Exposure ndogo ya 'waimbaji' wetu TZ

Brooklyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
1,459
284
Wadau katika pitapita yangu mtandaoni nimekutana na picha kadhaa za 'waimbaji' (sidhani kama ni wanamuziki) wa kibongo wakiwa wamepiga picha na Mh. Rais Ikulu Jijini DSM hivi karibuni.

Nashangazwa na mavazi (hasa suruali) walizovaa waimbaji hawa, naamini hayakushahili kuvaliwa mahali kama Ikulu. Nakumbuka katika baadhi ya ofisi za serikalini kuna mwongozo wa mavazi hata kwa wageni wanaoingia sehemu hizo. Licha ya hivyo hata hawa waimbaji si walijua wanaenda kukutana na Mh. Rais Ikulu, kwa nini wasivae 'formal zaidi'? Najua hizo Tshirt za 'zinduka' walivalia palepale Ikulu.

Nimekuwa nikiona wasanii wenzetu wa nje wakialikwa Ikulu za kwao wanainda wakiwa wamevalia 'decent' zaidi.

Hapa kwetu inakuaje??? Ama ni sawa hata ukiingia na 'pensi nyanya'?

zinduka+3.jpg

zinduka+2.jpg


zinduka+2.jpg


zinduka+6.jpg




Jana Jumatano tulikuwa Ikulu na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwaajili ya kupiga picha kwaajili ya campaign maalum za kutokomeza Malaria Tanzania



Source: http://www.ladyjaydee.blogspot.com/
 
Hivi exposure maana yake ni kuiga vitu vya watu ikiwa ni pamoja na mavazi? hivi ile timu ya IvorY Coast sijui ya akia Lydiah Ogoba walienda na masuti?????

Mmmh ila nasikia maana ya MSANII NI KIOO cha jamii ni kuwa ukimuona msanii muonekano wake na tabia zake basi ujue hata hiyo jamii inayomzunguka au anayoiwakilisha ndivyo ilivyo. SO TIA AKILI
tehee namkumbuka KANUMBA na BBA
 
Mie sielewi kabisa kitu kabisa ,mie naona hao jamaa wamevaa vizuri tena very smart wamechomea hadi jeans zao na wamependeza kweli kweli.
Sijui walitakiwa wavae nini?
Hivi siku nyingine Raisi anavaaga jaeans alafu anaenda sijui shamba au sijui kuzindua nini sijui......si anatokea Ikulu,sasa ulitaka hao nao wavaaje.....?
Hata Obama anapiga Jeans kama kawaida muda mwingine.kama ingekua vingivyo WABOLONGAJI wa IKULU wange-issue dress code kwa ajiri ya mchakato mzima
 
Mbona sioni tatizo, nguo za kawaida tu. ulitaka watinge na suti? kumbuka they merely artists. JK mwenyewe alikuwa casual...so whats the problem.
 
We unataka kila mtu avae kama PeDeJee Papa Mutozi mkanda kitovuni?

Ushaambiwa wasanii hao, kwani umesikia mawaziri wanataka kuapishwa hao? Kwani Ikulu mbinguni? Kwani unawasaidia kununua nguo? Vipi wengine wakikwambia hizo nguo unazosema hata hawana, na hizo jeans wameazima kwa kumpa heshima rais lakini kwa kawaida huwa wanavaa ile mijeans iliyochanika chanika?
 
labda walitakiwa wavae suti.. banana kajikaba hiyo shingo
ila wamependeza ingawa mdau unasema hizi nguo ni za kupandia stejini
 
Back
Top Bottom