibaki together jamani. Lakini husikiagi wakisemwa sana kwenye mambo ingine.

  Hawa jamaa wabishi vile utafikiri wao ndio wanajua sana. Si ulionaga Wanjiru alipoimbiwa national anthem pale ameshinda Gold ya marathon?

  Waache wapande mori sisi tunajitangaza na sasa Rais wa Marekani ni damu yetu.

  Otholong'ongo na Mama Kayai wanapenda msalimia Mzee Kipara na Mzee Jongo.....

  2 damn hours of Dean Cain "eyes on Kenya" WaTz watalia chozi la pilipili na Kilimanjaro yao...


  Dean Cain: 'Eyes on Kenya' - CNN.com

  Eyes on Kenya - AOL Television
   
 2. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Put jokes aside, this is serious! How can Kenya continue to outsmart us on everything?

  Just imagine after all those 15 trips by Kikwete to US, we should have at least gain some popularity to get 10 one hour mini Series of Jambo: Hakuna Matata(or Ahsante sana smash Banana)!

  Sasa tumelundika matangazo kwenye teksi bubu pale London huku tunawaachia kina Ralitsa Vasilleva, Jonathan Mann au Christiane Amanpour wakitangaza mambo mengine na tusinunue 30 minutes pale CCN au hata kwenye Superbowl ya Marekani?

  That program was a huge publicity kwa Kenya, iwe ni watalii, wawekezaji, NGO au watu wenginewe.

  Nasubiri Membe na Mkuchika au ni Chiligati watoe majibu!
   
 3. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145

  Wao wanabaki kusema CCM ni safi ingawa ushahidi wa uchafu wanao na ndio maana mahakama imewabana kwa kuanzia.

  Its tempts people to suspect them IQ's
   
 4. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mshiiri,

  Kenya uchumi wao utakuwa unaongezeka kutokana na mapato ya Utalii na menginewe sisi tunasubiri misaada na wawekezaji!

  Sijui kama pale Utalii na Viwada na Biashara kuna watu wenye upeo wa kujua nini kifanyike tuweze kuwanza peta na kujitangaza.

  Ari, Kasi na Nguvu mpya inabidi iwe wabunifu na si kupigwa tobo kila siku!
   
 5. M

  Mpanda Merikebu Senior Member

  #5
  Dec 4, 2008
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 170
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Mchungaji,

  Naona umesahau msemo usemao "Msafiri Kafiri"! JK na posse wake wanaona ujiko kuwa karibu na kichaka. Lakini hawaangalii nje ya boksi. Hawajifunzi kwa wakenya, wahindi au hata hawa wazungu ya kuwa mtu anakuwa rafiki yako kwa sababu anatafuta kitu?
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Did you seriously expect anything from a country whose citizens are proud of their COCONUT TENDENCIES?
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  hivi ili uchumi wetu tuendelee kutegemea Utalii?

  surely you can do better than that
   
 8. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  GT,

  You know better than that kuwa Mchungaji hategemei Utalii pekee uwe kichocheo cha Uchumi.

  Imagine tukitangaza si mbuga tuu, bali hata ardhi tuliyonayo na jinsi ambavyo tunazalisha Pamba, Kahawa, Tumbaku(though this is a tough sell now), Korosho, Karafuu, Chai na uwezekano wa kulima maharage, mahindi, mpunga, mboga za majani na shughuli nyingine.

  Umesikia Wakenya wanatulaumu kuhusiana na EAC? unajua sababu ni nini? si kuwa hatuna rasilimali, bali ni "uvivu" wetu wa kufanya kazi kibunifu.

  Let say tunataka kuboresha kilimo, lakini hatuna uwezo wa kufanya mapinduzi hayo sawa sawa. Kwa nini basi tusitafute Wakulima wabia kutoka Korea kusini au nchi za ghuba ya Uajemi na jirani ambazo zina ardhi duni isiyo na rotuba au maji tosha na kuwakaribisha wawe wawkezaji kwa kukodi ardhi huku tukiweka masharti ya kutuletea mapinduzi ya kilimo kwa wakulima wetu na si kukubali kunyonywa kma tulivyofanya kwenye madini?

  China wanakodisha ardhi Kenya ili walime Soya na Mahindi, sehemu kubwa ya rasimlimali hii pia inawahusu Wakenya na kuwasaidia waweze kuwa na kilimo cha kisasa.

  China hawa haw, wameingia Congo na wana miradi mikubwa ya Kilimo, Madini na zaidi wanajenga barabara, reli, bwawa la maji, kurekebisha nishati na miundo mbinu.

  Sasa wenzetu wako creativ na uwekezaji, lakini sisi tunalaghaiwa na "all that you can eat buffet" na kusahau ku-negotiate vizuri uwekezaji wa maana.

  Hichi kipindi cha Eyes on Kenya, kilikuwa ni kuhusu jamii fulani na hasa waathirika wa HIV, watoto yatima na wengine. Lakini hakikuacha kuiuza Kenya kwa mengine ambayo ni ya maunfaa kwa Kenya.
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Dec 4, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,065
  Trophy Points: 280
  Rev.Kishoka,

  ..hivi hawa jirani zetu tumewakosea nini? kwanini wanakuwa na negative attituted kwa Tanzania kuliko nchi zote za EAC?

  ..nadhani mahusiano ya nchi hizi mbili yanahitaji msaada wa mshauri nasaha.
   
 10. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Kishoka, i actual watched this last night on my50 ,i even stop watching my favorite show private practice for Eyes on Kenya.It was nice watching it but i was so jealousy i wish kama ningekuwa naaangalia Tanzania for really.
  And it true kuna matangazo mengi sana kuhusu Tanzania in London,like 3 weeks ago i was in New york nikaona a tour basi with tangazo about Bugando University.Ila Kenya ipo so popular kiasi kwamba ukimueleza mtu unatokea tanzania wanakuwa so left out hawajui Tanzania and never heard ila ukisema tupo jirani na kenya utakuta mtu anakwambia ooh yeah..what can we do kufanya nchi yetu na sisi ijulikane world wide...ok yes raisi wetu anakuja sana marekani and stuff lakini labda hatangazi nchi ipasavyo...i don't know its my thought.
   
 11. Capitol Hill

  Capitol Hill JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2008
  Joined: Oct 19, 2007
  Messages: 733
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu..chance tulikuwana nayo pale watani wetu wa jadi walipokuwa wakipigana vita. Unajua ile ndio ingekuwa "competitive advantage yetu", na at the same time tuki promote aggressively hiyo notion, vile vile tungekuwa tunatakiwa tu boreshe Miundo mbinu yetu. Kiwanja chetu cha ndege cha kimataifa cha pale kaskazini (KIA), ambacho ndio port of entry kwa watalii wengi nchini ni cha hali ya chini mno. Despite kwamba hakina hadhi ya kuitwa international airport, kinaendeshwa bila ufanisi. Tumshukuru Mungu kwamba pamoja na matatizo ya kutokuwa na reliable umeme shirika kubwa la ndege la Uholanzi KLM wame stick na sisi..japokuwa kuna kipindi uzalendo uliwashinda kutokana na kukatika katika kwa umeme hali iliyowalazimisha kushusha abiria kwenye destination nyingine e.g Nairobi, and Dar es Salaam na kulazimika kuingia gharama ku compensate hotel expenses na usafiri kwa abiria waliotakiwa ku land Kilimanjaro.
  Halafu kuna suala la promotion lenyewe. Two weeks ago NBC News crew iliyoongozwa na Ann Curry walikuwa wanapanda Mt. Kilimanjaro. Niliangalia kwenye magazeti ya Tanzania, ili kuona kama kuna statement kutoka kwa msemaji wa Wizara ya Utalii ama Waziri wa Utalii. Hizi segments za kupanda Mt. Kili zilikuwa zina air kila asubuhi kwenye TODAY show ambayo ni one of the top rated morning news hapa U.S. kwa siku nne mfululizo. Mungu atupe nini tena? Kuna namna unaweza kufanya vitu kupata free publicity. Vitu vingine vya ki binadamu tu. Hivi hata mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro alishindwa kuwakaribisha hawa watu kwa kikombe cha chai kwenye ikulu ndogo, ili kuonyesha ukarimu tulio nao watanzania? Na kama hawa watu "high profile" wamekuja Tanzania na Wizara ya Utalii" hawajui, kosa ni la nani? Ubalozi wetu pale DC unafanya kazi gani?
   
 12. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
 13. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #13
  Dec 5, 2008
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Kenya ni Nchi masikini kama Tanzania tu na watu hapa mnaongea Kenya kama vile inafanya vizuri na ukweli si hivyo. Tanzania inajulikana kuliko zamani na raisi kusafiri si makosa kama analeta wawekezaji na miradi nyumbani.
   
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Dec 5, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280

  Good Question!!

  Kenya inapakana na nchi za Somalia, Ethiopia, Sudan, Uganda na Tanzania. Hawajaongelea kuungana na Sudan, au Ethiopia au Somalia; kelele zote ni kutaka kuungana na Tanzania kwa nini?

  Hebu angalia jinsi inavyoishai na majirani zake wengine. Hali ya amani huko Somalia siyo nzuri wala Kenya haijawahi kuchukua initiative yoyote kusaidia kuleta amani kule. Hali kusini mwa Sudan siyo nzuri wala Kenya haijawahi kuchukua initiative yoyote kusaidia kutuliza hali kule. Uhusiano wa Ethiopia na majirani zao Eritrea ni mbovu sana, wala Kenya haijafanya lolote kuwapatanisha majirani zao.

  Wakati kulipokuwa na machafuko kule Rwanda na Burundi, Tanzania ilikuwa msitari wa mbele kuwasuruhisha hadi wamefikia hali nzuri leo hii kiasi cha kenya kutamani wawe kwenye shirikisho. Mwalimu Nyerere alisimamia zoezi la amani pale Rwanda na Burundi lhadi alipotangulia mbele ya haki. Wakati Musumbiji ilipokuwa inakaliwa na wareno, Tanzania tulisimama kidete kutatua tatizo hilo hadi pale Flerimo iliposhinda. Mgogoro wa Malawi tuliusimamia kupata suluhisho. Hata Kongo tumejishughulisha kuweka amani, juzi juzi tulikuwa kwa majirani zetu Komoro kusaidia kuweka amani. Tumejitahidi kujenga mazingira mazuri kwetu kwa kuhakikisha kuwa majirani zetu wanaishi kwa amani. Hata walipokuwa wanachinjana wenyewe kwa wenyewe, bado tulimpeleka FISADI wetu awasaidie kurudisha amani na mwishoni ni rais wetu aliyewasimamia kukubaliana kurudisha amanai kwao.

  Kenya wanaangalia upande mmoja tu, palipo na amani ambapo wanaweza kuvuna haraka haraka. Kama kweli wanaona kuwa kuungana ni kuzuri, basi waanze na majirani zao walioko pale kaskazini wakati sisi tunaanzia kusini halafu tuje tukatane katikati.
   
 15. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2008
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  N they want us to federate with them!!These guys are not smart than us it just that history imewabeba kidogo.
  But we r all poor!!
   
 16. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #16
  Dec 5, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Trip za Kikwete zimekuwa ni za kupoteza muda na raslimali tu. Ili kuitangaza nchi, ni vizuri Kikwete pamoja na Membe watumie njia ambazo ni effective kuliko wao wenyewe kuwa watembeaji tu. Mtu kama Kikwete anapokuwaja hapa marekani hakuna hata jirani yangu anayefahamu kuwa Kikwete yupo hapa na ametokea Tanzan; wanaofahamu hivyo wale wanasiasa wa Washington DC ambao tayari wanaijua Tanzania, kwa hiyo trip inakuwa haikusaidia lolote. Baadhi ya njia ambazo ni effective ni kama vile:

  (a) Kuwakaribisha viongozi maarufu wa nchi za nje na wale controversial kuitembelea Tanzania. Angalia jinsi ziara ya Bush na mke wake ilivyofanya Tanzania ijulikane hapa Marekani. Daktari wa familia yangu alikwenda Tanzania na kukaa kule Arusha kwa wiki mbili kutokana na taarifa alizopata kuhusu Tanzania kufuatia ziara ya Bush, na sasa hivi amekuwa mgonjwa kabisa anataka aende tena mwakani na wakwe zake wote.

  (b)Kuna wakati tulitembelewa na akina Beyonce na mumewe pamoja na mwanamuziki mwingine wa kimarekani sikumbuki jina lake; kwa bahati mbaya sana viongozi wetu hawakutumia hiyo opportunity kuwakarimu na kuwafanya wajisikie - hilo lilikuwa ni kosa. Kuwakarimu watu hao na kuwafanya wapende kuwepo Tanzania kwa mambo kama kuwakaribisha kwenye dinner na viongozi wazito wa serikali au kuwapa ulinzi wa ziada kutumia askari wetu japo kwa geresha na vitu kama hivyo vinasaidia kuwapa moyo kuwa nchi hii ni nzuri, na hivyo kuitangaza vizuri warudipo kwao.

  (c) Serikali ijitahidi kuwa inavutia mikutano mbalimbali na michezo ya kimataifa kufanyikia Tanzania, na inapotokea hivyo, serikali iweke utaratibu wa kuwakarimu wajumbe na wanamichezo wale kwa namna moja ama nyingine kusudi waendelee kuikumbuka Tanzania baada ya kurudi makwao.

  (d) Serikali iangalie tena swala la uraia wa nchi mbili kwa vile hiyo nayo itapromote sana nchi kujulikana. Hebu fikiria kama Rev. Kishoka amekuwa Seneta wa marekani lakini bado ni raia wa Tanzania kama ambavyo Schwarznegger na uraia wa Austria. Na tuwe wakweli kuwa kujulikana kwa Kenya duniani kumepanda sana siku za hivi karibuni pia kwa ajili ya Rais Obama.

  (e) Wasanii wetu waendapo ziara huko nje, serikali iwalipe na kuwapa jukumu la kuitangazan nchi kwa kutumia vitu kama flyers na posters na vitu kama hivyo.
   
 17. M

  Mutu JF-Expert Member

  #17
  Dec 5, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  Ni nzuri tu hiyo docomentary.

  Ila Rev. Kishoka kama unavyosema tunatakiwa kuweka kama hii kitu ktk vituo vya maana.Ingawa siku moja niliona tangazo la utalii Bongo hapa New York ila lilipita kama kishada just one second.
  Kweli kuna umuhimu wa kujitangaza zaidi.
   
 18. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #18
  Dec 5, 2008
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Kumbe Rev Kishoka uliona hio kitu?..Nilidhani ni mie tu lakini naona
  ilikua beamed kila mahali.

  Jamani inabidi tukubali Wakenya wamezidi wabongo when it comes to advertising
  their rasilmali.Kama alivyosema CapitolHill, chance poa ya Bongo kujimarket ilikua
  ule wakati wa fujo la Kenya baada ya zile kura.Someone should have been promoting
  Dar as an alternative location..lakini najua wakuu pale boardi walikua wamelala tu.

  Hio documentary niliangalia kwa umakini na kwa upande wangu ilinipa idea
  kibao za kuanzisha miradi hapo Bongo.Hao kina Lou Gosset na kundi lake si
  eti walikuja Kenya at random bali wamekua wakimfuatilia yule dingi wa ABC
  homes ambaye anachukua yatima na kuwalisha na kuwasomesha.Huyu bwana
  hata humu marekani ana-informercial zake za ku-raise hela and you saw how
  he came out in the documentary akishirikiana nao kuwalisha wale vijana.

  Sasa hebu jiulize, Bongo kuna mtu anashughulikia yatima na other disadvantaged
  people kama hapati mtaji?Humble projects like these can go a long way in shining
  the light on Tanzania.Ile shule ya yatima ilikua bomu ksihenzi lakini jamaa wametoa
  hela yao na construction imeanza in earnest and the project itakua completed
  sometime next year.Kwa hivyo jamaa wa mitaani wamepata kazi ya kukoroga zege
  na kujipatia posho for a while. Kisha najua huu ndo mwanzo tu and they will coming
  back to monitor progress in the school...thus links have been established for a now
  and times to come.

  Pia kuna swala la utashi wakisiasa kwenye haya maswala.Je serikali inaipa
  kipa umbele sekta ya utalii?...ama cha mno kwao ni kufuja madini ya wabongo
  na kuwaacha watu kama hawanachao? JK anapiga tripu kibao unyamwezini
  lakini je kile kikundi kinachoandamana naye, are they thinking about marketing
  the country ama wapo katika msafara ili kusuka dili zao binafsi za biashara?
  Mawazo ya Kichuguu on this subject nimeyaona poa sana and I hope somebody is
  reading na kuwa-forwadia wahusika.

  Bongo can do better.Yes We can!
   
 19. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #19
  Dec 5, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Tatizo la nchi yetu tunapenda mambo mazuri lakini bado tunafikiria kijamaa....kama serikali iko serious na kutaka kuitangaza nchi watoe tenda na fungu la kueleweka nchi itatangazwa vizuri tu.
   
 20. Dar_Millionaire

  Dar_Millionaire JF-Expert Member

  #20
  Dec 5, 2008
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  I don't see anything so special about Kenya being featured on CNN. Tanzania has had it's moments as well. We have run an ad, Bush was here, Clinton was here too, plus everyone now knows where Kilimanjaro is.

  Unless we still have tourists who do not use the internet in planning their trips then it's almost impossible to miss out on the true location of Kilimanjaro. If there's a website out there that says Kili is in Kenya someone bring it up and I'll have dealt with in no time.

  There's no reason to fill bad or low just because Kenya is on CNN. That's called competition. No one is going to monopolize CNN.
   
Loading...