Experience yangu ya ukiranja wa nidhamu

Gojaga Nize

JF-Expert Member
Jul 1, 2015
2,756
1,732
1. Kiongozi ni "msimamia maono tu" ya wale anaowangoza

2. Kiongozi lazima awe na sifa ya kusikiliza mawazo ya kila anayemuongoza

3. Kiongozi lazima achambue hoja za wale anaowaongoza bila kuwakwaza kwa kufanya vizuri zaidi yale waliyoyawasilisha kwake na kujibu yaliyoshindikana kwa hoja za msingi.

4. Kiongozi hana dharau wala kejeli lazima amuheshimu kila mtu. Mdogo na mkubwa, masikini na tajiri, mlemavu na asiyrmlemavu.

5. Kiongozi lazima asimamie sheria zilizomuweka pale anapoongoza kuhakikisha kila mtu anapata haki yake..

6. Kiongozi lazima awe na dira akijua kabla hajamaliza shule kuna kiranja mwingine atakuja ushika kijiti hivyo lazima afanye vizuri.

7. Kiongozi lazima ajue kuongoza ni kipawa ambacho mtu anacho. Ndio maana kila mtu sio kiongozi. Kiongozi anayetambua kuwa kuongoza ni kipawa lazima atazingatia sifa tajwa hapo juu.

8. Kiongozi ni mvumilivu, mwenye kiasi, mtu mwema, hajivuni, hahesabu mabaya, anayefadhili, hapendelei, hana kisasi, anajiheshimu na anaupendo wa dhati kwa kila mtu anayemuongoza.

9. Kiongozi hana sifa ya kujiona yeye anaakili kuzidi darasa zima. Ndio maana unakuta mara nyingi kiranja sio namba moja darasani, moja anashika mwingine ila yeye ni kiongozi tu na anaweza akawa wa 30.

Mwisho: Naomba muniombee nifanye vizuri mtihani wangu wa form four "ya miaka miwili"

Shukurani: Kwa mwalimu wa nidhamu kunifanya niyajue haya machache:
 
Back
Top Bottom