External hdd imecrush

Kwetunikwetu

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
1,535
410
Waungwana naomba msaada wa kiufundi. Nina external hdd ya laptop ilianguka na nilipojaribu ku-connect tena ikagoma ila nikaisikia inagonga. Nilipoifungua ndani nikakuta iko ok haina physical damage. Sasa nilipo-connect tena stilll haitambuliki. Naomba msaada wa mawazo please nifanyeje manake i have a lot inside!
 
You may try removing the HDD from the enclosure and plug it onto another external hdd enclosure.

Kwa kusema "inagonga" una maanisha kuna sauti inatoka isiyo ya kawaida?



.
 
Waungwana naomba msaada wa kiufundi. Nina external hdd ya laptop ilianguka na nilipojaribu ku-connect tena ikagoma ila nikaisikia inagonga. Nilipoifungua ndani nikakuta iko ok haina physical damage. Sasa nilipo-connect tena stilll haitambuliki. Naomba msaada wa mawazo please nifanyeje manake i have a lot inside!

POLE SANA NDUGU!!

Kwa maelezo uliyotoa mpaka hapo... hiyo ndiyo imetoka, unless unafanya kazi kwenye maabara za uchunguzi wa HDD maana huko ndiyo wanavifaa vya kuweza kusoma open individual hdd platters. Kuifungua katika mazingira ya kienyeji ni KUIHARIBU!!

Physical damage kwenye cylinder hdd ni vigumu au haiwezekani kabisa kutengenezeka/kurekebishika kwa ufundi mdogo wa kinyumbani-nyumbani, ni kwenye maabara maalum ndiko wanakoweza ku-retrieve data. Platters za hdd ambapo data ndiyo huandikwa huwa ziko sealed ndani ya airtight container. Header inayosoma bits kwenye hdd wala huwa haigusi platter wakati ina spin, kwa ku-create vacuum hivyo kuelea juu juu.

Hivyo mkuu, nimekupa pole kwa wino mwekundu kwa mantiki kuwa hiyo ndiyo imetoka. Natumaini umenielewa hapo.

Anyway, unaweza kuitunza tu... huwezi jua mambo haya ya teknolojia yanavyokimbia kwa mwendo kasi... huchelewi kusikia miezi kadhaa ijayo wametangaza rescue tools za hdd zilizoharibika katika mazingira hayo.

Kwa maoni yangu ni kuwa, option ya kuwa nayo siku hizi kama backup tool kwa mambo ya haraka haraka ni USB thumb drive. Hizi zimepungua bei siku hizi, ukubwa nao umeongezeka sana tu... kuna 8GB, 16GB na 32GB.... na nina imani 64GB iko njiani soon. Zina dunda vizuri na hazina matatizo mengi. Kama mahitaji ya back up yako si ya mambo ya mafile makubwa makubwa ya video... basi hizi USB thumb drive zinafaa sana.

Kingine ni kwamba, siku hizi kuna SSHDD/SSDD (solid state harddiskdrive/solid state disk drive). Hizi ni teknolojia mpya, zina speed kubwa zaidi kuliko zile traditional, zina uimara zaidi kwenye physical impact, ila bei yake ndiyo iko juu sana. Lakini kama gharama si tatizo, basi unaweza kuzimendea hizi kama unautegemezi mkubwa wa external hdd.

Naishia hapa.
Pole, i hope unaweza kuta ulikuwa na back up ya yale uliyo save kule ndani pahala pengine.

SteveD.


 
SteveD nashukuru kwa maelezo ya kina mkuu, manake nilijaribu kuwauliza mafundi kadhaa nao wamenipa majibu kama yako pia. Thanks
 
Back
Top Bottom