Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,655
- 729,714
Unaweza ukadhani kwakuwa ni neno la kizungu basi likawa na maana nyingine tofauti lakini kiasili exortism ni neno la kigiriki lenye maana ya kujihinikiza na kiapo (binding by oath) ambapo unakuta unaposoma kwa undani utakuta ni kupunga mapepo kwa njia ya kidini hasa kikristo na chimbuko likiwa ni Vatican.
Kupunga mapepo ni tofauti kabisa na kutoa majini na mapepo kwa waganga wa kienyeji/jadi, na tofauti yake kubwa ni kwamba hakuna tunguli mizimu wala madawa bali hutegemea nguvu ya Mungu.
Kiasili ndio hivyo lakini katika kipindi cha miaka 50 hivi hili zoezi limekuwa maarufu sana duniani hasa ulaya na marekani ambapo hata vyuo Kwa mfano cha Texas vinafundisha exorcism na hii yote inatokana na ongezeko la wateja.
Exorcism inatumiwa sana na hawa wanaojiita mitume na manabii walionea kila kona ya dunia, huku wakiwa wamechanganya na mambo yao mengine na kujifanya ni nguvu ya kimungu
Kimsingi na kiuhalisia kuna asilimia ndogo sana duniani ya watu wanaosumbuliwa na mapepo lakini wengine woote waliobaki ni kwasababu ya msongo wa mawazo, vurugu za kimaono, changamoto za kimaisha na kuumizwa kihisia kulikovuka mipaka ya kiwango cha uvumilivu wa binadamu.
Exorcism ni tofauti na uponyaji wa Kristo Yesu, yeye hakutumia nguvu wala sauti kali bali alitamka na ikawa, hawa ndugu zetu wa kileo wamechukua nafasi ya kupunga mapepo kazi ya waganga wa jadi na kujifanya ni nguvu ya uponyaji ya kimungu
Exorcism ina mengi, na katika baadhi ya matukio watu kwenye mchakato wa kutolewa mapepo walipigwa hadi kufa.... Kwahiyo ndugu zangu unapoona ndugu yako ana dalili za kuchanganyikiwa au kuwehuka usikimbilie kwenye kudhani kuwa katupiwa mapepo utaongeza tatizo badala ya kutibu...
Maisha ya siku hizi Yana changamoto nyingi inahitaji muda kuchunguza tatizo lililofichika kabla ya kufikia uamuzi wowote, watu wanateseka na wengine hutumia mwanya huo kupiga dili..
cc: @black sniper

Last edited: