Exlusive:MV Spice Islander: Zanzibar Tuitakayo;Uzembe unapogeuzwa Mtaji ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Exlusive:MV Spice Islander: Zanzibar Tuitakayo;Uzembe unapogeuzwa Mtaji !

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bikra, Sep 16, 2011.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Sep 16, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tarehe 10 ya mwezi Septemba, siku moja tu kabla ya Kumbukumbu ya Septemba 11, siku ambayo dunia nzima inakumbuka maadhimisho ya miaka 10 ya Septemba 11, Zanzibar ilipata Maafa ya kihistoria.
  Jina langu ni SABRY, muathirika wa maafa ya kusikitisha ya MV Spice katika visiwa vya Zanzibar ambayo siku ya tarehe 9 Ijumaa ambapo meli hii, kwa kweli si meli ni Ferry tu ambayo imesajiliwa kubeba mizigo kutoka Zanzibar tu kwa sababu ya Usajili wake wa kazi katika Dare salaam, Tanzania ilikuwa imezuliwa na SUMATRA, Mamlaka ambayo inasimamia Usafiri wa Nchi Kavu na baharini Tanzania Bara kwa Sababu ya Hali Yake ya Usalam ana Kiufundi.


  Nini kilichotokea. . . .?
  "Baada ya kuadhimisha kumalizika kwa Mwezi wa Ramadhani, Nilikuwa na ndoto mbaya juu ya familia yangu, na kwa sababu mke Wangu alipanga kusafiri, nilikuwa na wasiwasi sana kuhusu safari hii." Alisema Sabry.


  Ni Utamaduni hapa Zanzibar kwamba, wakati familia inafunga ndoa ni lazima wanafamilia wote wa Familia wahudhurie na kutoa baraka kwa Bwana Harusi na bibi Harusi na kuwaaga. Kwa sababu ya mila hii nilitoa ruhusa kwa mke wangu kuhudhuria sherehe huko Matuuni Pemba, Kisiwa Cha Pili cha Zanzibar akiwa na Wifi Yake, Amina Mmanga na mtoto wake Mariam.

  Nilifanya Maandalizi yote kwa ajili ya safari hii ikiwa ni pamoja na kuandamana naye mpaka Bandarini lakini sikuweza kupata fursa ya kumpeleka hadi ndani kwa sababu hali ilikuwa mbaya kwani eneo la bandari kulikua na wasafiri wapatao 3,000 ambao wote wanataka kupanda ndani ya Meli hio. Nilimkabidhi mke wangu kwa Kaka yake ili amsaidie apande Ndani ya Boti, Sikujua kumbe Niliyakabidhi Maisha yake kwa Mungu.

  Safari Iipoaanza . . . .
  Meli ilianza Safari yake kutoka Dare salaam, siku ya Ijumaa tarehe 9 Lakini Ripoti zisizothibitishwa zinasema kuwa, meli ilikuwa imebeba mizigo na abiria zaidi ya uwezo wake na hii iliwafanya SUMATRA kuingilia kati na kuidhuia meli mpaka baadhi ya Mizigo iliposhushwa. Mabaharia Walishusha baadhi ya mizigo hadi SUMATRA waalipokubaliana na Hali hio na Kuruhusu Meli kuondoka.


  MV Spice iliwasili Kisiwani Zanzibar siku hio hio jioni na abiria wapatao 300 (watoto wachanga na Wanaoingia bila ya Tiketi hawajahesabiwa) na ukadiriaji wa Abiria zaidi ya 100 ambawo hawakuwa katika Orodha ya meli. Moja ya tatu tu ya wasafiri kutoka Dare salaam walimaliza safari yao katika Bandari ya Zanzibar na inakadiriwa watu kati ya 200-250 walibaki ndani na Meli kwa Safari inayofuatiya, Safari ya Pemba.

  Safari ya Pemba Ikaanza.
  MV Spice ilikuwa tayari na Wasafiri 350 na mizigo ambayo ni pamoja na chuma, Ngano, Mchele, Saruji na magari, inakadiriwa Mzigo tu ulikua Tani 500!.


  Usalama wala Meli mara nyingi unaweza kuathiriwa na hali ya hewa mbaya , Bahari Chafu, Kugongana na Chombo chengine au miamba. Aidha, kanuni za Bahari zinataka Nahodha na Baharia kulinda usalama wa Abiria wao ikiwemo kufuata kanuni zote za usafiri wa Baharini kama Kujaza kwa Idadi na Kuwa na Makoti ya Kuogelea kutokana na Namba ya abiria waliochukua ama zaidi.

  Katika Mamlaka ya Bandari Zanzibar Meli iliruhusiwa kubeba watu 610 ambao walikua Wasafiri Wapya kwa mujibu wa Orodha ya meli ikiwa ni pamoja na watoto zaidi ya 400 ambawo hawakuonyeshwa katika Orodha ya Meli sababu waliruhusiwa kupanda meli bila tiketi. Tunasema zaidi ya watoto 400 kwa sababu ni Mila na Silka hapa Zanzibar kwa watoto kusafiri na kwenda kula Sikukuu ya Eid na Familia zao maana Shule pia huwa zimefungwa kwa Kipindi kirefu. Pia kuna idadi ya Abiria wengi ambao hawakukata Tiketi walipigwa Mihuri Mikononi na Idadi yao haijulikani.

  Hivyo jumla ya idadi ya wasafiri waliopanda Boti hii Inakadiriwa kuwa kati ya 1500 – 2500.

  Wakati wa kuondoka Bandarini Zanzibar kuna baadhi ya Abiria wametoa Ushuhuda kua walipoona Meli imejaa sana walishuka na Jamaa zao lakini Mabaharia walipoona hivyo kwa tamaa ya Biashara waliwazuia wasitoke wengine wanasema waliwazuia wasitoke maana ingeanzisha vurugu na Meli ilikua imeshaanza kuyumba wakati bado ipo Bandarini! .Pia walipoanza kuiondoa Meli ilianza kuyumba na wakaamua kuirudisha tena Bandarini na Kuitazama Tatizo Kisha walipoona haiyumbi tena, Haoooo wakaanza Safari ya Pemba.Kawaida inachukua masaa Nane Mpaka Kumi Kufika Pemba.Kuna Ripoti zisizothibitishwa kua hata Mmiliki wa Meli aliaambiwa kuhusu hatari kama Nahodha angeondoa Meli, ila baada ya kushauriana na Wenzako Wakasema, "Haya Ombeni Mungu" na Safari ikaanza,Kilisema Chanzo hiki cha Habari.


  Haya, Na Safari ya Pemba Ikaanza . . . . . .

  "Ilikuwa karibu na usiku wa manane wakati nilipopokea simu kutoka kwa Shemegi Yangu, Dada wa Mke wangu Akisema,Sabri Jikaze Kaka angu, kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba MV Spice Islander inazama! Hamadi ! Nilishtuka sana na Taarifa hizi na kutokana na Hali ya Wasiwasi niliyokua nayo kabla mke wangu hajasafiri niliziamini Taarifa hizi na Kuanza Kumuombea Mke wangu "! Alisema Sabry


  Sabry akaendelea, Nilikuja Kujua Baadae kuwa Mke wangu alimpigia Simu Dada ake na Kumwambia " Mpaka sasa Meli inazama na Dada tusameheane, Mwambie Shemegi Yako tusameheane na muniombee dua mi natangulia nawasubiri Akhera . . . . Simu ikakatika dalii za Kuishiwa Chaji." Alimazia Sabry

  Mamlaka za Zanzibar zina Nini la kusemaaaaa ... ..
  Mpaka sasa Ripoti za Serikali ya Zanzibar zinasema Abiria waliosajiliwa na meli hio ni 610 Lakini cha Kujiuliza, Ni hao hao waliotangaza watu waliookolewa ni 619 na Maiti zilizopatikana ni 202, Je, Wanajua Hesabu vizuri hawa!


  Baada ya Juhudi binafsi ya Wabunge, Hadi sasa watu wafuatao hawajulikani Walipo, Kojani (108) Ole (157) Micheweni (88) Magogoni (184) Wete (149) Gando (418) Mtambwe (214) na Konde (96)Jumla watu ambao inaaminika waliku katika meli hii na hawajapatikana ni 1,596,Sasa tukijumlisha na Maiti (202) na waliookolewa (619) Jumla ya watu waliokuemo ni (2,214) Kwenye Meli iliyosajiliwa Kuchukua Mizigo na abiria wachache.

  Kwenye mahojiano rasmi na Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC), Muheshimiwa Hamad Masoud (Engineer) Waziri wa Usafiri Zanzibar alisema kuwa, kati ya sababu ya ajali hii ni kwamba Wazanzibari wana mila ya kusafiri kwa makundi na Kifamilia, watoto wengi, na wanaweza kupanda melini hata kama itajaa vipi, Alisisitiza kuwa Serikali ina sehemu yake ya kuhakikisha Ajali kama hii kamwe haitokei tena.
  Sasa Mamlaka zitujibu Masuala yafuatayo

  1. Mara nyingi Mamlaka za Zanzibar zimeweza Kuzuia Mandamano ya Kupinga Serikali, Wanafunzi au Mikusanyiko ya Dini, Imeshindwaje kuzuia Meli hii isiondoke, Au Walikua washalala?

  2. Muda Mfupi uliopiopita kuna Ajali ya meli iliwahi kutokea ya MV Fatihi ambayo kwa Uzembe ilizama Wakati imeshafika Bandarini ikitokea Daresalaam, Japo kuna watu waliwahi Kushuka lakini Baadhi hawakuwahi na kufa Maji.Tume ikaundwa na Jambo Moja ililoligundua ni kwamba Meli zinapakia sana Mizigo na Watu, Mbovu sana na hazina Vifaa vya kutosha wakati wa dharura na Serikali ikawahakikishia wananchi kua Ajali kama hii haitoweza kutokea tena, Baada ya Ajali hii, Je Serikali inasemaje?


  3.Kabla Meli haijaanza safari Maafisa wa Bandari, kabla hawajairuhusu meli kuondoka ni wajibu wao kuangalia utabiri wa hali ya hewa; kama kuna Maboya ya kutosha katika kila kiti na sehemu za wazi hasa za Milangoni za Meli , Mstari wa kuonesha Alama ya Kuelea kwa Meli upo katika kipimo Sahihi kuonesha kua hakuna dalili ya uzito ulipotiliza.Je haya yote yalizingwatiwa?

  Baadhi ya Ripoti zinasema, Bado Kuna maiti wengi kwenye Melii hii Ambayo imezama Takribani Mita 350 Chini ya Bahari kiasi ya kufanya Mabingwa wa kijeshi wa Kuzamia kutoka Afrika kusini kushindwa kuifikia maana Vyombo vyao vya kisasa vinawawezesha kuzama Mita 50 tu chini ya Bahari.Kama wazungu wameshindwa wataweza Wabongo!


  Mengi yanasemwa na yatasemwa kua, Kama hamu yao ilikua ni Kutengeneza TITANIC ya ZANZIBAR, Wamefanikiwa.Na wajiandae kwenda HOLLYWOOD Kuchukua Mshindi wa Filamu za Baharini.

  Ushuhuda

  "Nilikuwa katika MV Spice Islander na tulipofika Nungwi meli ilipasuka na kuanza kuingiza Maji Upande Mmoja, Mabahari walitunadia kuelekea Upande wa Pili ambao nao ulikati na Maji yakaanza Kuingia.Taharuki ikaanza na Mabaharia Wakatangaza Hali ya Hatari kila mtu ajiokoe,tukatupiwa magodoro Mapya Baharini na wengine wakavaa makoti ya kuogolea na tukapiga Mbizi (Tukajitupa Baharini) "alisema mmoja wa wasafiri

  "Niliona idadi ya maiti wengi pwani ya Nungwi" Kilisema Chanzo chengine cha Habari.


  "Hakika sote tumeeumbwa na Mungu, Na Hakika sote kwake tutarejea, Utake Usitake"Alimaliza Sabry kwa Majonzi

  Kwa Mawasiliano: zanzibaraccident@gmail.com
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  so sad inabidi tuamke sasa kudai uwajibikaji kwa viongozi wazembe, HIVI mkuu wa kaya alikwenda kufanya nn zanzibar kama alihuzunika kwa nn alishindwa kuchukUA maamuzi magumu ya kuwafukuza wote waliohusika na uzembe huu akianzia na mawaziri wake,SHEIN nae hajamtimua mtu hadi leo hivi serikali inacheka cheka tu,
  nadhani sumu ya ujamaa isipoisha tutabakI kuwa wajinga siku zote, INGEKUWA nchi kama kenya au RWANDA kwa kagame watu wengi wangeshwajibishwa tayari hata mmiliki wa meli yenyewe wanamficha ni ujinga, WAIGE mfanO wa waziri mkuu wa japan aliejiuzulu kutokana na janga la tsunami. mm sio mwanasiasa lakini nasema TANZANIA itakuwa maskini na tutakufa wengi kwa uzembe kama serikali hii ya CCM isiojali watu itazidi kukaa madarakani.tumevuna nini kwa miaka 50????? TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA KABISA.
   
 3. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hakika ushuhuda huu umenitoa machozi.Mungu awarehemu waathirika.Nafuatilia kwa makini suala hili maana nimekaa Pemba na najua matatizo ya usafiri huko,hasa kwa masikini.Bado nasisotiza kuwa kama si siasa na kutojali watu wale masini wasingepoteza maisha.
   
 4. l

  lasix JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  dah poleni sana waathirika wote wa ajali hii,kila nikiwafikiria naumia mno moyoni hasa kwa ambao hawajapatikana,sijui viongozi watatuambia nn naona wataikaushia tu, nchi hii haina uongozi imara,watu wanacheza na maisha ya wenzao.
   
 5. j

  junior05 Senior Member

  #5
  Sep 17, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hakika ni habari ya kusikitisha sana,vyombo husika vya bandari na hata baadhi ya wahusika wa serikali hakika wajiwajibishe, msafiri yeyote anahitaji kufika aendako,awe amekata tiketi au wahudumu wachukue pesa kumsaidia ila yeye anataka kufika, ni jukumu la mamlaka husika kuhakikisha safety first,how come watu wateketee hvi then wahusika wajikaushe,haki ya mtu haipotei and may we remember ignorance is not a defence.
   
 6. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2011
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 670
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80
  Hii simulizi inatia huzuni sana! Nitashangaa kwa kweli kama hili jambo litapita bila ya mtu kuwajibishwa. Inasikitisha kama kweli sheria zipo na hazifuatwi!!! Wahusika wote lazima wawajibishwe! Wakati fulani natamani tupate kiongozi kama HITLER au WACHINA labda mambo kama haya yatanyooka na watu watakuwa na discipline ktk maeneo yao ya kazi.
   
 7. l

  lasix JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  ivi hata wakileta hilo nyambizi toka SA wataweza kuwapata hao maiti wote kweli?maana watakua washadecompose na kuishilia baharini.maskini ndugu zetu,mungu awarehemu huko mliko.
   
 8. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Dini ni kitu cha ajabu sana, mtu anasema anarejea kwa Mungu lakini anaenda huku analia. Si unaenda ahera, majonzi ya nini? Watanzania, tu deal na vyanzo vya ajali, "Mungu amerejesha, Mungu aliumba" ni upupu, ndio maana tutaendelea kufa kizembe.
   
 9. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  Mkuu wewe wa dini gani? Kama hufuati dini yoyote basi sitokushangaa. Waislam tunasema INALILAHI WAINAILAIHI RAJIUUN. Sisi ni viumbe wake na kwake tutarejea.
   
 10. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kama kweli umefiwa na mkeo,Pole.
  Pamoja na hivyo habari yako imejaa majungu na habari za kusikia na pia takwimu zake za kubabaisha.Isitoshe huo utamaduni wa kufunga ndoa na kuagana ni wa ndoto yako uliyoiota tu.Wacha tukasome kwengine kuhusu hili janga.
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  walivyo myopic, wao wanaangalia voda kuliko walipoangukia
   
Loading...