EXIM yatoa mkono wa pole kwa waliopoteza mali Sido | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

EXIM yatoa mkono wa pole kwa waliopoteza mali Sido

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sumasuma, Feb 10, 2012.

 1. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mwandishi Wetu, Mbeya
  BENKI ya Exim Tawi la jijini Mbeya, imetoa Sh13.3 milioni kwa wafanyabiashara wanawake 267 wa Soko la Sido lililotekea kwa moto mwishoni mwaka mwaka jana.

  Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi hundi ya fedha hizo, Meneja wa tawi hilo, Geoffrey Kitundu, alisema msaada huo umetokana na benki kuguswa na tukio hilo lililoathiri maendeleo ya kibiashara ya wanawake hao.

  Alisema katika tukio hilo, wanawake hao waliokuwa wakijishughulisha kwa biashara mbalimbali, walipoteza mali zao na hivyo kurudi nyuma katika jitihada zao za kujikomboa kiuchumi.

  Meneja huyo alisema hali hiyo, iliulazimisha uongozi wa benki kufikiria namna ya kuwasaidia wanawake hao, ili angalau warejee katika hali ya kawaida katika uendesha biashara zao

  “Tulipokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kuungua kwa Soko la Sido na tukaahidi kwamba tungeungana na taasisi zingine kuwasaidia wanawake walioathiriwa na sasa tunatimiza ahadi yetu kwa kutoa mchango huu,” alisema Kitundu.

  Kitundu alisema benki yake ina mpango maalumu ya kuwakomboa wanamke na kwamba hiyo inatokana na kuthamini mchango wao mkubwa katika kuinua uchumi wa taifa.

  Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Evans Balama aliushukuru uongozi wa benki hiyo kwa kutimiza ahadi ya kuwasaidia wafanyabiashara hao na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano.

  “Desemba mwaka jana nilikuja kutembelea Soko la Sido baada ya kupata taarifa kuwa limeungua. Katika soko hilo nilikutana na watalaam wa benki ya Exim ambao waliahidi kutusaidia na nashukuru kwamba leo (juzi) wametimiza ahadi hiyo,” alisema.

  Mkuu huyo wa mkoa, alielezea matumaini yake kuwa fedha hizo zitasaidia kuwawezesha wanawake kupiga hatua moja mbele katika jitihada zao za kujikomboa.

  “Nawasihi wananake kuzitumia fedha hizi vizuri ili kuendeleza biashara zao na si vinginevyo,” alisema Balama.
  Balama aliwasii mawanawake hao kukopa na kurejesha mikopo kwa wakati muafaka ili waendeshe biashara zao kwa ufanisi.:lol:
   
 2. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  mbona naziona hizo hela ndogo sana?anyway tuwashukuru kwa moyo wao mzuri.Mungu awabariki
   
Loading...